TANZANIA YAAHIDI KUWAREJESHA RAIA WAKE WALIOKO LIBYA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akitoa taarifa ya ziara ya Rais Kikwete nchini Ivory Coast katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi.
Jopo la Marais watano kutoka katika nchi tano za Africa wanaosuluisha mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast wamekubaliana kutoa taarifa kamili ya hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo mwishoni mwezi huu.
Akitoa taarifa ya ziara ya Rais Kikwete aliyoifanya nchini Ivory Coast hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amesema viongozi hao wamekubaliana kukutana baada ya siku tatu na baraza la la amani la (AU) na kutoa mapendekezo yao ili viongozi hao wachukue hatua kabla ya tamko la Umoja wa Mataifa.
Amesema nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kukumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Waziri Membe amekutana na Balozi wa Libya nchini na kuzungumzia kuhusu hali ya Watanzania wanaoishi nchini humo huku kukiwa na machafuko ya kisiasa ambapo ameahidi kuwarejesha watanzania wanaaoishi nchini humo mpaka pale hali ya utulivu itakaporejea nchini humo.
Membe amebainisha kuwa nchi ya Libya haina watanzania wengi ambapo amesema watanzania wapatao 28 ndio walioko nchini humo wakiwamo wanafunzi 22 pamoja na wananchi wa kawaida 6.
Baadhi ya waandishi wa Habari katika mkutano na Waziri Membe.
No comments:
Post a Comment