Saturday, 25 December 2010

Magari ‘tinted’ yakamatwa Z’bar




na Mwandishi wetu, Zanzibar
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Usafiri na Leseni, wameanzisha ukaguzi wa magari mabovu na yenye vioo vya giza (Tinted) na kuyachukulia hatua.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Kanda ya Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Makame Ali Makame na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Magari Zanzibar, Suluiman Mbarouk Salum, walisema jana kuwa magari 118 yamekamatwa na mengi kati ya hayo yalikuwa yamebandikwa vioo vya giza.
Wakizungumzia ukamataji huo wa magari yenye vioo vya giza baadhi ya wananchi wamepongeza mpango huo na kusema zoezi hilo likitekelezwa vizuri, litasaidia kupunguza uhalifu na maasi mengine yakiwemo ya ngono uzembe.
Wananchi hao, Ali Selemani, Mohammed Hamis Hamadi na Salum Juma Abeid, wakazi wa Zanzibar, wasema wahalifu wengi wamekuwa wakitumia magari yenye vioo vya giza na pia baadhi ya wamiliki ama madereva wa magari yenye vioo vya giza wamekuwa wakifanyia vitendo vya ngono uzembe.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limekemea vikali na kupiga mafufuku magari ya abiria na mizigo kujaza kupita uwezo wake na kusema dereva atakayekamatwa kwenda kinyume na agizo hilo atafungiwa leseni yake pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kamanda Makame amesema ujazaji huo ni wa hatari na ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kila atakayebainika kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment