*Ni mkazi wa Kawe jijini D’Salaam * Aliuhifadhi kwenye ndoo na vidumu *Atolewa kwa ulinzi mkali wa polisi Na Neema Fredy, Kawe ZIKIWA zimesalia siku chache kumalizika kwa mwaka 2010, mwanamume mmoja (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Kawe jini Dar es Salaam ametoa kali ya mwaka baada ya kukutwa na lita 100 za mkojo chumbani kwake. Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi majira ya saa 4 asubuhi wakati mwenye nyumba aliyokuwa akiishi mwanamume huyo kwenda kumhamisha kwa nguvu akifuatana na wajumbe wa serikali ya Mtaa wa Ukwamani Kawe pamoja na polisi wa kituo cha Kawe baada ya kushindwa kulipa kodi. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo, Alhaji Abdul Risasi, baada ya kuingia kwenye chumba cha mwanamume huyo walipigwa na butwaa baada ya kuzikuta ndoo 4 za lita 20 kila moja zikiwa zimejaa mkojo na chupa 40 za nusu lita pamoja na bomba moja la sindano. Imedaiwa kuwa mwanamume huyo alikuwa anadaiwa kodi ya nyumba, kitu ambacho kilimsukuma mwenye nyumba hiyo, Seif Ally, kutoa taarifa serikali ya mtaa ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo. Hata hivyo, James alikiri kudaiwa fedha za kodi ya nyumba kiasi cha shilingi milioni mbili na nusu na aliahidi kuzilipa baada ya muda kwa kile alichodai kuwa hakuwa nazo kwa wakati ule. Pamoja na kukiri huko, mwanamume huyo hakutaka kuzungumzia suala la kukutwa na kiasi hicho cha mkojo.Awali james aliahidi kuwa angelipa deni hilo Desemba mosi mwaka huu 2010 kitu ambacho hakukitekeleza hadi alipotolewa kwa nguvu chini ya ulinzi wa Polisi. Imedaiwa kuwa mwanamume huyo baada ya kuona anadaiwa alikuwa akirudi usiku na wakati mwingine kuruka ukuta ili asionane na mwenye nyumba. Hata hivyo, mwanamume aliyekutwa na mkojo huo amedai kuwa ndani ya chumba chake kulikuwa na sh. milioni tano, madai ambayo yalithibitishwa kuwa sio ya kweli baada ya kukaa kikao cha pamoja kati yake na mwenye nyumba, Polisi na wajumbe wa serikali ya mtaa. Haijajulikana kwanini mwanamume huyo alikuwa amehifadhi mkojo mwingi kiasi hicho chumbani kwake, na pia haijulikani kwanini kulikuwa na mkojo tu lakini siyo na kinyesi pia. Haijajulikana pia mkojo huo umekusanywa kwa muda gani na kama ni wa kwake mwenyewe. Hata hivyo, mkojo huo haukuwa ukitoa harufu kutokana na yeye kufunika ndoo na vidumu hivyo. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Thursday, 16 December 2010
Akutwa na lita 100 za mkojo chumbani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment