Monday, 14 March 2011


CCM yamtabiria Slaa urais

*Yadai CHADEMA ilichangia mauaji Arusha
Na Anneth Kagenda,Temeke

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, aendelee kufanya mazoezi ya kuingia Ikulu kwani huenda baada ya miaka
50 ijayo atanyakua nafasi hiyo.Pia kimeitaka Serikali kuacha kumtafuta mchawi katika tukio la mauaji lililotokana na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha na badala yake iwakamate viongozi wa juu wa chama hicho akidai kuwa wamekuwa wachochezi wakuu wa kuvuruga amani nchini.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Gugunita, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Temeke Mwembe Yanga wakati akijibu hoja mbalimbali zinazohusu chama hicho.

Amesema Dk. Slaa aendelee kuhangaika kutafuta urais labda huenda ipo siku Mungu atamuona na kumbarikia urais.

Amesema kama wao walijiona ni ‘ngangari’ kwanini hawakuingia kituoni kuchukua silaha na badala yake waliwashinikiza wananchi.

“Naunga mkono kauli ya waziri Mizengo Pinda bungeni kwamba CHADEMA ndio waliosababisha vurugu na vifo vya watu na hii ni kutokana na kukosa hoja ya kuing'oa CCM madarakani na badala yake wanatangaza udini makanisani eti mchague Wakristo ndio wenye hoja za msingi,” amesema Gugunita.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Ramadhan Madabida, amesema mfanyabiashara atakayepandisha bei ya sukari zaidi ya sh. 1,700 atanyang'anywa leseni yake ya biashara.

No comments:

Post a Comment