| Monday, 13 December 2010 09:27 |
| Na Waandishi Wetu, jijini JESHI la Polisi limepatwa na mshangao baada ya kulinasa jambazi sugu lililokuwa likitumikia kifungo cha miaka 60 jela likiwa uraiani likijihusisha na ujambazi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema jambazi hilo pamoja na wenzake walinaswa jana baada yapurukushani ya kufukuza na polisi katika kona mbalimbali za jiji wakati wakijiandaa kufanya uhalifu. Mtuhumiwa huyo (jina linahifadhiwa) pamoja wenzake wawili walinaswa na polisi Buguruni Relini baada ya kufukuzana na polisi wakitokea Mbezi-Mwenge na Barabara ya Mandela - Buguruni Relini ndipo walipokamatiwa ambapo gari lao lilipinduka wakati wakiendesha mwendo kasi kuwakimbia polisi. Majambazi hayo yalichomoka ndani ya gari hilo kisha kuanza kutimua mbio ambapo kikosi maalumu cha polisi cha kupambana na uhalifu kilifanya jitihada za kuwanasa watuhumiwa watatu wakiwa na majeraha pamoja na bunduki mbili ikiwamo ile aliyoporwa askari Polisi aliyekuwa lindo Benki ya Akiba Mwananyala, Kinondoni. Baada ya kuwanasa watuhumiwa hao, walikwenda kwenye gari lao na kuifuma SMG namba 00430 ikiwa na risasi 29 ambayo moja imetumika, pia walikuta silaha nyingine aina ya Mark IV ikiwa na risasi 13, pia walinasa simu nane zilizoporwa, kadi za benki, risasi moja aina ya shot-gun, begi jekundu na raba moja. Majambazi hayo yalikuwa yakitafutwa muda mrefu. Mmoja wa majambazi hayo ni yule ambaye mwaka 2003 alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela. “Tunajiuliza bado hili jambazi moja limetokaje (gerezani). Tunafanya uchunguzi kufahamu jinsi lilivyotoka na majina yao tunayahifadhi kwa uchunguzi zaidi,” amesema Kamanda Kova. Amesema tangu kuibwa kwa bunduki hiyo, jeshi la polisi lilifanya upelelezi wa kina ambapo ndani ya saa 29 wamefanikiwa kuyanasa majambazi hayo ambayo yamekiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu. Ameongeza kuwa majambazi hao walipora silaha hiyo Desemba 10, mwaka huu, saa 2 usiku, baada ya kumpora PC Fikiri aliyekuwa lindoni katika benki ya Akiba, Mwananyamala, ambapo jana saa 9 usiku, waliwanasa majambazi hao wakiwa na silaha hiyo. “Nawapongeza sana askari wangu waliokesha usiku na mchana kuwasaka wahalifu na kufanikiwa kuinasa silaha hii ambayo ilikuwa ikitumika mitaani,” amesema Kamanda Kova. Amewaomba raia wema kushirikiana na Polisi kutoa taarifa za siri zitakazosaidia kuwanasa wahalifu na kutokomeza vitendo hivyo nchini. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Monday, 13 December 2010
Polisi wanasa majambazi sugu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment