Wednesday, 15 June 2011



HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA FEDHA MHE.KABWE ZUBERI ZITTO (MB) KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2011

Mheshimiwa   Spika,   Kwanza   namshukuru   Mwenyezi   Mungu   kwa    kunipa afya njema na kuweza kusimama hapa mbele ya Bunge hili,    kuwasilisha   Maoni na Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kuhusu    hali  ya  uchumi  ya  nchi  yetu  na  bajeti  kwa  mwaka  2011/2012  kwa    mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 96(6).        Mheshimiwa Spika,  Naomba kwa niaba ya waheshimwa wabunge    wote wa  Kambi ya Upinzani ambao hawakupata nafasi ya kushiriki    au kutoa rambirambi zao kwako kwa msiba mkubwa uliokupata wa    kuondokewa na Mama yako mpenzi, nifanye hivyo kwa niaba yao.         Mheshimiwa Spika, Kabla ya kuanza kutoa mtazamo wetu naomba    nikishukuru   chama   changu   cha   Demokrasia   na   Maendeleo   –    CHADEMA,          viongozi      wangu       wakuu       wote,      kwa     juhudi     kubwa    tunazozifanya  ili  kuhakikisha  Watanzania  wanaelewa  maana  halisi    ya     “wananchi        kuwa       na    mamlaka         kwa     Serikali     waliyoiweka    madarakani  kwa  njia  ya  kura”.  Vile  vile  na  kwa  umuhimu  wa    kipekee  namshukuru  Kiongozi  wa  Upinzani  Bungeni  Mhe.  Freeman          

