RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amekuwa akisitasita kuwaapisha majaji wanne aliowateuwa Novemba 29 mwaka huu kufuatia barua aliyoandikiwa na Chama Cha Mawakili Zanzibar (ZLS) juu ya uteuzi huo kutozingatia taratibu.
Kusita huko kwa Dk Shein kuwaapisha tangu awateuwe kunaelezwa kuwa kunatokana na utata wa kisheria uliopo kutokana na majaji hao kutoiva vya kutosha katika taaluma ya sheria na kwa mujibu wa sheria tume ya utumishi ilipaswa kukaa kuidhinisha majina hayo jambo ambalo halikufanywa kwa baadhi ya majaji walioteuliwa.
Baadhi ya mawakilishi wakiongozwa na rais wa chama cha mawakili zanzibar, Yahya Khamis Hamad waliosaini barua ya kumpinga Dk Shein juu ya uteuzi wa majaji hao ambao kwa mujibu wa maelezo yao hawana sifa zinazowafanya wawe majaji wa mahakama kuu.
Rais wa Zanzibar kwa mamkala aliyopewa alifanya uteuzi wa majaji wanne wa Mahkama Kuu pamoja na Mwenyekiti wa Mahkama ya Ardhi ambaye ni Haroub Sheikh Pandu, na majaji wanne wa mahakama kuu akiwemo Abdul-hakim Ameir Issa, Fatma Hamid Mahmoud, Mkusa Isaac Sepetu, na Rabia Hussein Mohammed.
Chama hicho kilisema uteuzi huo, ulikuwa unatumia mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Zanzibar, 1984 kifungu cha 94(2) na (3) ambapo Chama cha Mawakili hakina mashaka na uteuzi wa Abdul-hakim Ameir Issa, wala uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahkama ya Ardhi, Haroub Shehe Pandu isipokuwa mashaka yapo kwa Fatma ambaye ni mtoto wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mkusa Isaac Sepetu na Rabia Hussein Mohammed ambao wote watatu wanadaiwa kutokuwa na sifa zinazostahiki kuteuliwa nafasi hiyo.
Aidha chama hicho kimesema kwamba Rais binafsi hawezi kuwaelewa majaji wala hakuna sababu ya kumjuwa yeyote katika Majaji wanne aliowateua ila wanachoamini uteuzi wake unatokana na ushauri uliopewa na Tume ya Utumishi ya Mahkama iliyoanzishwa chini ya Sheria Namba 13 ya mwaka 2003 ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid pamoja na wasaidizi wa rais wengine katika sekta ya sheria.
Juzi disemba 3 usiku Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud aliitisha kikao cha tume ya utumishi ambacho anadaiwa kuwa hakikupitisha jina moja la jaji aliyeteuwa na mawakili hao ili wajadiliane lakini kikao hicho kilishindwa kufanyika baada ya kupokea barua nyengine kutoka chama cha mawakilishi kusema kwamba kikao kitakachofanyika hakitokuwa halali kwa mujibu wa sheria kwa kuwa wajumbe wa kikao hicho hawakutimia.
Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na katibu wa chama cha mawakili, Salim Mkonje iliyotumwa kwa rais wa Zanzibar ya Desemba 3 mwaka huu, ambayo tayari saini ya rais inaonesha ameshaipokea ilisema kwamba wakili Awadh Ali Said ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya uajiri anayetokana na chama hicho katika vipindi viwili vimekwisha tokea septemba 17 mwaka huu hivyo hawezi kuwa mjumbe tena hadi hapo atakapoteuliwa tena.
Mbali na mjumbe huyo lakini pia Jaji Mshibe Ali Bakari naye muda wake umekwisha kwa mujibu wa sheria ya tume hiyo No 13 ya mwaka 2003 koramu ni wajumbe watano kifungu cha 9(2).
“Kufutia kikwazo hiki wakili Awadh alifahamishwa na katibu wa tume ya uajiri ya mahakama asihudhurie kikao cha leo 3 Desemba jana usiku” ilisema barua hiyo kutoka kwa mawakili. Na kuongeza kwamba.
