Tuesday, 22 February 2011

Misaada zaidi yamiminika kwa ajili ya waathirika wa Mabomu


Spika wa Bunge Mhe Anna Makinda akikabidhi Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Utaratibu na Bunge Mhe William Lukuvi hundi ya Tshs  millioni 37,80
 leo hii kwenye kituo cha kupokea misaada ya walio athirika na mabomu,
Fedha hizo zimetolewa na Wabunge kwa kuwasaidia Wananchi walio athirika
 na mabomu Na kulia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar er saalam Mhe Said Mecky Sadiq


Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam msaada wa vyakula vyenye thamani ya shs milioni moja na laki nane
Kulia ni Mkuu wa Wilaya Ilala Mhe Leonidas Gama na kushoto  Mkuu wa Wila ya Kinondoni
Mhe Jordan Lugimbana

Mwenyekiti wa CUF  Prof Ibrahim Haruna Lipumba akibeba kipolo cha Unga
 kwa ajili ya kukabithi msaada kwa waathirika wa maafa ya Gongola mboto
yaliyo tolewa na chama chake.





Naibu Katibu Mkuu wa chadema Mhe Victor Kimesela akikabidhi msaada
wa mashuka 166 kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Ukonga



Wake wa viongozi wakiwakilisha misaada kwa niaba ya wake wa viongozi wenzao
kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa walio athirika na mabomu
 kutoka kulia  kamanda wa kanda maalum  wa Dar es salaam
Suleiman Kova na kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe Sadiq Mke wa Waziri Mkuu
Tunu Pinda na Mke wa Makamo wa Rais Asha Bilal

No comments:

Post a Comment