Picha Balozi wa Ingunn Klepsvik wa Norway akiwasilisha Hati na Efracia Massawe |
MABALOZI wawili kutoka nchi za Norway na Sweden jana waliwasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Jakaya Kikwete na kusisitiza uwepo wa ushirikiano baina ya nchi zao na Tanzania. Mabalozi hao pia walipongeza hatua iliyopigwa visiwani Zanzibar kwa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kufikiwa kwa muafaka baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). Katika uwasilishaji wa hati hizo, Balozi Lennarth Hjelmaker wa Sweden alikuwa wa kwanza akifuatiwa na Balozi Ingunn Klepsvik wa Norway, lakini wote kwa pamoja katika mazungumzo yao walisisitiza uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa nchi ya Sweden kwa shambulio la mabomu ya kigaidi lililotokea mji mkuu wa nchi hiyo Stockholm hivi karibuni. |
No comments:
Post a Comment