BAADHI YA TASWIRA ZA BUNGENI LEO MJINI DODOMA NA VURUGU ZILIZOTOKEA
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi akiteta na Mwanaheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi akifafanua jambo Bungeni Mjini Dodoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Bumbumbuli na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, Bungeni Mjini Dodoma
Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini ,
Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)











No comments:
Post a Comment