Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA)Mh,Zitto Kabwe
---
Zitto Kabwe:'Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’.
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.Kusoma Zaidi Tamko la Zitto Kabwe Bofya na Endelea......>>>>>>
.Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kutokana na swala la kiusalama na kutoharibu upelelezi,kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutokea nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo Waandishi wa habari wakimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.(Picha na Full Shangwe Blog) KUNRADHI KWA PICHA HII: Dk. Steven Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo na kuokotwa huko Mabwepande.
Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:
Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku
wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------
Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.
Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.
Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.

No comments:
Post a Comment