Muimbaji Issa Kijoti ni miongoni mwa waliofariki dunia katika ajali hiyo
Habari za kuaminika tulizopata usiku huu kutokea Mkoa wa Pwani kuwa kikundi cha Taraab cha Five Stars Modern kimepata ajali mbaya kikiwa kinatokea Songea Mkoa wa Ruvuma kuelekea jijini Dar kwa shuhuli zake za Taarab
Ajali hiyo imetokea Mikumi -Morogoro ambapo Bus lao la abiria la Toyota Coaster kuligonga lori lililokuwa limeharibika limeegeshwa bara barani na kupinduka inasemekana watu wanane wamekufa hapo hapo na wengine wawili wamekufa njiani kuelekea Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani na wengine wameumia na hali zao ni mbaya sana Bus hilo lilokuwa limepakia wanamuziki 22 Habari zaidi tutawaletea baadae
No comments:
Post a Comment