

Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu,Hamad Masoud Na Nafisa Madai, WMM Zanzibar Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewasilisha ripoti ya usajili wa meli mbele ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi katika mkutano wa bajeti unaoendelea Mjini Zanzibar. Akiwasilisha ripoti hiyo, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud alisema kwamba Serikali imelazimika kutoa ripoti hiyo kuweka kumbukumbu sawa kuhusu madai yaliyochapishwa na kutangazwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na vile vya Kimataifa. Waziri Masoud alisema katika mojawapo ya taarifa za vyombo vya habari vilisema “Meli za mafuta za Iran zinatumia Bendera ya Tanzania kukwepa vikwazo”. “Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kuliarifu Baraza lako kwamba Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN”Aliliambia Baraza Waziri Masoud. Waziri huyo alisema Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imeundwa kwa mujibu wa sheria namba 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006. Alisema sheria hiyo katika kifungu cha 8(1) kinaeleza kutakuwa na Mrajis wa Meli Tanzania Zanzibar ambaye atasajili meli zinzofanya safari za nje na zile za ndani. Waziri Masoud aliwaambia Wajumbe kwamba Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. “Mheshimiwa Mwenyekiti Open Registry, Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.” Alisema Waziri huyo. Waziri Masoud alisema “SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo” Waziri amezitaja meli hiyo na Mataifa yao kwenye mabano kuwa ni Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd(, Malta)Justice164241Justice Shipping Co. Ltd (Cyprus), Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd( Malta) Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd ( Malta) Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd (Cyprus),Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd (Malta). Amezitaje nyengine ni Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd ( Malta) Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd ( Malta) ,Courage 163660 Courage Shipping Co. lt (Cyprus),Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd (Cyprus na valo160930 valor Shipping Co. Ltd.(Cyprus) Alisema Meli hizo ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration). Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”. Hata hivyo, alisema ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN. Waziri huyo alisema Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry). Alisema pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta. “Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi”Alisisitiza Waziri Masoud Aliongeza kwamba Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake.
|
No comments:
Post a Comment