  Aikael  Mbowe  (Mb)  kwa  kuniteua  kuwa  Waziri  Kivuli  wa  Wizara  hii    nyeti katika uchumi na maendeleo ya nchi. Kama ilivyo ada yangu,    nitaifanya kazi hii kwa uaminifu, uadilifu na umakini mkubwa sana.        Mheshimiwa            Spika,      Aidha,      namshukuru           Mheshimiwa           Christina    Mughwai  (Mb)  Naibu  Msemaji  Mkuu  wa  Kambi  –  Wizara  ya  Fedha    kwa ushirikiano wake pamoja na timu nzima ya Kambi ya Upinzani    kwa  kazi  yao  kubwa  waliyoifanya  katika  maandalizi  ya  hotuba  hii.    Napenda  kuwashukuru  kwa  dhati  kabisa  Watanzania  waliotupatia    maoni mbalimbali kupitia ‘social media’ kama facebook, twitter na    hata   wengine   kwa   kupitia   ujumbe   mfupi   wa   sms.   Maoni   yao    yamesaidia  kuboresha  Hotuba  hii  na  pia  kuimarisha  ushiriki  wa    wananchi katika kutengeneza Sera za nchi.        Mheshimiwa   Spika,   Nitakuwa   sijatenda   haki   kwa   wananchi   wa    Jimbo  la  Kigoma  Kaskazini  kama  sitawashukuru  kwa  imani  kubwa    waliyonayo kwangu, nami nawaahidi kuwa nitaitunza na kuiheshimu    imani  yao  kwangu,  kuendelea  kushirikiana  nao  kuleta  maendeleo    katika Jimbo na Mkoa wetu  na mwisho kukifanya CHADEMA kuwa    chama tawala hapo mwaka 2015. Asanteni sana.        Mheshimiwa           Spika,      Bajeti    ya     Nchi     ni   nyenzo       (instrument)        ya    maendeleo. Sio suala la Urari tu wa Mapato na Matumizi. Ni namna    ya  kutumia  rasilimali    chache  tulizo  nazo  kwa  ajili  ya  kutengeneza rasilimali nyingi zaidi na hatimaye kuboresha maisha ya wananchi na    kujenga Taifa Imara.     Hivyo basi, Bajeti inahusu namna ya kukusanya na kutumia pesa za    wananchi   kwa   manufaa   yao   ya   pamoja.   Kwa   bahati   mbaya,    mchakato          wa     kuamua         namna        ya    kuzitumia,       kuzisimamia        na    kuhakikisha   kuwa   pesa   hizo   zinaenda   zinakotakiwa   kwenda   ni    mgumu  kwa  wananchi  wa  kawaida  kuweza  kushiriki.  Hii  inatokana    na  ukweli  kuwa  sehemu  kubwa  ya  taarifa  zinazohusiana  na  bajeti    huwa haziwekwi wazi kwa umma, na hata zile zinazopatikana huwa    katika namna iliyo ngumu kueleweka. Hivyo, wananchi wengi huwa    hawana  fursa  ya  kushiriki  katika  michakato  ya  bajeti.  Kwa  ujumla,    michakato mingi rasmi huwa haiko wazi kwa wananchi. Hata hivyo,    juhudi  zilizoanza  sasa  za  kutaka  kuanzisha  Ofisi  ya  Bajeti  ya  Bunge    zitasaidia sana kuweka uwazi katika Bajeti ya Nchi na hivyo kuweka    urahisi wa wananchi kushiriki katika mchakato.        Mheshimiwa   Spika,   Kambi   ya   Upinzani   imekuwa   ikiitaka   Serikali    kuweka vitabu vya bajeti katika mfumo rahisi unaoweza kueleweka    na kufuatiliwa na wananchi wengi, lakini suala hilo limekuwa gumu    kufanyika. Nina matumaini kuwa kwa miaka ijayo na hasa baada ya    kuanzisha   Ofisi   ya   Bajeti   ya   Bunge,   vitabu   vya   Bajeti   vitakuwa    vinapatikana mapema na kwa njia rahisi.        Mheshimiwa Spika, Tunaamini kuwa ushiriki mkubwa zaidi wa umma    na  uchunguzaji  wa  utungaji  na  utekelezaji  wa  Bajeti  utaboresha  uwajibikaji na kuziba mianya zaidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya    rasilimali za nchi.        Mheshimiwa  Spika,  Mahatma  Gandhi  aliwahi  kusema  “Mabadiliko    ya   kidemokrasia   hayawezekani   iwapo   hatupo   tayari   kusikiliza    upande         mwingine.         Tunafunga          milango        ya      kufikiri     wakati    tunapokataa kuwasikiliza wapinzani wetu, au baada ya kuwasikiliza    tunawafanyia  mzaha.  Kutokuvumiliana  kunapokuwa  ndio  mazoea,    tunajiweka katika hatari ya kutokujua ukweli”.     Kambi  ya  Upinzani  ilitoa  maoni  yake  ya  mwelekeo  wa  Bajeti  na    kuainisha  mambo  kadhaa  itakayoyapendekeza  katika  Bajeti  yake    Mbadala. Mambo hayo ni pamoja na;      i.    Kupunguza misamaha ya Kodi ili isizidi 1% ya Pato la Taifa.      ii.   Kupunguza kodi na  tozo  kwenye Mafuta  ya  Petroli  na Dizeli ili            kupunguza         mfumuko         wa     Bei    na    ukali    wa     maisha       kwa           wananchi.     iii.   Kufanya   Marekebisho   makubwa   katika   mfumo   wa   malipo           Serikalini hususan kuondoa Posho za vikao (sitting allowances)            kwa watumishi na viongozi wote wa Umma     iv.    Kuelekeza        sehemu        ya     tozo     ya     kuendeleza         ujuzi    (Skills            Development levy) kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa            Elimu ya Juu.                                                  
    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Hotuba  ya  Waziri  wa  Fedha  na  Uchumi,    baadhi  ya  mambo  haya  yalizingatiwa  na  kupewa  kipaumbele.    Ninachukua  fursa  hii  kumpongeza  Waziri  mwenzangu  kwa  kusikiliza    maoni  yetu  kwenye  baadhi  ya  mambo  hayo  na  hivyo  kuonyesha    kwa  umma  moja  ya  faida  ya  mfumo  wa  vyama  vingi.  Tunataraji    kuwa  Serikali  itaendelea  kusikiliza  maoni  yetu  na  kuyafanyia  kazi.    Changamoto hii na kwa uzito ule ule pia ipo kwetu sisi wa Kambi ya    Upinzani  kusikiliza  pia  maoni  ya  Serikali.  Ni  kwa  namna  hii  ndio    tutajenga  Taifa  la  watu  walio  huru,  lenye  demokrasia,  usawa  na    haki, na lenye kutoa fursa kwa wananchi wake.        TATHIMINI YA HALI YA UCHUMI.        Mheshimiwa  Spika,  Ninapopitia  Hali  ya  Uchumi  ili  kutoa  maoni  ya    Kambi  ya  Upinzani  Bungeni  ni  vema  tulijue  Taifa  letu  kwa  Takwimu    Chache.     Mheshimiwa  Spika,  Pato  la  Taifa  limefikia  shilingi  32  trilioni  na  hivyo    Pato  la  wastani  la  kila  mtu  kuwa  shilingi  770,000.  Tanzania  ina    takribani wananchi 42 milioni na kati ya hao 11 milioni wapo kwenye    taasisi za Elimu kwa maana ya Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya    Ufundi  na  Vyuo  vya  Elimu  ya  Juu!  Kwa  hiyo  Robo  ya  Watanzania    wanasoma  hivi  sasa  na  wakimaliza  wanataraji  kupata  ajira  kwa    kuajiriwa au kujiajiri.     Mheshimiwa  Spika,  Mwaka  2010  Watanzania  19  milioni  walikuwa    wanatumia   simu   za   mkononi   na   hivyo   kufanya   asilimia   45   ya                                                    
    Watanzania  kuwa  na  simu  na  kuliweka  Taifa  katika  nafasi  ya  juu    kabisa  duniani  ya  matumizi  ya  simu.  Asilimia  64  ya  Watanzania    wanapata maji safi na salama mijini na asilimia 57.8 hupata huduma    hii vijijini. Asilimia 14 ya Watanzania wanapata huduma ya umeme    na kwa vijijini ni asilimia 2 tu.     Mheshimiwa  Spika,  Asilimia  33.4  ya  Watanzania  wanaishi  chini  ya    mstari  wa  umasikini  na  kwa  waishio  vijijini  ni  asilimia  37.4  wakati    asilimia 16.2 tu ya Watanzania waishio Dar es Salaam wanaishi chini    ya mstari wa Umasikini. Wakati tofauti ya kipato kwa Watanzania ni    asilimia 35, matajiri wa juu asilimia 20 wanamiliki asilimia 42 ya Pato    la  Taifa  (consumption  expenditure)  na  masikini  wa  chini  kabisa    asilimia 20 wanamiliki asilimi 7 tu ya Pato la Taifa.        Mheshimiwa Spika,  katika taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika    mwaka  2010/11  iliyosomwa  hapa  Bungeni  inaonyesha  kuwa  katika    mwaka 2010/11 Pato halisi la Taifa lilikuwa kwa kiwango cha asilimia    7.0  ikilinganishwa  na  ukuaji  wa  asilimia  6.0  mwaka 2009/10.  Taarifa    inaonyesha  kuwa  ukuaji  huu  wa  uchumi  ulitokana  na  kuchangiwa    zaidi  na  kuongezeka  kwa  viwango  vya  ukuaji  katika  shughuli  za    kiuchumi  zenye  mchango  mkubwa  katika  Pato  la  Taifa  na  hasa    Kilimo, Biashara na matengenezo na ujenzi.        Mheshimiwa Spika , pamoja na taarifa hiyo ukweli ni kuwa ukuaji wa    viwango  vya  juu  ulionekana  zaidi  kwenye  sekta  za  Mawasiliano    (22.1%),  ujenzi  (10.2%),  umeme  na  gesi  (10.2%),  fedha  (10.1%)  na                                                      6    uzalishaji viwandani  (7.9%).  Hata  hivyo,  pamoja  na  ukuaji wa  sekta    hizi,  mchango  wake  katika  pato  la  Taifa  ni  mdogo  kulingana  na    kiwango cha ukuaji wa sekta husika kwa mwaka 2010/11.        Mheshimiwa  Spika,  taarifa  ya  Hali  ya  uchumi  inaonyesha  kuwa    pamoja na sekta kadhaa kukua lakini bado hazijaongeza mchango    wake katika ukuaji wa pato la taifa ukilinganisha na ukuaji wa sekta    husika. Kwa mfano, sekta ya mawasiliano imekuwa kwa asilimia 22.1    ila  mchango  wake  katika  pato  la  Taifa  ni  asilimia  2.1  tu,  shughuli    ndogo   za   hoteli   na   migahawa   ukuaji   wake   ulikuwa   6.1   lakini    mchango  wake  katika  ukuaji  wa  pato  la  taifa  ni  2.3%  tu.  Hii  ina    maana kuwa sekta hizi hazina uhusiano wa moja kwa moja (strong    linkages) katika ukuaji wa uchumi na katika kukuza pato la taifa na    hivyo kushindwa kupunguza hali ngumu ya maisha kwa wananchi.         Mheshimiwa  Spika,  taarifa  ya  hali  ya  uchumi  inaonyesha  kuwa    mchango  wa  shughuli  za  kiuchumi  za  kilimo  umeendelea  kushuka,    hii  ni  pamoja  na  ukweli  kuwa  Serikali  katika  mwaka  husika  ilijikita    kwenye  “Kilimo  Kwanza”  jambo  ambalo  halionyeshi  kama  ni  kilimo    kwa kauli tu ama ni kweli tunawekeza kwenye kilimo katika kukuza    uchumi  wa  wananchi  takribani  asilimia  71  ambao  wanategemea    kilimo kama msingi mkuu wa maisha yao. Pia mauzo ya mazao nje    ya  Nchi  yalipungua  kama  ifuatavyo:  kahawa  (36.4),  Pamba  (24.3),    Chai  (39.0),  Karafuu  (47.0);  hii  ni  pamoja  na  ukweli  kuwa  bei  za    mazao  husika  iliongezeka  ukilinganisha  na  mwaka  2009/10,  ila  sisi tulishindwa  kuitumia  fursa  hiyo  katika  kukuza  uchumi  wa  wananchi    wetu ambao ni wakulima wa mazao haya kwa kuongeza uzalishaji.        Mheshimiwa Spika ,    Ukisoma  taarifa  ya  hali  ya  uchumi  utaona  kuwa  ni  sekta  mbili  za    utoaji huduma na viwanda na ujenzi ndizo zinachangia pato la Taifa    kwa  asilimia  66.3.  Hii  maana  yake  ni  kuwa  sekta  mama  ya  kilimo    ambayo  ndiyo  inaweza  kuwaondolea  watanzania  umasikini  kwa    sasa ina mchango mdogo katika Pato la Taifa. Mabadiliko haya ya    kimuundo   wa   uchumi   wetu   ndio   sababu   kubwa   tunakuwa   na    uchumi  unaokua  bila  kupunguza  umasikini.  Narejea  kusema  kuwa    kwa  sasa,  ukilinganisha  na  tulipotoka,  licha  ya  kwamba  tunahitaji    ukuaji  wa  kasi  zaidi  wa  uchumi,  ukuaji  sio  changamoto  kubwa.    Changamoto sasa ni namna gani ukuaji huu wa uchumi unawafikia    wananchi. Sekta zinazokuwa kwa kasi ni zile zinazoshawishi uwekezaji    wa  sekta  binafsi  kwa  urahisi.  Sekta  ya  Kilimo  inahitaji  uwekezaji    mkubwa  wa  kimiundombinu  wa  Serikali.  Nchi  yetu  itaendelea  na    changamoto  ya  kupunguza  umasikini  hadi  hapo  tutakapoamua    kwa  dhati  kuwekeza  katika  kukuza  uchumi  wa  vijijini.   Kambi  ya    Upinzani inapendekeza katika Bajeti hii mbadala mikakati maalumu    ya kukuza uchumi wa vijijini kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya    vijijini, umeme vijijini na maji vijijini.        Mheshimiwa Spika,    Katika mwaka 2010/11 ukuaji katika shughuli za kiuchumi za Madini                        
na  uchimbaji  mawe  uliongezeka  na  kufikia  asilimia  2.7.  Ukuaji  huu    ulichangiwa  zaidi  na  kuongezeka  kwa  uzalishaji  wa  dhahabu  na    kuongezeka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia. Hata hivyo,    mchango wa sekta hii pamoja na kuongezeka uzalishaji na bei kuwa    kubwa  zaidi  ya  mwaka  2009/10  bado  uliendelea  kuwa  ule  ule  wa    mwaka  2009/10  wa  asilimia  3.3  pamoja  na  kuuza  nje  dhahabu    yenye thamani ya dola za kimarekani 1,516.6 milioni mwaka 2010/11.    Mauzo  haya  ya  Dhahabu  nje  kwa  mwaka  2010/11  ni  sawa  na    asilimia 7.1 ya Pato la Taifa kwa hesabu za mwaka husika. Ukiangalia    mchango  wa  Sekta  ya  Madini  kwenye  Pato  la  Taifa,  mchango    kwenye Mapato ya Serikali na Mchango wa Sekta katika Mauzo ya    nje  unaona  dhahiri  kabisa  kuwa  bado  tunahitaji  kufanya  kazi  ya    ziada kuhakikisha sekta ya Madini inakuwa na mahusiano na Sekta    nyingine za uchumi (linkages). Masuala haya yanahitaji kusimika sera    madhubuti  (policy  interventions)  ili  kulifanya  Taifa  lifaidike  na  utajiri    wa  Madini.  Kuboresha  sera  za  Kikodi  ikiwemo  kujenga  uwezo  wa    Wakandarasi  wa  ndani  katika  sekta  ya  Madini  na  kuhusisha  sekta    ndogo       ya    Umeme        na    sekta     ya   Madini       ni   masuala   ambayo    tunapaswa kuyaamulia wenyewe.        Mheshimiwa Spika,    Taarifa     ya    hali   ya    uchumi       inaonyesha         kuwa      mwenendo           wa    mfumuko wa bei umekuwa ukiongezeka tangu mwezi Oktoba 2010    kutoka asilimia 4.2 na kufikia asilimia 5.6 mwezi Disemba 2010 , mwezi    Januari  2011  ulikuwa  asilimia  6.4  na  hadi  kufikia  mwezi  Aprili  2011 mfumuko  wa  bei  ulikuwa  umefikia  asilimia  8.6.  Hii  ina  maana  yake    kuwa  mfumuko  wa  bei  unaongezeka  kwa  wastani  wa  asilimia  0.8    kila mwezi . Hali hii inaelezwa kuwa ni kutokana na ongezeko la bei    za umeme , gesi na chakula , jambo hili ni la hatari katika ukuaji wa    uchumi   kama   hatua   za   haraka   na   dharura   hazitachukuliwa   ili    kuweza kukabiliana na jambo hili kwani kama hali itaendelea kuwa    hivyo kwa miezi mitano tu ijayo,  mfumuko wa bei utakuwa umefikia    asilimia  12.6.  Serikali  imekubaliana  na  hoja  ya  Kambi  ya  Upinzani    kwamba  itaangalia  tozo  katika  bei  za  mafuta  ili  kudhibiti  hali  hii.    Hata hivyo, suluhisho la muda mrefu la kudhibiti mfumuko wa Bei ni    kuzalisha chakula cha kutosha kwani chakula ni sehemu kubwa ya    kikapu   cha   bidhaa   na   huduma   ambazo   Mtanzania   anatumia.    Ikitokea kuwa Bei za Mafuta katika soko la Dunia zikapanda tena na    kuyafanya  maamuzi  yetu  ya  kikodi  hayana  maana  kuna  haja  ya    Serikali  kuangalia  jinsi  ya  kufidia  kupanda  kwa  Bei  za  Umeme  kwa    asilimia 18 ili kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi.        Mheshimiwa Spika,    Thamani  ya  Shilingi  ya  Tanzania  imeendelea  kushuka  ukilinganisha    na  fedha  za  kigeni  na  hii  inatokana  na  kukosekana  kwa  mikakati    thabiti ya kuhakikisha kuwa shilingi inaimarika kwenye soko na hasa    kutokana  na  sera  mbovu  za  kiuchumi  na  usimamizi  usio  makini.    Kushuka kwa thamani ya Shilingi licha ya kupanda kwa mauzo yetu    nje  kwa  sekta  zote  mbili  tunazotegemea  sana  (Madini  na  Utalii)    kunaacha maswali mengi kuhusiana na chaguo letu kuhusu Hifadhi ya  Fedha  za  kigeni.  Kambi  ya  Upinzani  inaunga  mkono  ushauri    uliotolewa  na  Kamati  ya  Bunge  ya  Hesabu  za  Mashirika  ya  Umma    kwamba  sasa  Benki  Kuu  ya  Tanzania  ianze  kutunza  sehemu  ya    Hifadhi ya nchi katika Dhahabu. Benki Kuu inunue dhahabu kutoka    kwa  wachimbaji  wadogo  na  pia  tuangalie  uwezekano  wa  kutoza    sehemu  ya  mrahaba  katika  madini  kama  ‘dhahabu  safi’  (‘pure    gold’).            Mheshimiwa Spika,     Deni  la  taifa  linaonekana  kuongezeka  kwa  kasi  ya  ajabu  sana  na    hivyo  kupelekea  Taifa  kuwa  na  mzigo  mkubwa  sana  wa  Madeni.    Kwa  mujibu  wa  Mdhibiti  na  Mkaguzi  Mkuu  wa  Hesabu  za  Serikali,    Deni  la  Taifa  limeongezeka  kwa  asilimia  38  kutoka  Tshs  7.6  trilioni    mwaka 2008 mpaka Tshs 10.5 trilioni mwaka 2009 na sasa kwa mujibu    wa  Hotuba  ya  Waziri  wa  Fedha  na  Uchumi  Deni  limefikia  Dola  za    Kimarekani 11. 4 Bilioni ambazo ni sawa na Tshs 17.1 Trilioni kwa bei    ya   Dola   ya   Kimarekani   ya   Disemba   2010.   Jedwali   hapa   chini    linaonyesha Deni la Taifa na Malipo ya Deni hilo.                                                      
                                                                                                                               Mheshimiwa Spika, Mataifa yote Duniani hukopa sembuse sisi Taifa    linaloendelea.  Hata  hivyo,  kasi  ya  ukopaji  wetu  sio  endelevu  hata    kidogo  na  kwa  kweli  ni  mzigo  mkubwa  kwa  kizazi  kijacho.  Kwa    mfano, tunapoangalia Bajeti ya mwaka huu utaona kuwa asilimia 50    Ya Bajeti itagharamiwa na Kodi zetu, lakini asilimia 30 itagharamiwa    na Mikopo ya ndani, ya nje na ya kibiashara, asilimia 17 Misaada na    asilimia  3  Makusanyo  ya  Halmashauri.  Hii  maana  yake  ni  kwamba    asilimia  30 ya gharama za sasa za Serikali itabebwa na kizazi kijacho    kwani madeni haya yatalipwa na kizazi hicho.                                                                  
    Mheshimiwa Spika,     Kambi   ya   Upinzani   Bungeni   inapendekeza   ufanyike   uchunguzi    Maalumu  kwenye  Deni  la  Taifa  ili  Mdhibiti  na  Mkaguzi  Mkuu  wa    Hesabu za Serikali atuambie madeni haya tunayokopa kwa kasi ya    namna  hii  tunayapeleka  kweye  miradi  gani  (Matumizi ya  Madeni)    na namna gani tunaweza kudhibiti Deni la Taifa.                 UDHAIFU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA.        Ripoti ta CAG katika Mwaka wa Fedha 2009/10    Mheshimiwa Spika,     Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuwa kikwazo   kikubwa  katika  utekelezaji  wa  miradi  ya  maendeleo  ya  wananchi.    Uchambuzi  wetu  juu  ya  ripoti  ya  Mdhibiti  na  Mkaguzi  Mkuu  wa   Hesabu  za  Serikali  (CAG)  kwa  mwaka  2009/2010  pekee,  umebaini   takribani jumla ya Tsh trilioni 2.4 za fedha za umma zilitumika vibaya,   ambazo  ni  sawa  na  asilimia  25%  ya  bajeti  yote  ya  mwaka  huo   ambayo  ilikuwa  na  jumla  ya  Sh  9.5  trilioni.    Hii  inaonyesha  kuwa   katika  kila  Shilingi  100  tunayopitisha  hapa  Bungeni  katika  Bajeti   Shilingi 25 zinaingia kwenye mifuko ya wezi na wabadhirifu wa fedha   za Umma. Hali hii lazima ikomeshwe mara moja.        Mheshimiwa Spika,     Mifano ya fedha zilizopotea au kutumiwa vibaya katika mwaka wa   fedha  wa  2009/10  ni  manunuzi  yaliyofanywa  nje  ya  mpango  wa   mwaka ya jumla ya Tsh bilioni 50.6, malipo yenye shaka ya jumla ya Tsh bilioni 15.5, upotevu wa fedha na mali za serikali wa jumla ya Tsh   bilioni  11.1  na  malipo  ya  mishahara  kwa  watumishi  waliostaafu,   waliokufa na watoro kazini ya jumla ya Tsh bilioni 1.8.     Aidha, Mkaguzi hakukabidhiwa  nyaraka na orodha ya walionufaika   na kiasi cha jumla ya Sh. bilioni 48 (Stimulus package) kilichotolewa   kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania   katika  juhudi  za  kukabiliana  na  msukosuko  wa  uchumi  ulioikumba   dunia.     Katika mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi nilimwuliza Mheshimiwa   Waziri Mkuu kuhusu suala la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za   Serikali   kunyimwa   nyaraka   ili   kukagua   jumla   ya   Tshs   48   bilioni   zilizotajwa hapo juu. Natumai sasa Serikali itakuwa na majibu juu ya   suala hili. Kambi inaendelea kusisitiza ombi lililotolewa na aliyekuwa   Waziri   Kivuli  wa  Fedha   na   Uchumi,   Mheshimiwa   Hamad   Rashid   Mohammed  kwamba  Fedha  zote  zilizotolewa  kwa  ajili  ya  Stimulus   Package  zikaguliwe  na  CAG  na  kuwasilisha  Taarifa  hiyo  maalumu   Bungeni. Serikali ilikubaliana na ombi hili hivyo tunaomba taarifa hiyo   mara moja.    Mheshimiwa Spika,    Tunalisema  hili  la  Stimulus  Package  kwa  kuwa  kuna  ushahidi  wa   barua kutoka kwa Katibu Mkuu Hazina akiwaandikia Mameneja wa   vyama vya ushirika vya mikoa ya Kilimanjaro na Kagera akiwaeleza   kuwa Serikali pamoja na kuidhinisha kulipwa kwa vyama hivyo, kwa   sasa hakuna fedha kwa ajili ya kufanya malipo hayo.    Barua  iliyoandikwa  kwa  Meneja  Kagera  Cooperative  Union  (1990)   ltd  ya  tarehe  16  Septemba  2010  yenye  kumb.  Na  TYC/B/40/143   ilikuwa  ikimweleza  Meneja  kuhusiana  na  serikali  kulipa  kiasi  cha   shilingi 734,369,379.49 . Ila ilipofika tarehe 27 Aprili 2011 Katibu Mkuu   wa  Hazina  aliandika  barua  nyingine  kwa  Meneja  husika  yenye   kumb.Na.TYC/B/40/143/45   kwa   ajili   ya   kusitisha   Malipo   ya   fidia  kutokana na mdororo wa uchumi kwa kuwa Serikali haina fedha na   pia muda wa kulipa fidia hizo ulikwisha tangu mwaka 2010.    Kuhusiana   na   chama   cha   ushirika   cha   Mkoa   wa   Kilimanjaro   (Kilimanjaro  Native  Cooperation  Union  (1984),  Katibu  Mkuu  Hazina,   Ndugu  Ramadhan  Kijjah  mnamo  tarehe  16  Septemba  aliandika   barua   yenye   kumb.Na   TYC/B/40/143   iliyowajulisha   kuwa   Serikali   imeridhika  kuwa  wanastahili  kupewa  fidia  ya  shilingi  255,107,570.17   waliyopata  kutokana  na  mdororo  wa  uchumi  duniani.  Ila  ilipofika   tarehe   27   Aprili   2011   Katibu   Mkuu   huyo   huyo   aliandika   barua   nyingine yenye kumb.Na.TYC/B/40/143/43 akiwajulisha kuwa Serikali   haina fedha kwa ajili ya kulipa fidia hiyo na kuwa muda wa kulipa   fidia ulikuwa umekwisha tangu mwaka 2010.    Mheshimiwa Spika,    Kupatikana  kwa  barua  hizi  ni  uthibitisho  wa  wazi  kuwa  kuna  tatizo   kubwa  kuhusiana  na  fedha  zilizotolewa  na  Serikali  kwani  wakati   Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yusuph Mzee akiwa anajibu swali   la msingi la Mhe. Mhonga Saidi Ruhanywa wakati wa Bunge la Bajeti   la  mwaka  2010/11  alisema  kuwa  mpango  ulikuwa  unaenda  vizuri.   Pia wakati Waziri wa Fedha Mhe. Mkullo akiwa anahitimisha hotuba   ya  bajeti  ya  mwaka  2010/11  alilieleza  bunge  hili  kuwa  mpango   ulikuwa unaenda vizuri.    Kambi  ya  Upinzani  inasisitiza  kuwa  tunaitaka  Serikali  ifanye  ukaguzi   maalum kwenye mfuko huu.  
JEDWALI 1.     JUMLA YA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YALIYOAINISHWA KATIKA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI    MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010

