Thursday, 3 November 2011


Mradi wa samaki wapiga hodi Zanzibar

 
UJUMBE KUTOKA ZANZIBAR ULIOWAKUSANYISHA WATAALAMU WA SEKTA MBALI MBALI UKIONGOZWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR; BALOZI SEIF ALI IDDI ULIPOKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA BIASHARA LA MAREKANI LINALOSHUGHULIKIA KANDA YA AFRIKA (USTR).

TAASISI ya Ushirikano ya Jimbo la Houston,Texas Nchini Marekani na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefikia hatua ya kukubaliana kufanya utafiti wa pamoja utakaopelekea kuanzishwa kwa Mradi mkubwa wa Samaki Zanzibar.Hatua hiyo ya makubaliano imekuja kufuatia Kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Zanzibar ulioko Nchini Marekani kujitanga kwa wawekezaji wa nchi hiyo ukiongoza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Taasisi inayoratibu Miradi mikubwa ya Samaki Nchini Marekani ya (GRI) ikiongozwa na Rais wa soko la Kimataifa la Taasisi hiyo Bw. Thomas Newland.
Mazungumzo hayo yamefanyika hapo katika Afisi za Taasisi hiyo kwenye Jimbo la Houston, Texas Nchini Marekani ambapo Bw. Thomas Newland aliueleza ujumbe huo wa Zanzibar kwamba mradi huo mkubwa una uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi zaidi ya thalathini elfu (30,000).
Alisema miradi kama hiyo ambayo tayari imeshaanzishwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika, Asia, Marekani na Ulaya inazingatia zaidi uhifadhi wa Mazingira pamoja na utoaji wa mafunzo kwa Wavuvi na Wakulima wa maeneo ya Vijijini.
“Miradi kama hii ambayo hufadhiliwa na Taasisi za Uwekezaji Vitega Uchumi za OPIC na IFC hugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 20,000,000’ amesema.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri kuharakishwa kwa mawasiliano ya pamoja kati ya wataalamu wa pande hizo mbili ili kuona wazo hilo la muelekeo wa kuanzishwa kwa mradi mkubwa wa Samaki linafanikiwa.
Balozi Seif alisema kuanzishwa kwa mradi huo mbali ya kuleta uhusiano wa karibu kati ya Zanzibar na Marekani lakini pia utaleta faraja kwa wananchi walio wengi kujipatia ajira ya uhakika.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikuwa na mazungumzo na Seneta wa Jimbo la Houston,Texas Bw. Rodey Ellis.
Katika mazungumzo yao Senata Rodney aliipongeza Zanzibar kwa juhudi zake za kuharaisha Maendeleo ya Kiuchumi. Seneta Rodney Ellis amemkabidhi Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake hati Maalum inayompa heshima ya kuwa mkaazi wa Jimbo la Houston, Texas.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/11/2011.

No comments:

Post a Comment