Rais wa zanzibar dr Shein amteua Mwenyekiti mpya wa bodi ya mamlaka ya kusimamia usafiri wa Baharini.

Rais Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 7(2) cha sheria ya usafiri baharini Zanzibar. Dk Shein pia amemteua Bi.Sharifa Khamis Salim kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar. Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha 7(1) cha sheria ya Baraza la Michezo Zanzibar namba 5 ya mwaka 2010. Bi. Sherifa alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo lililopita. Uteuzi huo umeanza leo (jana) Juni 9, 2011. IMETOLEWA NA: IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment