Saturday, 2 July 2011


Balozi wa Tanzania nchini Marekani awakaribisha wakuu wa makampuni ya marekani chakula cha mchana katika hoteli ya East Africa

                     

BALOZI wa Tanzania nchini Marekani Bi Mwanaidi Maajar pamoja na ugeni
wake leo wamekula chakula cha pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara
pamoja na maafisa wa bodi ya utalii Tanzania katika Hoteli ya East
Africa.
Ugeni huo ambao ni Marais,wenyeviti na wakurugenzi wa makampuni
mbalimbali ya nchini Marekani wako nchini kwa ziara maalumu
iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja nchini
kuangalia maeneo kwa ajili ya kuwekeza pamoja na kutembelea vivutio
mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza baada ya chakula ,Rais wa kampuni ya usafirishaji ya
Ahmed’s Moving Express Inc,Bw Ahmed Issa , mtanzania aliyehamia
Marekani kwa zaidi ya miaka 20 amesema Tanzania ni moja ya nchi yenye
rasilimanli nyingi pamoja na mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji.




“Mimi ni mwenyeji wa Tanga naamini nina wajibu wa kurudi nyumbani na
kuwekeza na hatua hiyo imekuja baada ya kuonana na balozi wa Tanzania
nchini marekani ,lakini pia niliwahi kuonana na viongozi wa juu wa
serikali ambao nilishauriana nao na kukubali mwaliko wa kuja nchini
kujionea hali halisi ya mazingira ya uwekezaji”alisema Issa.
Kwa upande wake Erick Pike ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya umeme
ya Pike amesema kampuni yake inatarajia kuwekeza katika miradi ya
umeme na kuboresha miundombinu iliyopo hasa katika mikoa ya kanda ya
kati.



“Tumeelezwa kuhusu tatizo la umeme nchini Tanzania.tunatarajia
kushirikiana na Tanesco katika kuboresha miundo mbinu na kuzalisha
umeme”alisema Pike.
Naye mtendaji wa mtandao wa Hotel za Camden Bw Munir Walji amesema
kampuni yake imepata maelezo ya kina kuhusu maeneo ya uwekezaji na
kwamba ikipata ardhi itajenga hoteli mbili zenye hadhi ya nyota 5
katika jiji la Dar es slaam na Arusha.




Munir amesema ili kuunganisha hoteli hizo na sekta ya utalii,kampuni
yake inatarajia kujenga hoteli nyingine ndogo katika maeneo ya jirani
na hifadhi za taifa na mbuga za wanyama. 

No comments:

Post a Comment