Wednesday, 26 June 2013

Obama ziarani barani Afrika, ambapo atazuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania

Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ndefu barani Afrika, ambapo anaondoka leo katika kituo cha Andrews kilicho katika viunga vya jiji la Washington akiambatana na familia yake. 

Raia wa Marekani Barack Obama,na mkewe Michelle Obama
Photo: CHUCK BURTON/AP

Kwenye ratiba ya ziara hiyo inayoanza Juni 26 hadi Julay 3 ambapo hatuwa ya kwanza ni huko Senegal ambako atakutana kwa mazungumzo na rais Macky Sall na baadae atatembelea kisiwa cha Goree, kilichokuwa kinatumiwa kuwapokea watumwa. 

Baada ya hapo rais Obama ataelekea jijini Johannesbourg nchini Afrika Kusini Juni 29 ambako atakutana na rais Jacob Zuma jijini Pretoria kabla ya kutamatisha ziaqra yake nchini Tanzania ambako atakutana na rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuzuru kituo cha umeme cha Ubungo.

Hata hivyo hali ya afya ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambae anaelekea kutimiza miaka 95 na ambaye amelazwa Hospitalini takriban majuma matatu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya mapafu, huenda yakapangua agenda hiyo ya ziara ya rais Obama.

Kumekuwa na uvumi mkubwa kuhusu kurekebishwa kwa ratiba hiyo au kusitishwa kabisa iwapo kutatokea taarifa ya kufariki kwa kinara wa zamani wa Afrika Kusini na mtetezi wa ubaguzi wa rangi.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Maite Nkoane Mashebane amethibitisha jana kwamba rais wa Marekani hatokutana na Mandela, ambapo rais Obama alipenda kumuona kinara huyo wa zamani, lakini hali yake ilivyo hairuhusu.

Barack Obama alikutana na Mandela kwa mara ya mwisho mwaka 2005 wakati alikuwa bado ni seneta.

Kukoa muda uliopotea ziara hii ya kwanza kubwa barani Afrika kwa rais wa Marekani inalenga kwanza kuokowa muda ulipotea.

Mbali na ziara iliofanywa na rais huyo nchini Ghana Julay mwaka 2009, hakuwa kutembelea sehemu nyingine barani Afrika katika muhula wake wa kwanza
Ukiachia matumaini ya siku za mwanzo, watu wa Afrika wameanza kukata tamaa juu ya hatua zilizochukuliwa na rais wa kwanza mweusi katika historia ya Marekani.

Kama mwaka 2009 nchini Ghana, Obama ilizindua "damu ya Afrika katika mishipa yangu, historia ya familia yangu ni pamoja na maafa na vilevile ushindi wa hadithi kuu ya Afrika" Rais alionekana kulipa mgongo bara lake asilia na badala yake Kulenga mgogoro wa kiuchumi, mapinduzi katika nchi za kiarabu, kutamatisha operesheni za Marekani nchini Iraq na Afghanistan, na kuonekana kuangalia zaidi bara la Asia.

Lakini washauri wa rais wanaona kwamba kuna fursa za kiuchumi na rasilimali za nishati katika bara la Afrika ambazo zimeanza kuvutia kwa kiasi kikubwa wapinzani wa kiuchumi wa Marekani, hasa China.

Kulingana na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, China imekuwa katika mwaka 2009 mshirika wa kwanza wa bara la Afrika.

Katika ziara hiyo kubwa barani Afrika rais Obama hatotembelea nchini Kenya licha ya kuwa ndio chimbuko la baba yake, ambapo wadadisi wa mambo wanaonakuwa n kutokana na Uhuru Kenyatta rais wa Kenya, kushtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

No comments:

Post a Comment