“kwa sababu wajumbe waliokuwepo walikuwa sita hivyo kupungua kwa wajumbe wawili kunapelekea tume isiweze kufanya maamuzi kama sheria inavyotaka kwani yatakuwa batili kwa kukosekana koram” alisema barua hiyo.
Aidha chama hicho kimeitisha kikao chake jana kuteuwa jina la wakili ambaye atakiwakilisha chama hicho na kulipeleka kwa rais ili ateuliwe kuingia katika kikao hicho ikiwa pamoja na wajumbe wengine ambao sheria inasema tume hiyo iwe na wajumbe wanane akiwemo jaji mkuu, mwanasheria mkuu na mwenyekiti wa tume ya utumishi, na kadhi mkuu.
Wengine ni wakilishi anayetoka chama cha mawakili, jaji wa mahakama ambaye anaendelea na kazi ya ujaji, jaji mstaafu, na mtu yeyote atakayeonekana anafaa na rais.
Licha ya kuwa hakuna sheria inayompa muda rais kuwaapisha wateule hao lakini sio jambo la kawaida kwa uteuzi unaofanywa na rais halafu ikafika wiki nzima wateule wakawa hawajaapisha hasa kwa kuzingatia utaratibu uliozoeleka ni kulishwa viapo mara tu baada ya uteuzi.
Katika barua yao kwa Rais mawakili hao walisema “Mhe.Rais, wateule wa Ujaji tuliowataja hapo juu, hawatokuwa Majaji rasmi Kikatiba na kuanza kazi ya Ujaji wa Mahkama Kuu mpaka baada ya kula kiapo. Hilo likishafanyika, itakuwa dhiki sana kuondosha uteuzi huo. Hivyo, tunakuomba Mhe. Rais, utafakari upya juu ya uteuzi huo na uridhike kuusitisha” walisema Mawakilishi hao.
Hata hivyo inaoenkana Dk Shein amekuwa mwangalifu kufuatia kadhia hiyo na amekuwa akitafakari juu ya kuwalisha viapo majaji hao wanne ambao wanadaiwa kutokuwa na vigezo vya nyadhifa hizo.
Akizungumza na kituo kimoja cha radio nchini hapa, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu alisema Mawakili wana haki ya kupinga kama wanaona kitu hakikukaa sawa lakini watoe sababu nzuri za kupinga sio za kurusharusha.
“Nimesoma barua yao lakini ina mashaka barua waliyoandika ni ya watu 11 waliotia saini ni watu sita inawezekana hasa siya tasisi kwani walikuwa wanapinga wale majaji wanne lakini kuna ishara nyengine ya kumpinga jaji mkuu kuwepo kwake naona hizo ishara zimeingiliana” alisema Mwanasheria mkuu.
Hata hivyo Mwanasheria huyo alisema kwa kuwa mawakili wameandika barua kumpelekea rais basi rais mwenyewe ana maamuzi yake atakayoyafanya hivyo watu wasubiri waone namna gani mwenyewe rais atakavyoyashughulikia masuala hayo.
Kuhusiana na majaji hao kuteuliwa bila ya kufuatwa taratibu Mwanasheria huyo mkuu alisema “Ni kwamba majaji hayawezi kuteuliwa mpaka rais apate ushauri wa tume ya ushauri ya mahakama naona utaratibu umefuatwa. Kwa maoni yangu utaratibu umefuatwa hao waliopendekezwa walikuwa wanazo sifa lakini kila mmoja ana maoni yake wakati mwengine mtu wanatizama sifa lakini mtu mwengine anatizama kama mtu”.alisema.
Aliongeza pia “Mimi nadhani rais yeye atatumia busara yake na atazingatia na akitaka maoni kwa watu wengine yeye mwenyewe anajuwa utaratibu wake wa kuliendeleza hili suala” alimalizia mwanasheria huyo.
Kuna taarifa kwamba majaji hao wanatarajiwa kuapishwa leo ikulu mjini zanzibar ambapo baadhi ya maafisa wa ikulu wanasema majaji hao wataapishwa kwa mbwembwe kwa kuwa hawatavaa suti kama ilivyozoeleka lakini tayari wameshashonewa makoti ya kijaji ambayo watakwenda nao kula kiapo hapo ikulu.
kutoka Zanzibar Yetu

No comments:
Post a Comment