| Taji laenda Venezuela |
Ivian Sarcos akipunga mkono baada ya kutwaa taji la urembo la dunia, mashindano yaliyofanyika kwenye mji wa London, Nwishoni mwa wiki, Picha na AFP Mwandishi wetu na Mashirika VENEZUELA imeendelea kuweka historia ya ushindi katika sanaa ya urembo baada ya mlimbwende wake, Ivian Sarcos kutwaa taji la 'Miss World' usiku wa kuamkia Jumapili, huku Tanzania kwa mara ya sita mfululizo ikirudi nyumbani mikono mitupu kufuatia mrembo Salha Israeli kushindwa kutamba. Tanzania ambayo imeshiriki mfululizo mashindano ya urembo ya dunia tangu mwaka 1994, ni mwaka 2005 tu ilipoweka historia kwa upande wa Afrika baada ya mrembo Nancy Sumary kutwaa taji la 'Miss World Africa' Hii ni mara ya kwanza Venezula inatwaa taji hilo katika kipindi cha miaka 16 iliyopita, lakini likiwa taji la sita tangu mwaka 1951, na kuwa nchi pekee iliyotwaa mara nyingi. Shindano hilo lililowashirikisha zaidi ya warembo 100 kutoka nchi mbalimbali duniani, lilifanyika kwenye ukumbi wa Earls Court, mjini London, England. Philippines ambayo haijawahi kutwaa taji, mrembo wake Gwendoline Ruais alishika nafasi ya pili, huku mrembo wa Puerto Rico iliyowahi kutwaa taji mara moja, ikishika nafasi ya tatu kupitia mrembo wake Amanda Perez. Katika shindano hilo, Afrika ilifanikiwa kuingiza warembo wawili katika hatua ya 15-bora, ambao ni kutoka Zimbabwe (haijawahi kutwaa taji) na Afrika Kusini iliyotwaa taji mara mbili. |

No comments:
Post a Comment