Monday, 19 August 2013

SHEIKH PONDA APANDISHWA MAHAKAMANI MJINI MOROGORO LEO NA KUSOMEWA MASHTAKA MATATU





Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa mahakamani wakati akisomewa mashtaka



Sheikh Ponda Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi  tarehe 28.08.2013



Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo 


Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu ambapo inadaiwa alisema kwamba ”Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ”katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro. Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilika na  Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..

No comments:

Post a Comment