Wednesday, 6 July 2011

Raza: Katiba iwe dawa ya Muungano

Mfanyabiashara maarufu visiwani Zanzibar, Mohammed Raza
Mfanyabiashara maarufu visiwani Zanzibar, Mohammed Raza,(pichani) ametaka masuala ya msingi yanayohusu wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar yaingizwe katika Muswada wa Katiba mpya ya nchi unaotarajia kujadiliwa bungeni mwaka huu mjini Dodoma.
Raza alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipofika katika ofisi za NIPASHE zilizopo Mikocheni na kuongeza kuwa kama hilo halitafanyika hakutakuwa na maana yoyote ya kuwa na Katiba mpya.
Alisema masuala ya Katiba yasiingiliwe na kiongozi yoyote wa serikali, bali waachiwe wananchi wa pande mbili ili wayajadili na kutoa maamuzi yao ambayo yataingizwa kwenye muswada huo.
Alifafanua kuwa ikiwa mambo ya msingi yanayohusu Zanzibar hayataingizwa katika muswada huo na kujadiliwa ni bora Wabunge wanaotoka visiwani kuondoka nje ya vikao vya bunge na kurudi nyumbani.
Baadhi ya masuala aliyotaka yajadiliwe na kuingizwa katika muswada huo ni pamoja na vipengele vinavyoelezea kwa undani muundo wa Muungano.

No comments:

Post a Comment