 MAELEZO                                                                    
 KIASI    Manunuzi yaliyofanywa nje ya mpango wa mwaka                                       50,685,371,565.58    Matengenezo ya magari ambayo hayakupitia TEMESA                                       176,722,089.00    Malipo ya mishahara kwa watumishi waliostaafu, waliokufa na watoro kazini           1,842,607,565.29    Malipo ya posho ya samani kwa maafisa wasiostahili                                    770,087,895.00    Malipo yenye nyaraka pungufu                                                        4,303,339,515.00                                                        Vifaa vilivyolipiwa bado havijapokelewa                                                                 13,865,874,762.00    Malipo yaliyofanyika katika kasma isiyosahihi                                                             4,953,226,683.00    Malipo yenye shaka                                                                                      15,595,054,755.00    Madeni na mihadi ya serikali                                                                               254,616,874,180    Misamaha ya kodi                                                                                       680,667,900,000.00    Maduhuli yasiyokusanywa kwa wakati                                                                     116,320,437,345.00    Madeni ya dharura ambayo hayakutarajiwa                                                                 26,276,785,317.00    Kutoa udhamini kinyume na kiwango kilichowekwa na sheria                                               711,804,989,096.00    Madai na amana za serikali ambazo hazikutolewa taarifa                                                 134,046,000,000.00    Madeni ya vifaa na huduma ambayo hayakulipwa                                                           160,756,067,190.00    Upotevu wa fedha na mali za serikali                                                                    11,152,048,065.00    Kutokuwepo uwazi katika mifuko maalumu ya fedha                                                         78,014,807,604.00    Bakaa ambayo haikurejeshwa kwa mlipaji mkuu                                                             31,821,562,811.00    Kukosekana kwa orodha ya waliolipwa kuchochea ukuaji wa uchumi                                          48,000,270,000.00    Malipo kwa Benki ya Rasilimali bila nyaraka za muhimu kutolewa                                          70,000,000,000.00    Jumla ya fedha zilizotumika vibaya katika mwaka husika wa fedha                                      2,415,670,026,437.87    Bajeti ya mwaka husika ilikuwa                                                                     11,000,000,000,000.00    Kwa hiyo, Jumla ya fedha zilizotumika vibaya ni sawa na 20% ya bajeti nzima                          2,415,670,026,437.87  

MAMBO MENGINE YA KUTILIWA MAANANI                                                                                                           Deni la taifa limekua kwa 38% na kufikia                                                           Trilioni 10    Jumla ya mali za serikali ambazo hazipo katika rejista                                             Trilioni 7.9    Jumla ya fedha zisizoonekana kutokana na dosari za kibenki kwa muda mrefu                          Bilioni 747.1    Fedha nyingi zilizotumiwa na serikali zaidi ya amana iliyopo benki                                 Trilioni 1.3    Jumla ya vitega uchumi vya serikali ambavyo hesabu hazikurekodiwa                                  Trilioni 8.7                                                                                                            

BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012.      
Mheshimiwa Spika,    Bajeti  ya  mwaka  wa  fedha  wa  2011/2012  inapendekezwa  kufikia    shilingi  13.5  trillioni  kutoka  shilingi  11.2  trillioni  ya  Mwaka  wa  Fedha    unaokwisha  wa  2010/2011.  Kwa  maana  ya  Shilingi  za  Kitanzania    Bajeti inaonekana kukua hata hivyo ukiondoa mfumuko wa Bei kwa    wastani wa asilimia 7%, ambao unapunguza uwezo wa kimanunuzi,    utaona  thamani  halisi  ya  Bajeti  ni  kama  Shilingi  12.5  trillioni  hivi.    Ukiibadilisha  Bajeti  kwa  dola  za  Kimarekani  ambapo  mwaka  2010  ilikuwa  ni  wastani  wa  Shilingi  takribani  1400  kwa  dola  moja  ya    kimarekani  na  sasa  siku  Waziri  anasoma  Bajeti  thamani  ya  Shilingi    ilikuwa  na  thamani  ya  shilingi  1581  kwa  dola  moja  ya  Kimarekani    utaona kuwa kwa uhalisia (in real terms) hakuna nyongeza ya Bajeti.    Hivyo  kuna  haja  kubwa  ya  kuimarisha  sarafu  yetu  na  kudhibiti    mfumuko wa Bei.  

Mheshimiwa Spika ,    Mnamo  tarehe  08/06/2011  Waziri  wa  Fedha  Mhe.  Mustafa  Mkullo   aliwasilisha  Bungeni  Mapendekezo  ya  Serikali  kuhusu  Makadirio  ya   Mapato         na     Matumizi       kwa      mwaka         2011/12.       Na     aliwaeleza   Watanzania  kuwa  bajeti  ya  mwaka  huu  ni  mahususi  kwa  ajili  ya   masuala        yalioyoorodheshwa             hapa       chini.    Nanukuu,        “Bajeti     ya   mwaka 2011/12 itazingatia vipaumbele vifuatavyo:      i) Umeme;   ii) Maji;   iii)  Miundombinu  ya  usafiri  na  usafirishaji  (reli,  bandari,  barabara,   viwanja vya ndege, Mkongo wa Taifa);   iv) Kilimo na umwagiliaji; na   v) Kupanua ajira kwa sekta binafsi na ya umma.    

 Mheshimiwa Spika,    Wakati  waziri  akitaja  kuwa  kipaumbele  cha  kwanza  ni  Umeme    ukiangalia kwenye vitabu vya Bajeti vya serikali, Wizara ya Nishati na    Madini  imetengewa  jumla  ya  shilingi  402.4  bilioni    kwa  mujibu  wa    fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi    shilingi  76,953,934,000  na  kwa  upande  wa  bajeti  ya  Maendeleo    zimetengwa  shilingi  325,448,137,000.  Katika  hali  hii  tunaona  kuwa    umeme   hauwezi   kuwa   kipaumbele   katika   bajeti   hii   kwa   kuwa                                                     haujapewa uzito unaostahili.    

 Mheshimiwa Spika,    Wakati  Wizara  ya  Nishati  na  Madini  inatengewa  kiasi  hicho  cha    fedha,   ukiangalia   fungu   lililotengwa   kwa   ajili   ya   Hazina(“the    treasury”)  fungu  21  zimetengwa  jumla  ya  shilingi  1,054,411,138,000.    Fedha zilizotengwa kwa Hazina fungu 21 ni sawa na asilimia 8% ya    bajeti  yote  ya  serikali.  Wakati  Wizara  ya  Nishati  na  Madini,  vote  58    yote  imepangiwa  fedha  za  Maendeleo  Tshs  325.4  Bilioni,  Hazina    imepangiwa  Tshs   129   Bilioni   kwa   ajili   ya   matumizi   mengine   ya    kiutendaji (‘other operating expenses’) na Tshs 314 bilioni kwa ajili ya    matumizi        mengine        ila   yasiyo      ya    dharura       (‘contingencies-non    emergence’). Nimemsikia Mheshimiwa Mkulo anasema kuwa Fedha    nyingine ya Umeme ipo Wizara ya Fedha kupitia MCC. Hata hivyo,    ukiangalia fungu 50 fedha za Maendeleo MCC zimetengwa shilingi    111  bilioni  ambazo  hazifikii  jumla  anayosema  Waziri.  Zaidi  ya  hapo    fedha  za  MCC  sio  za  miradi  ya  Umeme  peke  yake,  ni  pamoja  na    Barabara         nk.     Ningependa            kupata        ufafanuzi       zaidi      ambao    unathibitishwa  na  vitabu  vya  Bajeti  na  sio  maneno  matupu  katika    Hotuba.      

Mheshimiwa Spika,     Wakati  Waziri  akisema  Bungeni  kuwa  bajeti  ya  mwaka  2011/12    itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti    matumizi,       nanukuu         “kupunguza          malipo      ya     posho      mbalimbali    yasiyokuwa  na  tija  (uk.53)  “  ,    ukweli  ni  kuwa  Bajeti  ya  serikali  ya    mwaka  2011/12  imetenga  jumla  ya  shilingi  0.987  trilioni  ambazo  ni    sawa  na  asilimia  13  %  ya  bajeti  yote  ya  matumizi  ya  kawaida  ya    serikali  na asilimia 6% ya Bajeti yote kwa ajili ya kulipa posho. Kambi    ya  Upinzani  inahoji,  je,  Waziri  atapunguza  posho  zipi  na  kwa  kiasi    gani  wakati  tayari  ametenga  kiasi  cha  sh.  Trilioni  0.987  kwa  ajili  ya    posho.      

 Mheshimiwa Spika,     Wakati       Waziri    wa     Fedha       akisema       kuwa       ili  kudhibiti    matumizi    watapunguza  posho  mbalimbali,  wakati  huo  huo  katika  hotuba    yake  uk.  66,  anapendekeza  kufanywa  kwa  marekebisho  ya  sheria    ya  kodi  ya  mapato  SURA  332  na  anasema  kwenye  (i)  “kusamehe    kodi   ya   mapato   kwenye   posho   wanazolipwa   wafanyakazi   wa    serikali   na   wanaofanya   kazi   kwenye   taasisi   zinazopata   ruzuku    kutoka kwenye bajeti ya serikali”. Sasa tumeanza kusikia vilio kutoka    sekta binafsi kwamba na wao wapate unafuu huu wa kodi.  Kambi    ya  upinzani  inapendekeza  mfumo  mzima  wa  kulipana  posho  za    vikao   (sitting   allowances)   uondoke   katika   utumishi   wa   umma.    Ninaomba  ieleweke  kuwa  hatupingi  posho  za  kujikimu  ambazo    viongozi  au  maafisa  wa  umma  hulipwa  wanaposafiri  nje  ya  vituo    vyao  vya  kazi.  Posho  hizi  zirekebishwe  kuendana  na  gharama  za    maisha   za   sasa.   Lakini   Posho   za   vikao   zifutwe   mara   moja.   Ili    kuonyesha kuwa Viongozi wa kisiasa tunaelewa kilio cha wananchi    kuhusiana   na   gharama   za   maisha   na   kupunguza   matumizi   ya  serikali,  waheshimiwa  Wabunge  tunaanza  na  posho  za  vikao  vya        Bunge. Iwapo sisi tukiendelea kujilipa posho za kukaa humu ndani na        kwenye  kamati  zetu,  tunakuwa  tunatoa  ruhusa  kwa  watumishi  wa       Serikali kulipana posho hizi na hatutakuwa na mamlaka ya kuwahoji        na kuwawajibisha. Mfumo wa Posho za Vikao ni rushwa ya kitaasisi       wanaojipa   watu   wenye   mamlaka.   Wakati   kiongozi   wa   umma        anapolipwa posho kwa kikao cha kufanya maamuzi yanayohusiana        na  majukumu  yake  ya  kazi  ambayo  kwayo  analipwa  mshahara,        Polisi halipwi posho kwa kulinda, Mwalimu halipwi posho kwa kuingia        darasani  na  wala  Nesi  halipwi  posho  kwa  kusafisha  vidonda  vya       wagonjwa.      

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inashauri kufanya marejeo ya        mfumo  wa  posho  na  mfumo  wa  mishahara  kwa  watumishi  wa        umma.       Suala     hili  ni  lazima     tulianze     sasa     na    katika    Bajeti    hii        tunayoijadili.  Lazima  kuwaonyesha  Watanzania  kuwa  tunajali  hali       zao ili kurejesha imani ya Umma kwa Wanasiasa na viongozi wao.            

