WAZIRI wa Mambo ya Ndani Akutana na Viongozi wa Dini na Waandishi Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.
Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.
Viongozi wa Jumuiya za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena ikaharibu Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.
SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment