
| Na Mwandishi Wetu,Jijini DAWA zinazopunguza makali ya ukimwi (ARV) zinazotumika kunenepesha kuku wa kisasa na nguruwe zimedaiwa kuwa zina madhara kwa wagonjwa wa UKIMWI ambao hutumia nyama hizo.Hayo yalisemwa na mtaalamu wa UKIMWI kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Mkundi Shayo, katika kipindi cha usiku wa habari kinachorushwa hewani na Televisheni ya Taifa ya (TBC1). Dk. Shayo amesema amepata taarifa kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia dawa hizo wakijali maslahi yao binafsi bila kujali madhara yanayowapata waathirika wa UKIMWI. “Wafanyabishara wengi wanatumia dawa hizo zinazoweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu ili mifugo yao ikue haraka,” amesema Dkt.Shayo. Amesema kitendo kinachotumiwa na wafanyabishara hao kinasikitisha kwa kuwa kinahatarisha maisha ya walaji wa bidhaa hiyo. Mwanaharakati wa UKIMWI kutoka Manispaa ya Ilala, Johnson Vigelo, amewataka wafugaji hao kuacha kutumia dawa hizo kwa ajili ya virutubisho vya mifugo yao badala yake watafute dawa mbadala. |
No comments:
Post a Comment