Mheshimiwa  Spika,  vipaumbele  sita  vilivyotolewa  katika  hotuba  ya Mheshimiwa Waziri ni: Fedha zimewekwa  katika
Tshs. Billioni    Miundombinu-Barabara,reli, bandari na mkongo wa Taifa                                           2,781.40
Nishati     na   Madini                                                                                           539.3
Maji                                                                                             621.6
Kilimo na Umwagiliaji                                                                            926.2
Elimu                                                                                            2,283.00
Afya                                                                                             1,209.10                                                              JUMLA KWA SEKTA SITA                                                                                              8,360.60      

Mheshimiwa Spika, Tshs 8.361 Trilioni ni kwa ajili ya Sekta sita tu ambayo ni sawa na  asilimia 62% ya      bajeti nzima.     Katika kufanya uchambuzi katika vitabu vya bajeti imeonyesha kuwa     hizo sekta sita zimo kati ya mafungu 15 ambayo yamepangiwa fedha     nyingi  ambayo  ni  pamoja  na  deni  la  taifa  ambalo  ni  sh.  1.9  trilioni.     Hivyo  basi,  ukiongeza  mafungu  mengine  sita  ambayo  ni  fungu  (21,     28,30,37,38 na 57) unapata jumla ya Tshs.12,586.11Trilioni.     Mheshimiwa Spika, Jumla ya bajeti nzima kwa mwaka huu ni Tshs.13,     525.90 Trilioni. Kwa mahesabu ya kawaida ni kwamba kuna tofauti ya     Tshs.939.8 bilioni kati ya matumizi kwa sekta za vipaumbele pamoja na     idara zingine zilizopewa fedha nyingi na Bajeti kuu. Mgawo wa fedha     za serikali kwa mafungu 15 ya juu ni kama ifuatavyo.      

SUMMARY OF PUBLIC EXPENDITURE AND DEVELOPMENT FUNDS FOR MINISTRY/ DEPARTMENTS AND AGENCIES -        S/N         VOTE            DESCRIPTION                                             PUBLIC EXPENDITURE                                                                                           AMOUNT                PERCENTAGE              
 1              22  Public Debt and General Services                        1,901,850,995,000              
2              98  Ministry of Works                                         245,440,294,000            
  3              21 The Treasury                                             1,000,073,144,000              
4              46  Ministry of Education and V. Training                     523,778,766,000                     8.3                5              52  Ministry of Health and Social Welfare                     219,367,376,000              
6              50  Ministry of Finance                                         85,794,616,000              
7              49  Ministry of Water                                           17,455,673,000              
 8              38  Defence                                                   415,416,165,000              
 9              58  Ministry of Energy and Minerals                             76,953,934,000            
 10              28  Ministry of Home Affairs - Police Force                   276,144,464,000            
 11              30  President's Office and Carbinet Secretariat               200,519,723,000            
 12              43  Ministry of Agriculture, Food and Cooperation             152,406,152,000              
13              62  Ministry of Transport                                       69,585,672,000            
 14              57  Defence and National Service                                14,973,547,000                                                               15            37  Prime Minister's Office                               32,291,737,000        

