Na Gazeti la Nipashe: `Kiwanja alichopewa Mama Karume kirejeshwe serikalini`
![]() |
| Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume. |
Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayochunguza ubadhirifu wa mali za Serikali ya Zanzibar imeitaka serikali kurejesha kiwanja alichopewa kinyume na sheria, mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi kiwanja hicho namba 186 chenye mita za mraba 750 kipo katika mtaa wa Kinazini, mkabla na Jemgo la historia la Dk. David Livingstone, mjini Unguja.
Ripoti imeeleza kwamba kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kabla ya kupewa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) kujenga makao makuu yake.
Uchunguzi wa kamati umebaini kuwa ZRB baada ya kupewa uwanja huo walishindwa kuuendeleza baada ya kupata uwanja mwingine katika eneo la Mazizini na kujenga makao makuu yake na uwanja ulirejeshwa Wizara ya Ardhi.

Ripoti imesema Wizara ya Kilimo ilitoa kiwanja hicho kwa ZRB kupitia barua ya Agosti 28, 2002 yenye kumbukumbu WKMMU/29/5/41/72 kwenda Wizara ya Ardhi ya kuwapa ZRB. Uamuzi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili ulikubaliwa na Wizara ya Ardhi na kukabidhi uwanja kwa ZRB Septemba 9, 2002 kupitia barua yenye kumbukumbu namba MUNA/34/14/378/ VOl.1 na kutoa shahada ya haki ya matumizi ya ardhi ya Aprili 4, 2003.
Hata hivyo, ripoti imesema baada ya ZRB kupata sehemu nyingine ya kuendelea na ujenzi waliamua kukirejesha kiwanja hicho serikalini ambapo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Makazi,Maji na Nishati, Mansour Yussuf Himid, aliamua kiwanja hicho kumpatia mama yake Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mwaka 2010.
Akihojiwa na kamati hiyo Desemba 7, mwaka jana, Waziri Mansour, ambaye sasa ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum alikiri kiwanja hicho kumpa mama Fatma Karume baada ya kumuomba ili aweze kukitumia kwa shughuli zake za biashara ambazo hazijaelezwa.
Hata hivyo, kamati imesema baada ya Waziri Mansour kuhojiwa juu ya kukosekana kwa maombi ya wahusika, alisema yalikuwepo maombi ya kampuni ya F&K Enterpreses LTD katika faili maalum na alishangazwa na taarifa za kutoweka kwa nyaraka hizo.

No comments:
Post a Comment