Sunday, 15 April 2012



Inatolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 5(3) ya Nyongeza ya Pili ya Kanuni za Bunge Toleo la 2007)

                                         _______________________________

 1.0 Tarehe 9 Machi, 2012 nilitoa Tangazo kwa vyombo vya habari na gazeti la Serikali juu ya      kuwepo kwa nafasi Tisa wazi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kufuatia kufikia ukomo wa maisha ya Bunge la sasa hapo 04 Juni, 2012.Katika Tangazo hilo niliwaomba wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo wafanye mchakato wa kugombea kupitia vyama vyao vya Siasa na fomu za wagombea waliopendekezwa zirejeshwe Ofisi ya Bunge kabla ya saa 10.00 jioni tarehe 10 Aprili, 2012 ambayo ndiyo siku ya uteuzi. Jumla ya Wagombea 34 kutoka Vyama vya Siasa vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP na TADEA wamerudisha Fomu.

2.0 Zoezi la uteuzi limekamilika, Wajumbe 33 wametimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, hivyo, wameteuliwa kugombea nafasi hizo. Aidha, Mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya kuthibitisha uraia wake na kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 5(3) na 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge, hivyo hakuteuliwa kugombea.

Ifuatayo ni Orodha ya Wagombea walioteuliwa na wasioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki:-

1. WAGOMBEA WALIOTEULIWAKUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE
S/NO.JINACHAMA
1. Nd. Angela Charles Kizigha CCM
2. Nd. Fancy Haji Nkuhi CCM
3. Dkt. Godbertha Kokubanza Kinyondo CCM
4. Nd. Janet Deo Mmari CCM
5. Nd. Janet Zebedayo Mbene CCM
6. Nd. Maryam Ussi Yahya CCM
7. Nd. Rose Daudi Mwalusamba CUF
8. Nd. Sebtuu Mohamed Nassor CCM
9. Nd. Shy-Rose Sadruddin Bhanji CCM
10. Nd. Sofia Ali Rijaal CCM 


KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR


S/NO.JINACHAMA
1. Nd. Abdullah Ali Hassan Mwinyi CCM
2. Dkt. Ahmada Hamad Khatib CCM
3. Dkt. Haji Mwita Haji CCM
4. Nd. Khamis Jabir Makame CCM
5. Dkt. Said Gharib Bilal CCM
6. Nd. Zubeir Ali Maulid CCM 


KUNDI C: WAGOMBEA WA VYAMA VYA UPINZANI


S/NO.JINACHAMA
1. Nd. Antony Calist Komu CHADEMA
2. Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha UDP
4. Nd. Juju Martin Danda NCCR-MAGEUZI
5. Nd. Micah Elifuraha Mrindoko TLP
6. Nd. Mwaiseje S. Polisya NCCR-MAGEUZI
7. Nd. Nderakindo Perpetua Kessy NCCR- MAGEUZI
8. Nd. Twaha Issa Taslima CUF 


KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA


S/NO.JINACHAMA
1. Nd. Adam Omar Kimbisa CCM
2. Nd. Bernard Musomi Murunya CCM
3. Nd. Charles Makongoro Nyerere CCM
4. Dkt. Edmund Bernard Mndolwa CCM
5. Nd. Elibariki Immanuel Kingu CCM
6. Dkt. Evans Mujuni Rweikiza CCM
7. Nd. John Dunstan Lifa-Chipaka TADEA
8. Nd. Mrisho Mashaka Gambo CCM
9. Nd. Siraju Juma Kaboyonga CCM
10. Nd. William John Malecela CCM 


2. MGOMBEA AMBAYE HAKUTEULIWA

S/NO.JINACHAMA
1. Nd. Mohamed Abdulrahman Dedes CUF 

3.1 Hivyo, bila ya kuathiri shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge, tarehe 17 Aprili, 2012 saa Nne na nusu asubuhi au muda mfupi baada ya hapo nitawasilisha majina ya Wagombea kwa wapiga kura.

Napenda kutoa shukrani kwa Wagombea wote kwa ushirikiano wao katika kukamilisha zoezi hili la uteuzi. Aidha, tunawaomba wapiga kura, wakati utakapofika, wazingatie matakwa ya Sheria na Kanuni zinazotawala chaguzi hizi.

Imetolewa na:

Dkt. Thomas D. Kashililah  KATIBU WA BUNGE NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI BUNGENI DODOMA
14 APRILI, 2012

No comments:

Post a Comment