 Mheshimiwa Spika,    Kambi ya Upinzani inaona kuwa bajeti  hii  ni  ya  nadharia zaidi  kwani    kwa  hali  ya  kawaida  Wizara  na  idara  za  serikali  zilizobakia  haziwezi    kutumia  Tshs.939.8  bilioni  tu!  Hapa  inaonyesha  bajeti  iliyosomwa  na    Mhe  Waziri  ilikuwa  na  lengo  la  kuwafumba  macho  watanzania  na    kuwapa matumaini tu. Hili ni jambo la hatari kwani mara zote ukweli    uliofichwa  pindi  utakapofichuliwa  kwa  njia  yeyote  madhara  yake    yanakuwa ni makubwa sana.    Mheshimiwa  Spika,  licha  ya  uchambuzi  hapo  juu  utagundua  kirahisi    kabisa  kuwa  Waziri  wa  Fedha  amerundika  Fedha  za  Miundombinu    kwa  pamoja  ili  kuhadaa  Umma.  Ukiangalia  vitabu  vya  Bajeti  utaona    kuwa katika Tsh 2.8 trilioni zilizotengwa kwa miundombinu, Tsh 1.5 trilioni    ni  kwa  Wizara  ya  Ujenzi  peke  yake  na  kuacha  fedha  nyingine  kwa    Wizara  zilizobakia.  Utaona  kuwa  Wizara  ya  Uchukuzi  inayosimamia    sekta nyeti kama Reli, Bandari, usafiri wa majini na Shirika la Ndege la    Taifa  imetengewa  fedha  kidogo  sana  ambazo  ni  Tsh  69  bilioni  kwa    matumizi  ya  kawaida  na  Tshs  167  bilioni  kwa  Maendeleo.  Shirika  la    Ndege, Shirika la Reli na Shirika la Usafiri majini  (MSCL) hazijatengewa    fedha za kuweza kuyafanya mashirika haya yaanze kazi mara moja,    kwa ufanisi na kutengeneza faida miaka ya usoni.          
 Mheshimiwa Spika,                                                      
    Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/12 imewaongezea mzigo mkubwa    sana  wananchi  na  hasa  wajasiriamali  wadogo  na  vijana  ambao    wamejiajiri  ama  kuajiriwa  kwenye  biashara  ya  usafiri  na  usafirishaji.    Kwani  serikali  inapendekeza  kufanyika  kwa  marekebisho  ya  sheria    ya  usalama  barabarani  sura  168  ili  kuongeza  ukomo  wa  kiwango    cha      faini    inayotozwa          kwa      kufanya        makosa        wakati       akiwa    anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000    hadi  shilingi  300,000.    Ingawa  Waziri  alitamka  kwa  maneno  kuwa    faini  itakuwa  Tshs  50,00  kwenye  kitabu  cha  hotuba  yake  ni  Tshs    300,000.   Kambi  ya   Upinzani   haipingi   adhabu   kwa   wakosaji   wa    makosa   barabarani   isipokuwa   tuna   wasiwasi   kuwa   adhabu   hii    itasababasha  rushwa  kuongezeka.  Ila  ikisimamiwa  vizuri  itapelekea    kupunguza ajali barabarani.        Mheshimiwa spika,    Ongezeko  hili  la  faini  ni  kubwa  sana  na  litawaangamiza  kabisa    kibiashara vijana ambao wamejiajiri kwenye biashara ya usafirishaji    kama vile daladala, taxi, bajaji na pikipiki .    Kambi  ya  Upinzani  inapinga  marekebisho  haya  ya  sheria  kwani    yataathiri maisha ya watanzania wengi ambao watakuwa sasa kila    mara  wanafanya  kazi  kwa  ajili  ya  kulipia  faini  polisi  badala  ya    kuweza  kukuza  uchumi wao.  Kwa  mfano,  kama  dereva wa pikipiki    atakutwa na makosa matatu, mathalani la kusahau leseni, kutovaa    helmenti  na  kutovaa  vazi  maalum  kwa  ajili  ya  kuendesha  pikipiki    atapaswa  kutozwa  faini  ya  shilingi  900,000  ambazo  ni  sawa  na        gaharama ya kununua pikipiki nyingine mpya.      
Mheshimiwa Spika,    Bajeti  ya  Serikali  ya  mwaka  2011/12  haijalenga  katika  kuimarisha    uchumi kwani fedha zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni kiasi cha    shilingi  4,925  trilioni  tu  na  kati  ya  fedha  hizo  shilingi  1,871  trilioni  ni    fedha za ndani na nyingine zilizobakia kiasi cha shilingi 3,054 trilioni ni    fedha  za  nje.  Hivyo  basi,  kama  wahisani  hawatatoa  fedha  kama    ambavyo  hali  hiyo  imekuwa  ikitokea  mara  kwa  mara  ni  kuwa    maendeleo  hayataweza  kupatikana  kwani  hakuna  fedha  kwa  ajili    ya kuendesha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.        Kambi ya Upinzani, inaona kuwa serikali bado haijaamua kuliondoa    taifa hili katika lindi la umaskini kwani hatutengi fedha zetu za ndani    kwa ajili ya maendeleo badala yake fedha za ndani tunatenga kwa    ajili ya shughuli za kawaida ambazo si za maendeleo.                              
  BAJETI MBADALA YA KAMBI YA UPINZANI    
Mheshimiwa Spika, zifuatazo ni dondoo za Bajeti Kivuli inayotolewa   na Kambi ya Upinzani Bungeni.      Dondoo za Bajeti Mbadala        
•    Kuongeza  mapato  hadi  kufikia  Shilingi  trilioni  14.160  kutoka           trilioni 13.525 za Serikali.                                                      
        •  Tumeongeza  mapato  ya  ndani  hadi  trilion  8.68  kutoka  6.7  za          serikali.    
 •  Tumeondoa kukopa mikopo ya kibiashara na hii inatokana na          ukweli kwamba kufanya hivyo ni kuliongezea taifa gharama za          kulipa  madeni  yenye  riba  kubwa  na  pia  hili  linafanya  uchumi          kuathirika  kwani  serikali  inakuwa  ikishindana  na  sekta  binafsi          katika  kuchukua  mikopo  kwenye  taasisi  za  fedha  na  hivyo          kuathiri uchumi.  
  •  Tumeondoa   posho   mbalimbali   ambazo   ni   0.987   trilioni   na          kuzipeleka   kwenye   kuboresha  Mishahara   ya   Watumishi  wa          Umma na katika bajeti ya maendeleo.    
•  Tumepunguza  matumizi  ya  kawaida  ya  serikali  kutoka  trilioni          8,600,286 na kuwa 7.913.    
 •  Tunapendekeza kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya          umeme na  Gesi ili kumaliza kabisa tatizo la nishati ya Umeme.          Vilevile kuchochea matumizi ya Gesi majumbani.    
•  Tutakusanya  mapato  ya  ndani  kwa  22.84%  ya  pato  la  Taifa          ukilinganisha na serikali ambao watakusanya 17%.    
 •  Tumepunguza misaada na mikopo kutoka nje na kuwa 27.54 %          ya bajeti wakati ya serikali ni 29%.    
•  Kutoka  Vyanzo  vipya  vya  mapato  tumeongeza  1.905  trilioni          ambavyo ni vyanzo havikusanywi na serikali na kupanua wigo          wa kodi na kurekebisha sheria za kuzuia ukwepaji wa kodi (anti          tax avoidance measures) na kuboresha mfumo wa Kodi.    
•  Tunapendekeza           kurahisisha      mfumo       wa     kodi    ya    Mapato          (Personal  Income  Tax)  na  kwamba  sasa  kila  Mtanzania  ajaze          fomu  za  kodi  (tax  returns)  kwa  mujibu  wa  sheria  hata  kama          hana kipato.    
 SERA YA MAPATO .
 Kuongeza mapato ya nchi kutoka katika bidhaa za misitu .                                              
    Mheshimiwa Spika ,    Katika  kuhakikisha  kuwa  bidhaa  mbalimbali  zitokanazo  na  misitu   kama  vile  mbao  ,  madawa,  magogo  na  asali  zinatumia  kikamilifu   katika kuliongezea taifa kipato hatua zifuatazo zitachukuliwa ;        
 (i)    Kuhakikisha  kuwa  Magogo  yote  yanayosafirishwa  nje  ya                  nchi  yanalipiwa  kodi  .  Tunashauri  kuimarisha  usimamizi                  bora  wa  uvunaji  wa  bidhaa  hizi  za  misitu  na  kuifanya                  idara ya Misitu na Nyuki kuwa Wakala wa Serikali. Juhudi                  zitawekwa  katika  kuhakikisha  kwamba  Bidhaa  nyingi  za                  Misitu  zinatumika  hapa  nchini  kuzalisha  Fenicha  kufuatia                  amri ya kutonunua Fenicha kutoka ughaibuni.        
 (ii)   Kutafuta soko la uhakika la asali kwa ajili ya kupata fedha  za  kigeni  kwenye  masoko  ya  Ulaya  na  Marekani  kwani yametawaliwa na asali kutoka nchi za Amerika ya Kusini kama  Brazili  na  Argentina  .  Lengo  la  kuongeza  juhudi katika  eneo  hili  ni  kusaidia  jamii  za  warina  asali  kupata  soko na nchi kufaidika na kodi na pia mauzo nje na hivyo                  kupata fedha za kigeni.       kupunguza misamaha ya kodi.        
  Mheshimiwa Spika ,    Kiwango   cha   misamaha   ya   kodi   zinazotolewa   na   Tanzania   ni   kikubwa  mno.  Hii  inaonekana  wazi  kwa  kulinganisha  kiwango  cha   misamaha  ya  kodi  kinachotolewa  Tanzania  na  kile  kinachotolewa   katika nchi za Uganda na Kenya. Nchini Tanzania kati ya miaka ya   2005/06 na 2007/08 misamaha ya kodi ilikadiriwa kuwa wastani wa   asilimia  3.9  ya  pato  la  taifa.  Mwaka  2008/09  misamaha  ya  kodi   ilikuwa  asilimia  2.8  ya  pato  la  taifa  na  mwaka  2009/10  asilimia  2.3.   Ukilinganisha na Kenya na Uganda misamaha ilifikia asilimia 1 na 0.4   ya pato la taifa la kila nchi husika kwa mtiririko huo.                                                  
       Mheshimiwa Spika ,      Kama  Tanzania  ingerekebisha  viwango  vya  misamaha  ya  kodi  ili   kulingana na kiwango kilichofikiwa na Kenya, zaidi ya TZS 600 bilioni   zingeokolewa kwa mwaka 2007/08 peke yake. Ukubwa wa kiwango   cha misamaha inayotolewa unaweza kuelezewa kwa kukilinganisha   na  malengo  ya  ukusanyaji  wa  mapato  ya  kodi  ambayo  Tanzania   inashindwa  kuyafikia.  Katika  mwaka  2008/09  na  2009  10  Serikali   haikutimiza lengo lake la mapato kwa wastani wa TZS 453 bilioni kila   mwaka.  Katika  kipindi  hicho  hicho,  misamaha  ya  kodi  iliyotolewa   ilifikia  wastani  wa  TZS  724  bilioni  kwa  mwaka.  Mpaka  mwaka  2011   mwezi Juni Msamaha wa Kodi unakadiriwa kuwa TZS 930 bilioni kwa   mujibu wa Taarifa ya TRA kwa kamati ya Fedha na Uchumi.      Kama misamaha ya kodi ingetolewa katika kiwango kinachofanana   na  kiwango  cha  misamaha  ya  kodi  inayotolewa  Kenya, TZS  bilioni   484 zingeokolewa mwaka 2008/09 na TZS bilioni 302 mwaka 2009/10.   Kwa  maneno  mengine,  upungufu  katika  ukusanyaji  wa  mapato   ungepunguzwa kwa kiasi kikubwa.      Kambi   ya   Upinzani   inaipongeza   Serikali   kwa   kukubali   wazo   la   kupunguza misamaha ya Kodi mpaka kufikia Asilimia moja ya Pato   la Taifa.   Mheshimiwa  Spika  hata  hivyo  Kambi  ya  Upinzani  inapendekeza   kupitia  upya  vivutio  vinavyotolewa  na  TIC  kwa  wawekezaji  kwa   kupiga        marufuku         msamaha           wowote         wa      kodi     kwa      bidhaa   zinazozalishwa nchini ili kulinda viwanda vya ndani.                 Sekta ya madini na makampuni ya kimataifa (multinationals)      Mheshimiwa Spika ,   Katika tathmini ya Hali ya Uchumi 2010 tumeonyesha ni namna gani   ambavyo  sekta  ya  Madini  imekuwa  haichangi  mapato  ya  ndani.                                                  
    Katika Mwaka huu wa Fedha  Taifa letu litakusanya Tshs 99.5 Bilioni   kutoka   katika   Mrahaba   kwenye   Madini   yanayochimbwa   nchini   kwetu. Mapato haya ya Mrahaba kwa mwaka ujao ujao wa Fedha   ni aslimia 4.5 tu ya Mauzo ya Dhahabu peke yake nje ya nchi.       Mheshimiwa Spika, Kwa Upande wa kodi nyingine zinazokusanywa   kutoka katika sekta ya Madini inakuwa ni vigumu kuweza kujua kiasi   gani  twakusanya  kwani Kampuni zote zalundikwa katika kapu moja   la   Idara   ya   Walipa   Kodi   Wakubwa.   Kwa   takwimu   za   Mwaka   2009/2010  mapato  yote  ya  kikodi  pamoja  na  mrahaba  na  malipo   kwa mifuko ya Pensheni (ambayo sio kodi) katika sekta ya ya Madini   yalikuwa   takribani   shilingi   256   bilioni   ambazo   zilikuwa   sawa   na   asilimia 16 ya thamani ya mauzo ya Madini nje ya nchi.       Mheshimiwa   Spika,   kuna   haja   ya   kuhakikisha   Taifa   linakusanya   mapato ya kutosha katika sekta ya Madini ili kuleta maendeleo ya   Wananchi wetu. Katika kuhakikisha kuwa tunaongeza ukusanyaji wa   Mapato ya kutosha kutokana na sekta ya Madini na makampuni ya   kimataifa tutachukua hatua kadhaa.       Mheshimiwa Spika,    Makampuni           makubwa          ya     kimataifa       (MNC)       hutumia        mbinu   mbalimbali kupunguza kodi wanazolipa kwenye nchi zinazoendelea.   Nchi     yetu     imekuwa        ikikaribisha     wawekezaji        wakubwa          kwenye   maeneo  mbalimbali  hasa  sekta  za  Madini  na  Mawasiliano,  hata   hivyo,  kwa  muda  mrefu  wa  uwekezaji  wao  wamekuwa  wakipata   misamaha ya kodi na pia kutolipa kodi ya makampuni ama kodi ya   “capital gains” wanapouziana makampuni hayo.    Mheshimiwa Spika,    Mfano  mzuri  ni  wa  kampuni  za  Madini  ambazo  hutumia  sehemu   kubwa  ya  uwekezaji  wao  kama  mkopo  (debt  financing),  njia  hii                                                     huwezesha         wawekezaji         (shareholders)        kupata       faida      (return)   mapema   zaidi   kuliko   kuweka   mtaji   (share   holders   equity).   Hii   inatokana  na  ukweli  kwamba    riba  huondolewa  katika  kukokotoa   kodi  ambayo  kampuni  hulipa.  Katika  kipindi  cha  kati  ya  mwaka   2001-2009  kiwango  cha  kodi  ambacho  kingelipwa  serikalini  iwapo   makampuni  ya  madini  yangewekeza  mtaji  wa  angalau  30%  ya   uwekezaji       kwenye       migodi      yao    kingelikuwa       takribani      dola    za   Kimarekani 830 milioni.    Mheshimiwa Spika,    Mifano ya asilimia ya mikopo katika Mitaji ya makampuni ya madini   hapa   nchini   ni  kama  ifuatavyo  (Chanzo  Masha   Mining   Review   Report);           (i)    Geita Gold mine –                   12,597,000 %          (ii)   Bulyanhulu Gold mine –              791 %          (iii)  Resolute Gold mine –                5088%    Mheshimiwa Spika,    Utaona  kuwa  kwa  muundo  huo  wa  mitaji  ya  Makampuni  haya   matatu  tu  ni  namna  gani  ambavyo  sehemu  kubwa  ya  Fedha   zinazotokana  na  faida  wanayopata  kwenye  mauzo  ya  dhahabu   huishia kulipia Madeni na Riba na hivyo kukosesha Serikali mapato.   Hii   kwa   wataalamu   wa   kodi   inaitwa   ‘tax   planning   measures’.   Muundo  huu  wa  mitaji  ya  uwekezaji  itapelekea  makampuni  haya   kutangaza hasara kila mwaka.    Mheshimiwa Spika,    Vilevile    kwenye        sekta     ya     Mawasiliano,        kampuni        ya    Celtel   International  ilifungua  kampuni  huko  Netherlands  (Celtel  Tanzania   BV)  ambayo  ndio  inamiliki  Celtel  Tanzania  limited.  Hivyo  uuzaji  wa   Celtel   kwenda   Zain   na   baadaye   kwenda   Airtel   haukulazimisha   kubadilishwa  kwa  mmiliki  wa  celtel  Tanzania  limited  na  hivyo  kwa   kutumia mikakati ya kiumiliki (ownership structure) kila mara kampuni   hii  ilipouzwa  serikali  haikuweza  kukusanya  kodi  yake.  Kwa  mfano,   kwenye  mauzo  ya  Zain  kwenda  Airtel  serikali  ingeweza  kukusanya   dola za Kimarekani 312 milioni.    
 Mheshimiwa Spika,    Kwenye   sekta   ya   Viwanda,   Kampuni   ya   Bia   Tanzania   ambayo   inamilikiwa  na  SABMILLER  nayo  pia  imeripotiwa  kutumia  njia  ya   kimkakati  kukwepa kodi  ikiwemo kusajili hatimiliki na hivyo kupata   mrahaba ambao hautozwi kodi , mfano ni kwenye pombe aina ya   CHIBUKU      ambapo   jina   hilo   limesajiliwa   huko   Netherlands   na   kampuni tanzu ya TBL. Inasemekana Tanzania imepoteza karibu dola   milioni 2 kila mwaka kutokana na mpango huo.
 Mheshimiwa Spika,    Kambi   ya   upinzani   Bungeni   tunapendekeza   hatua   zifuatazo   ili   kuweza       kukabiliana       na    ukwepaji       huu    wa     kodi    na    hatimaye   kuliongezea taifa mapato;        
(i)    Kutunga  sheria  kwa  kuimarisha  zaidi  sheria  ya  Kodi  ya                 Mapato ya mwaka 2004 kwamba, mikopo ya makampuni                 kwenye uwekezaji, kwa sababu za kikodi, isizidi asilimia 70                 ya  mtaji  wote  uliowekezwa  na  hii  ianze  mara  moja  bila                 kujali mikataba iliyopo.        
(ii)   Kutunga sheria kuhakikisha kwamba Riba kwenye mikopo                 kutoka        Makampuni           yanayohusiana           haitaondolewa                 kwenye kutoza kodi.        
 (iii)  Kuhakikisha        kwamba        mauziano        ya    Kampuni        yeyote                 ambayo  mali  zake  zipo  Tanzania  tunakusanya  kodi  ya                 asilimia 30 % kama ‘ongezeko la mtaji’ (‘capital gains’).            
 Kurekebisha Kodi za Mafuta                                        
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapongeza hatua ya   Serikali  kuchukua  wazo  la  Kambi  ya  Upinzani  la  kupunguza   Kodi na tozo kwenye Bidhaa za mafuta ili kupunguza Bei ya   Bidhaa   hizi   na   hivyo   kupunguza   ukali   wa   maisha   kwa   wananchi.   Ingawa   Serikali   haijasema   kiwango   cha   kodi   kitakachoondolewa,              tunapendekeza            kuwa      ushuru      wa   barabara  (road  toll)  usipunguzwe  ili  kubakia  na  Fedha  za   kutosha kukarabati barabara ambazo tunazijenga kwa kasi.   Tunapendekeza   Ushuru   wa   Bidhaa   kwenye   biadhaa   za   Mafuta  upunguzwe  kwa  asilimia  40  na  tozo  nyingine  zote   kwenye mafuta zipunguzwe kwa asilimia 40 pia.     Mheshimiwa          Spika,     tunapendekeza            pia    kufuta     kabisa   msamaha wa Kodi kwenye Mafuta kwa Kampuni za Madini   na Kampuni za Ujenzi kwani imethibitika kuwa msamaha huu   unapelekea upotevu mkubwa wa fedha za Umma. Takwimu   zinaonyesha kuwa kupitia misamaha hii jumla ya lita 133m za   Dizeli    ambazo       ni   sawa      na    asilimia    20    ya    Dizeli   yote   iliyoingizwa nchini, ziliingizwa nchini na Kampuni 5  za Migodi   ya Dhahabu.  na zililipa kampuni hizi zililipa dola laki mbili tu   kama  ushuru.  Mafuta  mengi  yanayoingia  kupitia msamaha   huu  hurudi  kwenye  sokona  kuuzwa  rejareja.  Misamaha  hii   ifutwe bila kujali mikataba iliyopo.         Mheshimiwa   Spika,   Kambi   ya   Upizani   Bungeni   inapinga   pendekezo la sasa la kuondoa msamaha wa kodi ya mafuta   kwa kampuni za utafutaji ya mafuta na Gesi. Msamaha huu   hauna  mantiki  kwani  Kampuni  za  utafutaji  mafuta  na  Gesi   kwa      Mujibu      wa      Mikataba        yao      (Production        Sharing   Agreements)   wataweza   kurejeshewa   gharama   hizi   bara   baada ya mafuta na Gesi kupatikana (Cost Oil).                                    
       Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema hapo juu hatua hii ya   kikodi ni ya dharura tu kwani bado inaweza kufanywa haina   maana  yeyote  kwa  kitendo  cha  bei  za  mafuta  kupanda   katika  soko la  Dunia.  Hivyo  tunahitaji  njia  endelevu nayo ni   kuhakikisha        Mafuta       yanaagizwa          kwa      wingi     na     hivyo   kupunguza         gharama         za    usafirishaji.    Mpango         wa     Bulk   Procurement   umekuwa   ukisemwa   bila   kutekelezwa   kwa   muda       mrefu      kutokana        na     nguvu       kubwa       ya    rushwa   waliyonayo   matajiri   katika            sekta     ya   Mafuta.       Ni   lazima   tuishinde  nguvu hii  hata  kama itakuwa  ni kwa baadhi  yetu   kupoteza maisha.    Mheshimiwa            Spika        Kambi         ya      Upinzani         Bungeni   inapendekeza  Serikali  kupitia  Shirika  la  Umma  la  Mafuta   (baada  ya  kurekebisha  TPDC  na  kuwa  na  Mamlaka  ya   Udhibiti  katika  kutafuta  na  kuchimba  mafuta  na  Gesi  na   Shirika la Kibiashara la Mafuta na Gesi), inunue hisa asilimia   50 zilizobakia za BP (T) Limited, kuweka mtaji wa kutosha na   kufanya  biashara  ya  Mafuta.  Nchi  nyingi  Duniani  hutumia   Mashirika yake ya Umma kwenye sekta ya Mafuta kudhibiti   Bei.  Ukienda  Dubai  Leo  vituo  vingi  vya  Mafuta  vinamilikiwa   na  Shirika  la  Umma.  Vilevile  Malaysia  licha  ya  Petronas   kushirika katika kuchimba Mafuta lakini pia inamiliki vituo vya   mafuta vya rejareja. Hii ndio hatua mwafaka ya kuchukua,   ipo  ndani  ya  uwezo  wetu  na  itaongeza  Ushindani  katika   soko na hivyo kudhibiti upandaji wa bei holela wa bidhaa za   mafuta.  Kwa  ufupi  tunashauri  BP  (T)  Limited  imilikiwe  na   Serikali  kupitia  Shirika  la  Umma  kwa  asilimia  100  badala  ya   asilimia 50 ya sasa.                                    
    Mheshimiwa            Spika,        Kambi         ya      Upinzani         Bungeni   inapendekeza  pia  kuwianisha  viwango  vya  bei  ya  Mafuta   ya  Taa  na  bei  ya  Mafuta  ya  Diseli  na  Petroli  ili  kudhibiti   uchakachuaji  wa  mafuta  ambao  unaligharimu  Taifa  fedha   nyingi sana na kuleta uharibifu mkubwa sana.        Kurekebisha mfumo wa Kodi ya Mapato    Mheshimiwa  Spika,  kupanda  kwa  gharama  za  maisha  kwa   Wananchi kumepunguza uwezo wa matumizi wa wananchi   walioajiriwa  na  kulipwa  mishahara  ambayo  inakatwa  kodi   (PAYE).  Tunatambua  kuwa  kodi  hii  ni  chanzo  kikubwa cha   Mapato  kwa  Serikali  ambapo  kwa  mwaka  huu  wa  Fedha   kinatarajiwa kuingiza takribani shilingi 450 bilioni kutoka idara   ya  Kodi  za Ndani  na Idara ya  Walipa  kodi wakubwa.  Hata   hivyo   kuna   haja   ya   kuangalia   upya   (tax   brackets)   na   kuzirahisisha kwa kuzipunguza na hata kuanza kufikiria kama   kuna haja ya kuwa na flat tax.        Mheshimiwa            Spika,       kwa       mwaka         huu       wa      Fedha   tunapendekeza             Sheria     ya     Kodi     ya     Mapato        ifanyiwe   marekebisho  na  kushusha  kiwango  cha  chini  kabisa  cha   PAYE  mpaka  asilimia 9  na  kiwango  cha  juu mpaka  asilimia   27. Uamuzi huu utawezesha wananchi kubakia na fedha na   hivyo  kutumia  katika  uchumi  na  kukuza  uzalishaji.  Uamuzi   huu  utapunguza  mapato  ya  Serikali  kwa  takribani  shilingi   bilioni 23 (asilimia 4 ya matarajio ya makusanyo ya kodi hii).        Mheshimiwa            Spika,       vile     vile     Kambi        ya      Upinzani   inapendekeza kuwa mchakato uanze ili kila Mtanzania awe anajaza  fomu  za  kodi  (tax  returns)  kila  mwaka.  Kuna  watu              wengi  sana  ambao  wanapata  mapato  makubwa  lakini              hawalipi  kodi.  Mfano,  watu  wenye  nyumba  za  kupangisha              mijini wanapata fedha nyingi sana na wengine hutoza kodi              kwa   kutumia   dola   za   Marekani   lakini   hawalipi   kodi   ya              Mapato.        Watu      hawa       hutumia       Barabara        na    huduma              nyingine za Umma ambazo gharama zake zatokana na kodi              ilhali   hawalipi      kodi.    Kambi       ya    Upinzani      inapendekeza              kuanzishwa         kwa     Real     Estate      Regulatory       Authority       na              kwamba         kila   mwenye        Nyumba         ya    kupangisha        lazima              atambuliwe na kulipa kodi inavyostahili.                               Mheshimiwa Spika, ninataka kila Mtanzania mwenye kipato              alipie  kodi  ya  kipato  chake.  Kulipa  kodi  ndio  ishara  ya              Uzalendo  na  ili  raia  aweze  kuinyooshea  kidole  serikali  yake              lazima  awe  na  uchungu  na  uchungu  unapatikana  kwa              kulipa kodi.        Kurasimisha Biashara ndogo ndogo    Mheshimiwa Spika, moja ya hatua ambayo imekuwa ikizungumzwa   siku  zote  ni  kupanua  wigo  wa  kodi.  Waheshimiwa  wabunge  wa   kambi  zote  mbili na  hata  wataalamu  mbali mbali wanarejea  sana   jambo  hili.  Imefikia  wakati  sasa  kutekeleza  jambo  hili  kwa  vitendo   kwa  kuondoa  vikwazo  vinavyofanya  Biashara  ndogo  na  za  kati   (SMEs)  zisiandikishwe.  Biashara  ndogo  na  za  kati  zinaunda  sehemu   kubwa  ya  shughuli  za  kiuchumi  nchini  na  hivyo  kuwa  moja  ya   chanzo kikubwa cha Mapato ya Serikali. Katika utafiti uliofanywa na   Shirika  la  Serengeti  Advisers  Limited  imeonekana  kuwa  licha  ya   maboresho yanayofanywa na TRA bado wafanyabiashara wadogo   na wa kati wanakutana na vikwazo vingi sana. Baadhi ya vikwazo ni   pamoja  na  vitisho  kutoka  kwa  maafisa  wa  TRA,  urasimu  na  hata   Rushwa. Pamoja na vikwazo hivyo bado SMEs zimekuwa zikichangia   kwa kiasi kikubwa kupitia kodi mbalimbali.  
 Mheshimiwa   Spika,   Kambi   ya   Upinzani   Bungeni   inapendekeza   kwamba  ushauri  wa  Mradi  wa  kuboresha  mfumo  wa  kodi   (Tax   Modernisation   Project)   ambao   ulishauri   kwamba   kuna   haja   ya   kuainisha  Kodi  ya  VAT  na  Presumptive  Tax  utekelezwe.  Tungeshauri   kuwa      kodi     anayotozwa          mfanyabiashara            ndogo       ndogo       kabla   hajaanza  kufanya  biashara  ifutwe  kabisa.  Uamuzi  huu  utapunguza   mapato ya Serikali (Shilingi 18 bilioni kwa mujibu wa Kitabu cha Bajeti   Vol.  I)  katika  kipindi  cha  muda  mfupi  lakini  itakuwa  ni  chanzo   kikubwa sana cha mapato katika kipindi cha muda mrefu.        Ada ya Leseni za Biashara    Mheshimiwa Spika,   Kambi  ya  Upinzani  Bungeni  inaona  kurejeshwa  kwa  leseni  kwa   biashara ndogo ndogo licha ya kuongeza mapato ya Halmashauri   za  Wilaya,  Miji,  Manispaa  na  Majiji  kutarejesha  ugumu  wa  kufanya   biashara. Madhumuni ya kuondoa leseni yaliyofanywa mwaka 2003   bado yana maana. Tunashauri uamuzi huu uangaliwe upya.      Msamaha wa Kodi kwenye Nyaya za Umeme      Mheshimiwa Spika,   Kambi  ya  Upinzani  inapendekeza  kufutwa  kwa  msamaha  wa  kodi   kwenye  orodha  ya  misamaha  kwa  nyaya  za  Umeme  (Removal  of   duty  remission  on  electric  wires  and  cables  (as  deemed  capital   goods)        through       Tanzania        Certificate        of    Incentive        scheme   administered  by  TIC).  Uamuzi  huu  utalinda  viwanda  vya  ndani  na                                                       kulinda        ajira    za     Watanzania            walioajiriwa         kwenye         viwanda   vinavyotengeneza nyaya za umeme.        
Muhtasari  wa  vyanzo  nyongeza  vya  mapato  kwa  bajeti  mbadala   2011/2012 (Shilingi)        1. Kurekebisha Kodi katika Misitu                                                                                                                                          100bn    
2.  Kurekebisha misamaha ya kodi                                                                                                                                        555bn    
 3.  Mauzo ya hisa za Serikali   550bn    
4.  Kurekebisha Kodi Sekta ya Madini 240bn    
5.  Kuimarisha usimamizi wa mapato ya Wanyamapori                                                                                                                                  81bn    
6.  Kuondoa msamaha wa ushuru wa mafuta Kampuni za Madini                                                                                         59bn    
7.  Usimamizi wa Mapato katika Utalii                                                                                                                                            68bn    
 8.  Kuimarika kwa Biashara na EAC  150bn
 Jumla  1905bn

