Sunday, 5 June 2011

Rais wa yeman kwenda kutibiwa Soud Arabia Baada ya shambulio la roketi
  

Smashed: The Mosque in Yemeni president Ali Abdullah's compound after it was attacked by rockets fired by opposition forces
eneo la Msikiti katika Yemeni rais Ali Abdullah baada ya kushambuliwa na makombora alikuwa fired na vikosi vya upinzani

Rais Ali Abdullah Saleh ameondoka nchini kwenda kutibiwa Saudi Arabia, baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kombora dhidi ya ikulu, ambapo rais na baadhi ya maafisa wake walijeruhiwa.

Day of departure: Yemenis in Sana'a celebrate the departure of president Saleh after four months of protests demanding the ousting of his 32-year regime
Maelfu ya Wayemen wanasherehekea kuondoka kwa Rais Saleh nchini.

Vijana wengi walisherehekea katika Medani ya Chuo Kikuu cha Sanaa, na wengine walitoka bara-barani wakipepea bendera. Lakini milio ya bunduki na miripuko ilisikika. Piya kuna taarifa kutoka Taiz kuwa mapambano yamezuka, na watu kadha wameuwawa.

Waliyemuona Rais Saleh Saudi Arabia, wanasema Rais Saleh aliteremka mwenyewe kwenye ndege lakini majaraha ya kichwani, usoni, na shingoni yakionekana. Rais Saleh, akifuatana na jamaa zake, aliwasili Saudi Arabi usiku wa Jumamosi.

Lakini mwanawe wa kiume na mpwa wake, ambao wanaongoza jeshi, inaarifiwa wamebaki nchini, na hao ndio walioisaidia Marekani kupambana na ugaidi nchini Yemen. Rais Saleh alijeruhiwa chini ya moyo katika shambulio la kombora siku ya Ijumaa.
Loyal: A group of armed government troops ride a pick-up truck through the streets of Sana'a
Waaminifu: Kundi la askari wenye silaha za serikali wakionekana wamepanda gari ya aina ya pick-up lori katika mitaa ya Sana'a

Maafisa wa serikali wamewalaumu watu wa makabila yenye silaha, wanaoshirikiana na wapinzani wa rais, kwa shambulio hilo, lakini makabila hayo yamekanusha kuwa yalihusika.

Mdadisi mmoja aliye karibu na Rais Saleh, anaona shambulio la Ijumaa lilitokana na bomu lilotegwa na mtu kati ya watu wanaomzunguka rais, lakini ni shida kuthibitisha hayo. Swala ni jee, Rais Saleh, ambaye ameongoza nchi kwa miaka 33, ndiyo ameondoka kabisa, au atarudi ?.

Angalia na usikilize kwa makini video ya vijana wa yemeni wakishangiria juu ya tokeo hilo !

No comments:

Post a Comment