Monday, 9 September 2013

JUSSA:BALOZI SEIF HUNA SIFA ZAKUWA MAKAMO WA RAIS JIUZULU
Wananchi wa Zanzibar kwa umoja wao wametakiwa kutokata tama tena bila kurudi nyuma katika harakati zakuitafutia Zanzibar mamlaka yake.

Mhe. Ismail Jussa.

Kauli hio imesemwa na Mkurugenzi wa haki za binadmu,habari uenezi na mawasiliano ya umma wakati alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchama wa chama cha wananchi CUF pamoja na wazanzibar wanaopenda mamlaka kamili ya nchi yao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Basra jimbo la Mtoni na jumala ya wananchama hamsini wapya kukabidhiwa kadi.

Alisema kuwa anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wajumbe wa kambi ya upinzani bungeni kwa kukataa kwao kuupitiasha swaada juu ya katiba mpya kwa kutokana kutokushirikishwa wazanzibar katika mchako huo,pia amezipongeza jumuia na asasi mbali za kiraia zilizopo Zanzibar kutokana na kauli yao ya kutaka kushirikishwa katika mchakato wa katiba mpya ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama zilivoshirikishwa jumuia nyengine kwa upande wa Tanzania bara.

Pia alimtaka Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhakikisha kuwa hatii saini ya kukubali mswaada huo mpaka pale wazanzibar ambao ni miongoni mwa wahusika wakuu wa muungano huu uliopo wameshirikishwa tena kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na hayo pia alivitaka vyombo vya dola kuhakikisha wanasimamia amani ya nchi kwa kuwadhibiti wale wote ambao lengo lao nikuichafua amani ya nchi iliopo hivi sasa.

Kashfa mbali mbali zinatolewa pamoja na uchochezi unafanywa hadharani ili wazanzibar waliowengi wachokozeke na hatimae kutoka kwenye lengo letu la kudai mamlaka kamili ya Zanzibar wakati haya yanafanyika Polisi pia wananshudia lakini waanachia’’alieleza.
 
Aidha alieleza kwamba sula la Mbunge wa jimbo la Donge ambae pia ni Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM Mh,Sadifa kuishusha na kuichana hadharani bendera ya CUF watahakikisha wanalifuatilia kwa kina na hatimae kumfikisha mahakamani na wataitaka mahaka pamoja na vyombo husika kuhakikisha hatua za kishgeria zinachukuliwa dhidi yake.

Nae Mgeni rasmi katika mkutano huo ambae ni Muakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe na mjumbe wa baraza kuu Taifa CUF Mh,Ismail Jussa Ladhu amewataka vijana kwa wazee kutokurudi nyuma kwa hapa tulipofika hadi pale Zanzibar ipakapokuwa na mamlaka yake kamili.

Amesema kuwa wananchi wa Zanzibar hawatopokea lolote lile kutoka katika tume ya Warioboga isipokuwa mamlaka kamili kwani anaamini kuwa ndio maoni ya wazanzibar waliowengi waliotoa katika tume ya warioba hivo basi chochote kile kisichokuwa mamlaka kamili basi watakirudisha kwa tume hio.

Alieza kuwa hata ukiwepo huo Muungano basi tume hio ihakikishe kwamba mambo yote ya muungano ambayo yatakuwa ni machache mno basi yawe na usawa wa pande zote mbili ziulizounda muungano huo nazo ni Zanziobar na Tanganyika na isiwe upande mmoja umemzidi mwenzake kama ilivo hivi sasa.

Akifafanua kuhusu muundo wa baraza la Mawaziri Mh, Jussa ameleza baraza la mawaziri hilo la muungano lisizidi mawaziri sita tena wawe na usawa Zanziba watoke watatu na Tanganyika watatu lakini kinyume na hayo hawatokubaliana na muundo huo.

Alisema kitendo kilichofanywa na Balozi Seif kuwasema wazanzibar Bungeni yakuwa wazanzibar wamekubali kupitishwa kwa mswaada huo sio jambo lakiungwana kwani wazanzibar wenyewe wapo na walipaswa kusema wenyewe na sio kusemewe kufanya kwake hivi nidhahiri kuwa hana nia njema na Zanzibar na kuna kila haja wazanzibar kumpiga vita.

Amesahau kama alikula kiapo mara mbili wakati akiapishwa Ikulu aliapa kuwa atailinda na kuitetea katiba ya Zanzibar sasa leo anafanya nini kama sio kukiuka kiapo unadhani ni nini hafai kabisa na hana sifa ya kuwa Makamo wa Raisi ajiuzulu’’alieleza Jussa.

Pamoja na hayo alisema kwamba katika watu ambao hawana tofauti katika suala lakuikandamiza Nchi basi ni Mh,Mizengo pinda pamoja na Balozi Seif na lengo lao nikuwahakikisha kuwa wamewatoa wazanzibar katika point ya kudai mamlaka yao.

Aidha Bwana Jussa alitoa wito kwa wazanzibar wote kuwa kutokana na hatuwa waliofikia ya kudai mamlaka kamili basi hawana budi kuzidi wakihakikisha kuwa hakuna mtu ambae atachokozeka kwa lolote lile hadi pale Zanzibar itakapopata mamlaka yake.

No comments:

Post a Comment