Majeshi ya Syria yaingia Shughour
Majeshi ya serikali ya Syria, yakitumia vifaru na helikopta, yanaarifiwa kuanza kusonga ndani ya mji wa Jisr al-Shughour, kaskazini-magharibi mwa nchi.
Udhibiti wa al Shughour
Operesheni kubwa ya kudhibiti eneo hilo, ilianza Ijumaa, baada ya wakuu kusema kuwa askari wa usalama mia-moja-na-20 waliuliwa na watu waliokuwa na silaha.
Watu wengi wamelihama eneo hilo na elfu kadha wamevuka mpaka kukimbilia Uturuki.
Kambi ya wakimbizi Uturuki
Wanaharakati na wakaazi wanasema kwa siku mbili sasa, wanajeshi wametumia vifaru kushambulia Jisr al-Shughour kutoka vitongoje, na tena kujongelea mji.
Taarifa moja inaeleza kuwa risasi zilitumiwa holela, na nyumba nyingi zimechomwa moto.
Inaarifiwa kuwa kati ya wanajeshi kuna makundi ya wanamgambo yanayoitwa Shabbiha,hawa ni wanamgambo wanao-ogopwa sana, na wanaelezwa kuwa wakora.
Televisheni ya taifa ilisema kuwa makundi mawili yenye silaha yamekamatwa na wengine waliuwawa au kujeruhiwa.
Shambulio hilo la jeshi limefanya wakaazi wengi zaidi kukimbia, baadhi yao wameelekea kwenye mpaka wa Uturuki.
Wa Syria Uturuki
Taarifa moja inasema baadhi ya wakimbizi walikamatwa njiani kabla ya kuvuka mpaka, na wengine walipigwa risasi na kuuwawa.
No comments:
Post a Comment