Mishahara Zanzibar juu kwa asilimia 25
Kima cha chini chaa mshahara wa watumishi serikalini Zanzibar kimepanda kwa asilimia 25.
Kwa nyongeza hiyo, mshahara wa kima cha chini utakuwa Sh. 125,000 badala ya Sh. 100,000 na mshahara huo utaanza kulipwa Oktoba mwaka huu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Haji Omar Kheri, alisema mshahara kwa watumishi wa ngazi nyingine utaongezeka kwa kuzingatia sifa za kitaaluma na uzoefu.
Waziri Kheir alisema hayo jana katika hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.
“Serikali imeamua kupandisha mshahara kwa asimilia 25 kwa wafanyakazi wa kima cha chini ambao wanaendelea na utumishi wao pamoja na wa ngazi nyingine,” alisema.
Hata hivyo, Kheir alisema kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali, nyongeza itaanza kutotolewa Oktoba badala ya Julai na haitakuwa na malimbikizo ya mshahara wao wa nyuma.
Alisema serikali pia itafanya mapitio ya posho mbalimbali za kila mwezi kwa watumishi wote wa umma.
Alisema mabadiliko ya mshahara yatazingatia ngazi za mishahara ya sasa kupitia miundo ya utumishi inayozingatia elimu na uzoefu kazini wa kila mtumishi.
Kuhusu wafanyakazi hewa, Kheir alisema watumishi wote wa serikali wameingizwa katika mfumo wa kumbukumbu unaotumia teknologia (data base) ili kuthibiti udanganyifu huo.
No comments:
Post a Comment