Monday, 6 December 2010

Ndege yaparamia miti, yaua watu wawili yajeruhi 90

 
Monday, 06 December 2010 09:06


Ndege ya abiria ikiwa imeanguka
















MOSCOW, Urusi
NDEGE ya Shirika la ndege la Dagastan nchini Urusi imeua watu wawili na kujeruhi watu zaidi ya 90 wakati ilipokuwa ikitua kwa dharura katika uwanja wa ndege mjini Moscow.
Habari zinasema kuwa, ndege  hiyo  ilikuwa  hewani  kwa  dakika  30  wakati injini  zote  tatu  ya ndege hiyo ziliposhindwa  kufanyakazi, pamoja  na  mfumo  wa kuongoza  ndege.
Picha  zinaonyesha   ndege  hiyo  ikiwa imevunjika  vipande  vitatu,  baada  ya  kutoka    katika  njia  yake na  kuparamia miti na kusababisha mauaji hayo.
Habari zinasema kuwa, ndege  hiyo  ilikuwa  na  abiria  171,  na 87  kati  yao  wamepelekwa  hospitalini mjini Moscow kwa uhangalizi zaidi wa afya za abiria hao.
Ajali za ndege zinaendelea kutokea sehemu mbalimbali za dunia hii inatokana mud mwingine uzembe kutokea kwa kutokufanya ukaguzi wa kutosha kabla ya ndege hizo kufanya safari.
Mwezi Julai mwaka huu, Ndege ya abiria imeanguka huko Islamabad, mji mkuu wa Pakistan na kuua watu wote 152 waliokuwa ndani yake.
Ndege hiyo, iliyokuwa katika safari kutoka Karachi kwenda Islamabad inaendeshwa na kampuni binafsi ya Airblue, ilianguka kwenye vilima vilivyoko kaskazini mwa jiji wakati ikijiandaa kutua.
Televisheni za Pakistan zilionyesha picha za mabaki ya ndege yakiwaka moto, huku helikopta za uokoaji zikiranda juu.
Airblue ndiyo kampuni kubwa zaidi ya ndege binafsi, miongoni mwa mashirika yaliyoibuka nchini Pakistan katika miaka ya karibuni.
Kampuni hiyo na idara ya usimamizi wa safari za anga hawadhani ndege hiyo ilikutwa na matatizo ya kiufundi wakati ikiondoka Karachi.rr
Wanasema hapakuwa na dalili za hitilafu ya kiufundi katika mawasiliano kati ya rubani na mnara wa kuongozea ndege wa Karachi.
Habari zinasema kuwa, ndege mbili zilizokuwa zitue kwenye mji huo mkuu zilikataliwa kabla ya ajali hiyo ya Airblue, katika ajali kubwa zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Pakistan.
Ingawa sekta ya safari za anga imekuwa kwa kasi, wakosoaji wanasema viwango vimekuwa chini na haviendani na ukuaji wa huduma.
Marubani hulalamika wanalazimishwa kuruerdxeka kwa saa za ziada, jambo linalosababisha uchovu, ingawa mashirika ya ndege yanakana madai hayo.
REUTERS

No comments:

Post a Comment