Monday, 7 November 2011

DIASPORA YA WAZANZIBAR YA SHEHEREKEA EID NCHINI MAREKANI.

Zanzibar Diaspora ya Marekani kwa delegation ya Makamu wa Rais iliongozwa na Waziri Fatama Ferej katika Mji wa Delaware Eid Lunch iliandaliwa na Wazanzibari wa Mji wa Delaware na Philadelphia kwa ushirikiano wa kuandaa tafrija hii

Waziri Bi Fatma Ferej Aliwashukuru na kuwapa ujumbe kuwa. Huu ndio Mwanzo wa mshikamano wa Wazanzibari aliouwaagiza Makamo wa Rais kuwataka Kila Mzanzibari alieko nje kuwa Balozi wa Zanzibar kitangaza Zanzibar , Balozi Seif EID Aliwataka Wazanzibari popote Duniani walipo waungane watafute maendeleo yao na bila ya kusahau nchi yao Zanzibar .

Mwenyekiti wa Diaspora ya Marekani Ustadh OMAR ALI na Secreatry Wake Shamis Abdulla pia walijumuika na Wazanzibari kwenye Sherehe hii Kuwakaribisha viongozi hao na Kina Dr Mohammed Adam na Dr Talib Ali na Engineer Salum Masoud na Bila ya Kuwasahau Kina Dada wengi waliofika na watoto wao.

 
Dr Mohamed Adam Dosi akimtambulisha Waziri kwa Wazanzibari na kwuaeleza Wazanzibari umuhimu wa Diaspora kwa faida yao na nchi yao kwa Ujumla mnufaa yake.

 
Baadhi ya Wazanzibari waliohudhuria kwenye tafrija hiyo iliofanyika Jana Jumapili Nov 6, 2011

 
Balozi Fatma akipata Picha ya pamoja na kina dada waliofika kujumuika nae Jana Jumapili Nov 6, 2011 ndani ya jimbo Delaware Nchini Marekani

 
Waziri Fatma na Ofisa Suleiman Wakifurahia machopochopo ya Eid Al Adha yalioandaliwa na wenyeji wao jana Nov 6,2011
.

No comments:

Post a Comment