Wakurugenzi Wengine Wateuliwa Zaidi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Walioteuliwa ni Ayoub Mohammed Mahmoud ambae anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti wakati Fatma Ali Suleiman, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
Wengine ni Ramadhan Mussa Bakari anaekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi, Abdalla Ali Mwinyigogo, Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba, January Honoratus Fusi ambae anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi na Usajili na Mohammad Juma Muhammad ambae ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipangomiji/Vijijini.
Aidha Dk. Shein amewateua Mohamed Abdulla Khamis kuwa Mkurugenzi Idara ya Nishati, Issa Sarboko Makarani, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wakati Dk. Mustafa Ali Garu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji.
Kwa upande wake Hassan Ali Mbarouk ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme na Hemed Salim Hemed anakuwa Ofisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Pemba.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza Februari 23.

No comments:
Post a Comment