 SERA YA MATUMIZI    Vipaumbele vya bajeti ya Matumizi.                    
(i)     Ukuaji  wa  uchumi  vijijini  (rural  growth)  kwa  kuboresha                   miundo         mbinu         ya     umeme,           barabara          na      maji.                   Tunapendekeza  kutumia  shilingi  450  bilioni  kila  mwaka                   (Bilioni  150  kwa  kila  sekta)  kwa  miaka  5  mfululizo  katika                   sekta hizi vijijini. Ujenzi wa barabara za vijijini utatumia kwa                   kiasi    kikubwa         nguvukazi         watu      (labour       intensive)       ili                   kuongeza kipato na kukuza matumizi ya Kaya vijijini kufikia  lengo la kupunguza umasikini wa vijijini mpaka asilimia 20          kutoka asilimia 37 ifikapo mwaka 2015.
(ii)    Ujenzi wa barabara na madaraja
 (iii)  Nishati  (umeme  na  gesi  asilia)  kuhakikisha  tunazalisha          360MW  za  umeme  kila  mwaka  ili  kufikia  malengo  ya          Mpango wa Maendeleo wa miaka Mitano. Pia kuwekeza          katika  Bomba  la  Gesi  kutoka  Mtwara,  matumizi  ya  Gesi          kwenye   nyumba   za   Dar   es   Salaam   na   mtambo   wa          kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant).
(iv)   Rasilimali watu (kuboresha Elimu na afya)  
(v)    Kuongeza         Kima      cha      chini     cha      Mshahara          kwa          Wafanyakazi  wa  Umma  mpaka  Tshs  315,000  kwa  Mwezi          na kutoa motisha kwa Walimu wanaofundisha Vijijini kwa          kuwapa   Mshahara   mara   moja   na   nusu   ya   wenzao          wanaofundisha mijini.
(vi)   Uchukuzi (reli, bandari na Shirika la ndege )
(vii)  Kujenga       Uwezo       wa      Wakandarasi         wa      ndani      kwa          kurekebisha   Sheria   mbalimbali   ili   kuhakikisha   kuwa
(i)          miradi yote ya Ujenzi nchini isiyozidi shilingi 30 bilioni iwe ni          kwa  ajili  ya  Watanzania  tu  na  kama  Mtanzania  hana          uwezo  ataalika mgeni kwa mapenzi  yake.
(ii)Miradi yote          ya  Ujenzi  inayozidi  Shilingi  30  bilioni  itakuwa  wazi  kwa          zabuni  za  ndani  na  nje  hata  hivyo  Kampuni  ya  kigeni          itayayopata Zabuni ni lazima iwe na ushiriki wa Mtanzania          kwa angalau asilimia 30 na
 (iii) Vifaa vyote vya ujenzi na          hasa   vile   vinavyozalishwa   nchini   vinunuliwe   nchini   na          itakuwa   ni   marufuku   kwa   Kituo   cha   Uwekezaji   kutoa          ruhusa     ya    msamaha         wa     kodi    kwa     makampuni          ya          uwekezaji   kwa   bidhaa   zinazozalishwa   nchini   na   hasa          Saruji.  Lengo  la  hatua  hii  ni  kuhakikisha  fedha  za  miradi          mikubwa  ya  Maendeleo  ya  Ujenzi  zinabaki  nchini  na                                                           kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Watanzania, kuongeza                 ajira na uzalishaji viwandani.          (viii) Pensheni ya uzeeni.      
 (ix)   Kuondoa  ada  Kwa  wanafunzi  wa  Shule  za  Sekondari  za                 Kutwa  na  kupunguza  ada  kwa  sekondari  za  Bweni  kwa                 kiwango cha asilimia hamsini kwa wavulana na bure kwa                 wasichana. Kwa kuwa kuna wanafunzi 1.6m katika shule                 za    Sekondari      nchini,    gharama        za    shilingi   32   bilioni                 zitakazopotea  zitalipwa  na  Serikali  kutoka  vyanzo  vipya                 vya mapato.        
(x)    Kuuza  nje  bidhaa  za  kilimo  na  mifugo  zilizoongezewa                 ubora.        
 (xi)   Kupunguza mzigo wa Matumizi ya Magari ya Serikali kwa                 kuweka  mfumo  wa  Viongozi  na  watumishi  ambao  stahili                 zao  zinapaswa  kupewa  magari  watakopeshwa  magari                 na kupewa posho ya mafuta. Magari kadhaa yatawekwa                 ‘pool’ na mengine yote yatapigwa mnada. Benki Kuu ya                 Tanzania      tayari   inatumia       mfumo      huu     ambapo   hata                 Gavana        wa      Benki     Kuu     sasa    amekopeshwa            gari.                 Tunatumia uzoefu wa Taasisi hii ya Serikali kwa Idara zote                 za     Serikali,     Mawizara,Mikoa,Mashirika               ya      Umma                 yanayopata Ruzuku ya Serikali na Serikali za Mitaa     MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO.        Mheshimiwa Spika,    Kama taifa tumezindua mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka    mitano      2011/2012       –   2015/2016       na     jana    bunge       lako    tukufu    limeupitisha        pamoja         na      mapendekezo            yaliyotolewa          na    waheshimiwa wabunge.    Mpango   unahitaji   wastani   wa   Shilingi   Trilioni   8.6   kila   mwaka   ili kuutekeleza,  na  fedha  zote  hizi  za  utekelezaji  wa  mpango  huu  ni    fedha za bajeti ya maendeleo. Katika bajeti iliyosomwa na Waziri wa    Fedha  Mh.  Mkullo  bajeti  ya  maendeleo  ni  Shilingi  Trilioni  4.9  tu    ambayo  ni  sawa  na  asilimia  36.3  ya  bajeti  yote  ya  serikali  kwa    mwaka huu.         MheshimiwaSpika,  ili  kuanza  kutekeleza  mpango  wa  maendeleo    kuanzia mwaka huu wa fedha, na iwapo tungesema fedha zote za    maendeleo   mwaka   huu   zitekeleze   mpango   huu,   ingekuwa   ni    asilimia   56.9   ya   fedha   zinazohitajika   kuutekeleza   mpango   kwa    mwaka.        Hii  inaonyesha         kuwa      serikali    haina     nia    ya    dhati     ya    kuutekeleza  mpango  huu  wa  kitaifa.  Kushindwa  kutenga  fedha  za    kutekeleza        mpango        huu     kwa     mwaka        huu,     kutapeleka        mzigo    mkubwa wa bajeti ya mpango huu katika mwaka ujao wa fedha.    Kambi ya upinzani inaona kuwa kuna ulazima wa kuanza kutekeleza    baadhi ya miradi ya maendeleo katika mwaka huu wa fedha.        1. Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa fedha Mhe. Mustafa Mkullo        akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti ya mwaka huu        ni   kumaliza       tatizo    la   Umeme         na    hivyo     kutamka        kwamba        ametenga  shilingi  537  Bilioni,  upembuzi  uliofanywa  na  Kambi  ya        Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV fungu la        58) vilivyotolewa na serikali, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na        Madini  imetengewa  jumla  ya  shilingi  402.4  bilioni.  Fedha  hizo        zimegawanywa  katika  mafungu  ya Matumizi  ya  kawaida  shilingi  76.95     bilioni    na     kwa      upande        wa     bajeti     ya     Maendeleo    zimetengwa  shilingi  325.4  bilioni.  Shilingi  Bilioni  325  zilizotengwa    katika   Bajeti  ya  Maendeleo  ya   Wizara  ya  Nishati   na  Madini    zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es    Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme    unaoonekana katika Bajeti hii.        Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo ya mpango wa kwanza wa    maendeleo  wa  miaka  mitano,  katika  uzalishaji  umeme  ambapo    kama taifa tumepanga kuzalisha megawati 1788 za ziada kutoka    MW   1034(installed   capacity)   zilizopo   sasa,   tunahitaji   kuzalisha    wastani  wa  MW  358  kila  mwaka  kwa  miaka  mitano.  Hivyo  basi,    ukiondoa        mradi      wa     MW      160    ambao        tayari     umeanza        na    umetengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu, tunahitaji mradi    mwingine wa angalau MW 200 ndani ya mwaka huu wa fedha.    Mradi  ambao  unaweza  ukatekelezwa  kwa  haraka  ni  mradi  wa    Kiwira awamu ya kwanza MW 200.     Taasisi za NSSF na STAMICO zimeonyesha nia ya kutekeleza mradi    huo  bila  ya  kutegemea  fedha  ya  bajeti  ya  serikali.  Kambi  ya    Upinzani  inapendekeza  mradi  huu  kuingizwa  katika  utekelezaji    ndani      ya    mwaka        huu    wa     fedha.      Kambi      ya    Upinzani      pia    inapendekeza kutenga fedha za ndani kutekeleza mradi wa njia    za   kusafirisha   umeme   huu   kutoka   Kiwira   mpaka   Mbeya                        na    usambazaji huu utekelezwe na TANESCO.                                                   40    
  Mheshimiwa  Spika,  miradi  iliyosalia  ya  Mchuchuma  na  Ngaka    (Makaa ya Mawe), Mtwara – Somanga Fungu na Kinyerezi ( gesi    asilia)  na  Ruhudji  (Maji)  ielekezwe  kwa  taasisi  zilizoainishwa  kwa    ajili ya utekelezaji na serikali kuingia makubaliano na taasisi hizo ili    kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati.        Mheshimiwa  Spika,  madhara  ya  ukosefu  wa  umeme  kwenye    Uchumi   wa   Taifa   ni   makubwa   sana.   Mamlaka   ya   Mapato    Tanzania  ilinukuliwa  kusema  kuwa  Mgawo  wa  Umeme  uliotokea    mwanzoni  mwa  mwaka  huu  unaweza  kuikosesha  mapato  ya    zaidi ya Shilingi 840 bilioni. Tumeona juhudi za Kamati ya Bunge ya    Nishati  na  Madini  katika  kutafuta  ufumbuzi  wa  Tatizo  la  Umeme    lakini juhudi hizi hazionekani upande wa Serikali na hasa Wizara ya    Nishati na Madini.        Mheshimiwa Spika, Imefikia wakati sasa kutangaza kuwa  Umeme    ni janga la Taifa na kwamba Bunge lipitishe Azimio la Uzalishaji wa    Umeme  kwa  viwango  vya  Mpango  wa  Maendeleo  na  kuweka    adhabu  ya  kumfukuza  kazi  Waziri  iwapo  miradi  hiyo  haitakuwa    imekamilika  kila  mwaka.  Kamati  ya  Bunge  na  Nishati  na  Madini    iwe  inatoa  Taarifa  mara  mbili  kwa  mwaka  (Bunge  la  Mwezi  wa    Novemba  na  Bunge  la  Mwezi  Februari)  kuhusu  maendeleo  ya    Miradi  ya  Umeme  na  kama  malengo  hayajafikiwa  Kamati  itoe    Azimio la kutokuwa na imani na Serikali.                                              

    Uwekezaji kwenye Gesi Asilia      
Mheshimiwa Spika, Inafahamika kuwa nchi yetu imejaaliwa kuwa    na Gesi asilia nyingi sana. Tafiti zinaonyesha kuwa hivi sasa kuna    zaidi ya 12tr cf ya Gesi na utafutaji bado unaendelea. Ndani ya    Miaka   michache   ijayo   nchi   yetu   itakuwa   moja   ya   mataifa    makubwa   yenye   Gesi   asilia   nyingi   sana.   Hata   hivyo   hali   hii    haionekani  katika  mipango  ya  Serikali  na  viongozi  wa  kisiasa  na    hata wataalamu hawaliandai Taifa kwa hali hii. Madhara yake ni    kuwa  itakapofika  siku  ya  siku  tutaingia  kwenye  migogoro  kama    tuliyoshuhudia          katika     sekta      ya    Madini.      Kambi       ya     Upinzani    inashangazwa   na   habari   kwamba   toka   Gesi   ya   Mkuranga    igunduliwe   mwaka   2007   mpaka   sasa   hakuna   mradi   wowote    umeanzishwa  kunyonya  gesi  hii  na  kuitumia  kuzalisha  utajiri  kwa    Taifa.  Tunapendekeza  kuwa  Mradi  wa  Ujenzi  wa  Bomba  la  Gesi    kutoka Mtwara ambalo pia litapita Mkuranga uwe ni kipaumbele    cha juu kabisa cha nchi. Mradi huu utekelezwe kwa nguvu kama    ilivyokuwa   kwa   Mradi   wa   Maji   wa   Ziwa   Victoria.   Bomba   hili    lijengwe  kwa  kushirikiana  na  Sekta  Binafsi  na    lifike  Tanga  na    Mwanza  ndani  ya  kipindi  cha  miaka  mitano  ijayo.  Ni  lazima    tuamua mambo makubwa na tuyafanye. Hili tunaweza kulifanya    na tulifanye.        Mheshimiwa Spika, katika suala hili la kuandaa Taifa kwa ajili ya    kuwa  Taifa  lenye  kuzalisha  Gesi  na  Bidhaa  zitokanazo  na  Gesi,   Kambi  ya  Upinzani  inashauri  kuwa  Tuanzishe  Chuo  Kikuu  Cha        Mtwara.       Chuo       hiki    kijikite   kuwaandaa           Watanzania          katika        utaalamu   wa   utafutaji,   uchimbaji   na   usimamizi   wa   sekta   ya        Mafuta na Gesi.      
Mheshimiwa  Spika,   moja  ya   njia   ya   kupunguza  matumizi  ya        umeme  majumbani  na  hivyo  kuhakikisha  umeme  wa  kutosha        unabakia kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji viwandani, Kambi ya        Upinzani  inapendekeza  kwamba  miradi  miwili  muhimu  ya  gesi        kwa  ajili  ya  matumizi  ya  majumbani  ianze  ndani  ya  mwaka  huu        wa fedha; nayo ni:         Mradi wa gesi ya LPG kwa ajili kujaza gesi kwenye mitungi na         Mradi wa kusambaza gesi majumbani katika jiji la Dar es salaam.        Miradi  yote  hii  itatekelezwa  na  shirika  la  maendeleo  ya  gesi  na        mafuta nchini TPDC. Hata hivyo Kambi ya Upinzani inakumbushia        pendekezo  la  kamati  ya  Bunge  ya  Mashirika  ya  Umma  kuhusu        kuifanyia  marekebisho  TPDC  kwa  kuigawa  na  kuunda  mamlaka        ya mafuta na gesi ambayo itahusika na kutoa vibali na leseni na        kusimamia   utafutaji   na   uchimbaji   mafuta   na   gesi   (upstream        regulator)  na  kampuni  itakayohusika  na  biashara  ya  mafuta  na        gesi.        Ukuzaji wa Uchumi Vijijini    Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri kuwa Uchumi wa Nchi yetu umekuwa   ukikua kwa kasi ya kuridhisha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.   Hata  hivyo  ukuaji  huu  wa  uchumi  haujaweza  kupunguza  umasikini  wa Watanzania kwa kiwango cha kuridhisha na cha kujivunia. Mara   mbili    viongozi     wetu     wakuu      wa       nchi    (Rais   na    Waziri    Mkuu)   wamehojiwa na vyombo vya habari na kukiri kuwa hawajui kwa nini   Watanzania  ni  masikini.  Kwa  wachumi  wengi  na  kwa  kasi  hii  ya   ukuaji  wa  uchumi  jibu  ni  hilo  hilo.  Kwamba  unakuwaje  na  Uchumi   unaokua kwa wastani wa asilmia 7 kwa miaka kumi bila kuounguza   Umasikini   ni   kitendawili   na   chemsha   Bongo.   Nina   imani   kubwa   kutokana        na     Tafiti   mbalimbali        kwamba         kwa      miaka      kumi   hatujawekeza vya kutosha katika uchumi wa vijijini na ndio maana   hatuoni  faida  za  uchumi  wetu  kukua.  Uwekezaji  mkubwa  na  hasa   uliofanywa  na  sekta  binafsi  umekuwa  ukifanywa  katika  uchumi wa   mijini.  Serikali  inapaswa  kufanya  uamuzi  wa  makusudi  kuwekeza   katika miundombinu ya uchumi wa vijijini.    Mheshimiwa  Spika,  Kambi  ya  Upinzani  kupitia  bajeti  hii  mbadala   imeleta  mapendekezo  ambayo  inaamini  kuwa  kwa  kiasi  kikubwa   kwa kipindi cha miaka mitano ijayo itasaidia kujibu kitendawili hiki na   itaondoa  matatizo  makubwa  yanayotukabili  ya  umasikini  uliokithiri   vijijini na kusababisha vijana wengi kukimbilia mijini.    Mheshimiwa Spika, Katika mkakati wetu wa kufanikisha mpango wa   kuondoa        umasikini     ni   kuzifanya      Halmashauri        zetu     za   Wilaya   kutayarisha kitu kinachoitwa “District Economic Development Master   Plan” yaani Mpango Mama wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Wilaya   ambapo  kila  halmashauri  kupitia  mpango  wake  kutengeneza  ajira   zisizopungua 2000 kwa mwaka.     Mheshimiwa Spika, Mpango huu utasaidia kuondoa dhana ambayo   imeenea kwa watendaji ngazi za mikoa na wilaya kukaa mkao wa   kupokea  fedha  na  kutumia  tu  toka  Serikali  kuu.  Mikoa  na  wilaya   zitatumia  fursa  zilizopo  katika  maeneo  yao  ili  kuondoa  matatizo   yanayowakabili           wananchi        wao       kuliko     kusubiri     kupelekewa   wawekezaji        toka     kituo    cha     uwekezaji,      ambapo         Halmashauri   zingeweza kuingia ubia na mwekezaji husika.                                            
    Mheshimiwa  Spika,  Kambi  ya  Upinzani  katika  kufanikisha  mpango   huo  tumeleta  vipaumbele  sita  (6)  na  kila  kipaumbele  kitasaidia   kuinua uchumi wa wananchi waishio vijijini.    Mheshimiwa  Spika,  Kwa  kuwa  baadhi  ya  vipaumbele  ambavyo    tumevipanga na Serikali imeleta hivyo hivyo, tofauti iliyopo ni jinsi ya    kuvitekeleza     ili  viweze   kuleta   tofauti   kwa   uchumi  wa   nchi   hii.    Mheshimiwa  Spika,  Kipaumbele  chetu  cha  muhimu  ni  Kuwezesha    Ukuaji  wa  Sekta  za  Uzalishaji  na  hasa ukuaji  wa  uchumi  wa  vijijini    (rural   growth).  Kambi   ya   Upinzani   inakichukulia  kipaumbele   hiki    kama tiba halisi ya kuwaondolea umasikini Watanzania waishio vijijini    kwa  kuwa  asilimia  kubwa  ya  Watanzania  wanaoishi  vijijini  maisha    yao yanaendeshwa na shughuli zinazohusiana na kilimo.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  kutimiza  azma  ya  kuinua  maisha  yao,    miundombinu   ya   barabara   na   umeme   itasababisha   ujenzi   wa    viwanda        vidogo       vidogo       vya     kuongeza        thamani        za    bidhaa    zizalishwazo vijijini, ni dhahiri pia asasi za fedha zitaenda zenyewe na    pia  itasaidia  kupunguza  uhamiaji  wa  kutoka  vijijini  kwenda  mijini    (“rural urban migration”) kwa vijana wetu.    Mheshimiwa          Spika,     Kambi       ya    Upinzani      inaamini      kwa      njia   hii   tutafanikiwa kuondoa umasikini uliokithiri na pia kuiondoa nchi yetu   kwenye hatari ya kuwa taifa la wachuuzi. Pendekezo kubwa katika   kuchochea ukuaji wa uchumi wa Vijijini ni la kupeleka vijijini shilingi   450 bilioni kila mwaka kwa miaka mitano mfululizo  katika  sekta  za   Barabara        za   vijijini,  Umeme   vijijini       na    Maji     vijijini.  Fedha      hizi   zitagawiwa kwa Halmashauri za Wilaya (sio miji, manispaa na majiji)   kulingana  mahitaji  ya  sekta  husika  kwa  Wilaya  husika  ya  Vijijini.                                              
    Tunaweza  kufikiria  kuanzisha  Mamlaka  ya  Maendeleo  Vijijini  (Rural   Development            Authority)       ambayo          itasimamia         Mpango          huu   utakaotekelezwa  na  Halmashauri  za  Wilaya  chini  ya  Ofisi  ya  Waziri   Mkuu.        Bandari    Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Tanzania inatumia vizuri fursa   ya  jiografia  yake  ya  kuwa  na  ukanda  mrefu  wa  bahari  Kambi  ya   Upinzani  itahakikisha  upanuzi  wa Bandari  ya  Dar  es  Salaam  na   Tanga  kwa  kutumia  Ushirikiano  wa  Sekta  Binafsi  na  ya  Umma  –   Private Public Partnership (PPP) unakamilika haraka ikiwa ni pamoja   na      kuimarisha   bandari   ya   Mtwara.   Kwa   njia   hii   tutawavutia   wafanyabiashara wa nchi ambazo hazina bandari kupitisha mizigo   yao katika bandari yetu.    Reli    Mheshimiwa  Spika,  Reli  ya  Kati  ni  kichocheo  kikubwa  sana  cha   uchumi  kwa wananchi wanaoishi mikoa iliyopo kando kando ya reli   hiyo, pia kuwa kiunganishi kikubwa kati ya bandari na nchi ambazo   hazina  bandari,  hivyo  basi  jambo  la  kwanza  ni    kuiboresha    reli  ya   sasa  ili  ifanye  kazi  kwa  uwezo  mkubwa  kusafirisha  abiria  na  mizigo   mpaka  hapo  fedha  za  kujenga  Reli  mpya  yenye  mataruma  ya   kisasa itakapopatikana. Ili kutimiza adhima hiyo tumetenga kiasi cha   Tsh.100bn  kuliwezesha shirika la Reli Tanzania kufanya kazi yake ya   msingi  ya  kusafirisha  Mizigo  na  Abiria  .  Hata  hivyo  uendelezaji  wa   Mradi   wa   Mchuchuma   na   Liganga   unataka   kuwepo   kwa   Reli   itakayounganisha Wilaya ya Ludewa na Bandari ya Mtwara. Kambi   ya Upinzani inapendekeza kuwa Upembuzi yakinifu wa Reli hii kama   ulivyoainishwa   katika   Mpango   wa   Maendeleo   wa   Taifa   uanze   kufanyika  mwaka  huu  na  mchakato  wa  Ujenzi  wa  Reli  hii  uanze sambasamba   na   kuanza   kwa   mradi   wa   kuchimba   Chuma   na   Makaa ya Mawe.    Mheshimiwa  Spika,  katika  kuimarisha  usafiri  wa  anga  ambao  ni    kiunganishi  kikubwa  kati  ya  watanzania  na  wale  wa-ughaibuni  na    kichocheo   kikubwa   cha   utalii.   Hivyo   basi,   Kambi   ya   Upinzani    itahakikisha  Shirika  letu  la  Ndege  linarudi  tena  kwenye  biashara.    Tumeweka Tshs. 200bn. Kulifufua upya shirika la ndege la ATC. Hata    hivyo,      tunashauri       kwamba          Serikali     iangalie      uwezekano           wa    kurekebisha umiliki wa Shirika la Ndege la Taifa kwa kuhusisha Taasisi    za  Umma  ambazo  zinafaidika  na  kuwepo  kwa  Shirika  mara  moja.    Kwa mfano, Shirika la Ndege linatarajiwa kukuza utalii wa nchi hivyo    Mashirika kama TANAPA na NCAA yanaweza kuelekezwa kuwekeza    mtaji katika Shirika la ATCL na kumiliki asilimia zisizozidi 30 za Shirika.    Badala ya Mashirika haya kupeleka tozo ya asilimia 10 ya mapato    yao Hazina, fedha hizi zaweza wekwa ATCL kwa kipindi cha miaka    kadhaa na hivyo kulirejesha Shirika katika Biashara. Tunashauri wazo    hili liangaliwe kiufundi kama linaweza kuleta tija.        Usimamizi wa mashirika ya umma    Mheshimiwa  Spika,  Kambi  ya  Upinzani  Bungeni  inakubaliana  na    Serikali katika hatua za kuiimarisha Ofisi ya Msajili wa Hazina ili iweze    kusimamia   vema   Mashirika   ya   Umma.   Ni   wazi   kwamba   kuna    Mashirika  ya  Umma  ambayo  iwapo  yakisimamiwa  Vizuri  yataweza    kufanya kazi kwa faida na hivyo kuondoa mzigo wa ruzuku za Serikali    kwenda   kwa   Mashirika   ya   Umma.   Vile   vile   Kambi   ya   Upinzani      Bungeni  inapongeza  pendekezo  la  Kuanzisha  Mfuko  wa  Uwekezaji    wa Taifa kwa ajili ya kutoa Mitaji kwa Mashirika ya Umma. Hatua hii    itasaidia sana.    
 Mheshimiwa          Spika,     Kambi       ya    Upinzani       Bungeni       inapendekeza    kufanya Marekebisho ya Sheria zifuatazo katika Finance Bill kwa ajili    ya kuboresha ufanisi wa Mashirika ya Umma. Sheria ya Mashirika ya    Umma ya mwaka 1992 ili kuiboresha na kutamka wazi wazi mamlaka    ya  Ofisi  ya  Msajili  wa  Hazina  katika  kusimamia  Mashirika  ya  Umma    ambayo  Serikali  ina  hisa  zaidi  ya  Asilimia  Hamsini  ikiwemo  kutoa    Mamlaka  kwa  Msajili  wa  Hazina  kusimamia  Waraka  anazotoa  kwa    Mashirika  na  pia  kutungwa  kanuni  zitakazopelkea  kuwepo  kwa    Mfumo   wa   Maadili   ya   Utawala   Bora   (CODE   OF   CORPORATE    GOVERNANCE FOR PUBLIC CORPORATIONS).        Mheshimiwa           Spika,      tunashauri        Sheria      iliyounda       Consolidated    Holdings  ifanyiwe  Marekebisho  kupitia  Sheria  ya  Fedha  ya  mwaka    2011 ili kulipa Uhai wa moja kwa moja Shirika hili na vile vile kupewa    Majukumu  ya  Kusimamia  Mashirika  ya  Umma  ambayo  Serikali  ina    hisa chini ya asilimia 50. Lengo la pendekezo hili ni kuhakikisha kuwa    Hisa  za  Serikali  katika  Makampuni  binafsi  zinasimiwa  ipasavyo  na    kwamba CHC iwe kweli ni Holding Company ya Serikali kwa hisa hizi.    Kwa  sasa  hisa  hizi  zinasimamiwa  na  Msajili  wa  Hazina.  Pendekezo    letu   ni   kutenganisha   majukumu   haya   ili   kuleta   ufanisi   na   hasa    ukizingatia kuwa CHC bado itakuwa inamilikiwa na Msajili wa Hazina  kwa asilimia 100. Uamuzi huu ukitekelezwa utarahisisha sana Kamati    ya Bunge ya Mashirika ya Umma kuwa na jicho la kiusimamizi kwa    kwa  mitaji  ya  Serikali  kwenye  Kampuni  binafsi  kwani  CHC  hutokea    mbele ya Kamati ya POAC baada ya kukaguliwa na CAG.        Pensheni kwa wazee    Mheshimiwa  Spika,  Tanzania  ina  mfumo  mzuri  wa  pensheni  kwa    wastaafu  ambao  unasimamiwa  na  Mifuko  Kadhaa  ya  Pensheni    hapa nchini. Hata hivyo kuna changamoto kubwa kwamba Serikali    inadaiwa   fedha   nyingi   na   mifuko   hii   hali   ambayo   tunadhani    inahatarisha maisha ya wastaafu. Kwa mfano, Serikali inadaiwa na    Shirika la PSPF na iliahidi kuanza kulipa Deni la Shilingi 700 bilioni lakini    bado  haijalipa.  Vile  vile  Serikali  bado  haijasaini  mkataba  wake  na    Shirika la NSSF kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Tunashauri    Serikali    itemize     wajibu      wake      huu    ili  kuifanya      mifuko      iendelee    kutumikia       Taifa     na    kuwekeza         kwenye        miradi      mikubwa        kwa    maendeleo ya nchi.  
 Mheshimiwa Spika, Tunashauri pia kuwa Serikali iangalie uwezekano    wa      kufanya       marekebisho           katika      Mfumo        wa     Pensheni        na    kuunganisha  mifuko  iliyopo  na  kubakia  na  mifuko  miwili  tu,  mmoja    kwa ajili ya Sekta ya Umma na Mwingine kwa ajili ya Sekta Binafsi na    sekta   isiyo   rasmi.   Hivi   sasa   nchini   kuna   jumla   ya   wanachama    1,073,444 kwenye mifuko ya Pensheni (NSSF – 506,218. PSPF – 298,046.    PPF  –  160,068.  LAPF  –  73,833  na  GEPF  35,279)  ambayo  ni  sawa  na    asilimia  2.4  tu  ya  Watanzania  wote.
Hiki  ni  kiwango  kidogo  sana  kuhudumiwa   na   mifuko   mitano   ya   Hifadhi   ya   Jamii.   Vile   vile    tunapendekeza kiwango cha chini cha Pensheni kifikie Shilingi 50,000    na kwa maana hiyo Shirika la PSPF lipandishe Pensheni kutoka 20,000    za sasa. Tunawapongeza NSSF kwa kulipa 80,000 na PPF kwa kulipa    50,000.      
Mheshimiwa  Spika,  Licha  ya  Udhaifu  huu  wa  Pesheni  kwa  Wazee    wetu  waliotumikia  utumishi  wa  Umma  kuwa  kidogo  pia  Tanzania    haina  mfumo  wa  Pensheni  kwa  Wazee  bila  kujali  kama walikuwa    waajiriwa kwenye Serikali au Mashirika ya Umma. Wazee wakulima    ambao wamechangia kwa kiwango kikubwa katika uchumi kupitia    kilimo hawamo kwenye mfumo wa Pensheni na hivyo kusababisha    kero kubwa kwa wazee wengi ambao ndio wanalea wajukuu huko    vijijini  kufuatia  vijana  wao  wengi  kupoteza  maisha  kwa  magonjwa    kama Ukimwi.        Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kuanzishwa kwa Pensheni    kwa  Wazee  wote  nchini  walio  na  umri  wa  zaidi  ya  miaka  65  na    ambao hawamo katika mfumo wa Pensheni. Kuna Jumla ya Wazee    1,362,435 ambao ni sawa na asilimi 3.2 ya Watanzania wote. Wengi    wa  Wazee  hawa  wapo  vijijini  na  ndio  walezi  wa  wajukuu  zao    kufuatia  janga  la  Ukimwi.  Itatakiwa  kutenga  Shilingi  280  bilioni  kila    mwaka  kwa  ajili  hii.  Ni  fedha  nyingi  lakini  muhimu  kulinda  Wazee    wetu  ambao  wamelitumikia  Taifa  letu  ama  kwa  kulima,  kufuga,    kuvua  au  hata  kwa  kutulea  tu.  Maelezo  ya  ziada  kuhusiana  na   mfumo  huu  wa  Pensheni  atayatoa  Waziri  Kivuli  wa  Kazi  na  Ajira    atakapokuwa  anawasilisha  maoni  ya  Kambi  ya  Upinzani  kuhusu    Wizara husika.      
HITIMISHO
 Mheshimiwa  Spika,  Baada  ya  Maelezo  hayo  sasa  napendekeza   Sura ya Bajeti ya Nchi iwe kama inavyoonekana katika Jedwali hili   hapa  chini.  Naomba  Bunge  lako  tukufu  lijadili  Hoja  ya  Waziri  wa   Fedha  kuhusu  Makadirio  ya  Mapato  na  Matumizi  ya  Serikali  kwa   kuzingatia maoni haya ya Kambi ya Upinzani Bungeni.  
SURA YA BAJETI MBADALA KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012    MAPATO                                       Tshs. Bilioni    Mapato ya Ndani                          
 8,681.   Mapato ya Halmashauri                        
 351.   Mikopo na Misaada ya nje                  
3,924.   Mikopo ya Ndani                            
1,204.        JUMLA YA MAPATO                              14,160        

