Tuesday, 10 September 2013

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)Sasa Kuishataki kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30 Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.
 
 
 Meli ya Gold Star iiliyosajiliwa Tanzania ikiwaka moto baada ya mabaharia wake kuichoma iliponaswa ikiwa imebeba dawa za kulevya aina ya bangi katika pwani ya Italia juzi. Picha ya Reuters
 
 
Mkurugenzi wa Mamalaka ya usafiri Zanzibar (ZMA) Abdi Omar Maalim akionyesha fomu za mashariti ya usajili wa meli kufuatia kukamatwa kwa meli ya MV Gold Star ikiwa na tani 30 za bangi meli hiyo imesajiliwa Zanzibar mwaka 2011.Picha na Mwinyi Sadallah  
----
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itafungua mashtaka dhidi ya kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30 Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.

Hatua hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, alipozungumza ofisini kwake Mlandege Zanzibar, jana.
Maalim alisema kwa mujbu wa sheria namba 5 ya mwaka 2006 ya usafiri baharini, kampuni hiyo imekiuka masharti ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba silaha, dawa za kulevya, wakimbizi au mzigo wowote wenye biashara haramu.
Alisema wanasheria wa ZMA wataipitia sheria hiyo kabla ya kuamua kuishtaki kampuni hiyo mabaharia tisa wanaodaiwa kula njma za kusafirisha bangi, kabla ya kukamatwa huko Italia.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......>>>>>
 
Kamishna wa Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa akizihesabu kete 43 za dawa za kulevya aina ya Heroin jana, zilizokamatwa katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, juzi usiku ambapo zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Japan. Picha na Michael Jamson  
----
  Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.

Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.Kwa Habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>>
 

No comments:

Post a Comment