Sudan kubana matumizi
Sudan kufunga mkanda
Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametangaza kuwa ataanzisha mipango ya kubana matumizi kufuatia kujitenga kwa Sudan Kusini.
Rais aliwaambia wabunge kuwa mpango huo wa miaka mitatu wa "dharura" utajumuisha kuwa na sarafu mpya. Pia ameahidi kuwa na jamii iliyo na uwazi zaidi ambapo watu watakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao ya kisiasa bila ya kuwa na wasiwasi wa kukamatwa.
"Serikali yetu iko makini kutozuia uhuru wa kujieleza. Kuanzia leo hakuna mtu atakamatwa kwa kutoa maini yake ya kisiasa," amesema rais huyo wakati akihutubia bunge, mjini Khartoum.
Mashauriano kuhusu katiba mpya - mabayo ni madai makuuya upinzani - yataanza hivi karibuni, amesema.
Utakuwa mchakato utakaojumuisha wanasiasa wa upinzani, viongozi wa dini na wahadhiri wa vyuo vikuu, na katiba hiyo mpya itafanyiwa kura ya maoni.
Mwezi Disemba mwaka jana, Rais bashir alisema katiba mpya itafanya Uisilam kuwa dini pekee nchini humo na utawala wa Sharia ndio utakaotumika.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum James Copnall amesema wapinzani wa Bw Bashir watakuwa na mashaka kuhusu ahadi hizo za uhuru zaidi wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment