| Maofisa Benki ya Dunia watua Ngorongoro |
| Mussa Juma, Samunge MKURUGENZI wa Benki ya Dunia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray Mclntire na ujumbe wa maofisa wengine watano wa benki hiyo, wametua wilayani Ngorongoro jana kupokea maoni ya wananchi kuhusu ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Mto wa Mbu, Loliondo mpaka mkoani Mara. Maofisa hao akiwamo mwakilishi wa Balozi wa Ujerumani, Gisela Habel walipokelewa na mabango ya wananchi ya kutaka barabara ya lami kutoka Mto wa Mbu, Loliondo mpaka mkoani Mara na baadaye walitarajiwa kupitia Samunge. Akizungumza kabla ya majadiliano na wananchi yaliyofanyika Kijiji cha Soitsambu, Mclntire alisema wamefika Loliondo kukusanya na kuwasikiliza wananchi kuhusu mradi wa barabara hiyo itakayopitia Hifadhi ya Serengeti. Alisema Benki ya Dunia haina kipingamizi na ujenzi wa barabara hiyo, bali inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wakiwamo wananchi na wanamazingira ili kuhakikisha barabara haiathiri Hifadhi ya Serengeti. Awali Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Saning'o Ole Telele alisema barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa Ngorongoro kwa kuwa itawasaidia kupata maendeleo na haitaathiri Serengeti. "Sisi wakazi wa Ngorongoro ni wanamazingira wazuri tunawahakikishia barabara hii haitakuwa na athari kwa Serengeti kama ambavyo baadhi ya wanaharakati wa mazingira wasema,"alisema Telele. Mpaka jana jioni kikao cha maofisa hao wa Benki ya Dunia na wananchi kilikuwa kikiendelea.Maofisa wengine wa benki hiyo ni ni pamoja na Mukami Kariuki anayesimamia masuala ya barabara, Ann Glauber na Jane Kiubassa wataalamu wa masuala ya mazingira na maofisa wengine Helen Shahriari na Uonas Mchomvu Mamia waendelea kutua Samunge Mamia ya watu, kutoka ndani na nje ya nchi, akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, jana walitua Samunge na kupata kikombe cha dawa ya Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila. Watu hao baada ya kupata tiba wengi wao wakiwa ni raia wa nchi jirani ya Kenya waliondoka Samunge.Mwisho wa kuuza pombe Samunge ni saa 3:00 usiku Siku tatu baada ya kuripotiwa habari ya kuibuka vitendo vya uzinzi na ulevi ulivyokithiri Samunge, serikali ya kijiji hicho, imepiga marufuku kufunguliwa na migahawa ya vilevi kuanzia saa 3:00 usiku. Mwenyekiti wa kitongoji cha Samunge, Jonas Ngiroboi alisema wameamua kuchukua tahadhari hiyo ili kuzuia wimbi la uhalifu na vitendo viovu Samunge. Ngiroboi ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho, alisema sambamba na kuzuia vilevi kuuzwa usiku kucha pia, wameanza kuoriodhesha wafanyabiashara wote ili kubaini watu wasio na kazi na kuwafukuza. "Tumeanza kuwaorodhesha majina na mahala wanapofanyia kazi kwani kuna ongezeko kubwa la watu hapa wakiwamo wahalifu,"alisema Ngiroboi. Mwasapila awaondoa hofu wagonjwa. Mchungaji Mwasapila jana, amewaondoa hofu wagonjwa wanaotumia dawa kwamba wasipate hofu endapo watapima afya na kubainika wana Virusi Vya Ukimwi (VVU). Akizungumza na mamia ya watu jana kabla ya tiba, Mwasapila alisema tiba hiyo ni ya kiimani zaidi na haitegemei mizizi ya mti wa Mungamuryogo au mugariga pekee. "Mnapokunywa dawa hapa muwe na imani na mtakuwa mmepona kabisa magonjwa yanayowasuymbua hata wale wenye uchawi, ukinywa dawa, uchawi unakwisha"alisema Mwasapila. |
No comments:
Post a Comment