MATUMIZI                                    Tshs.Bilioni    Matumizi ya Kawaida                    
  7,913    Matumizi ya Maendeleo                            
 i.  Fedha za Ndani:- 3,193                    
ii. Fedha za nje:-     3,054        
 6,247                JUMLA MATUMIZI                  14,160                                                  
        Mheshimiwa Spika,    Mmoja wa viongozi katika Duniani ninaowaheshimu sana ni pamoja    na Tun Dr Mahathir Mohamad, Waziri Mkuu Mkuu wa zamani wa nchi    ya  Malaysia  na  rafiki  mkubwa  wa  Mwalimu  Nyerere.  Ninapenda    kumaliza Hotuba yangu kwa kunukuu maneno yaliyopo ukurasa wa    nyuma  wa  Kitabu  chake  ‘A  doctor  in  the  house’.  Nanukuu  ‘……    Viongozi wachache wameweza kubadili uchumi wa nchi zao kutoka    uchumi   unaotegemea   kilimo   tu   mpaka   kuwa   na   uchumi   wa    viwanda  -  wachache  zaidi  wameweza  kufanya  hivi  katika  kipindi    cha miongo miwili tu.’    Dr   Mahathir   aliposhika   madaraka   ya   nchi   yake   mwaka   1981,    Malaysia ilikuwa ni nchi ambayo zaidi ya nusu ya Raia wake (asilimia    56) wakiishi katika dimbwi la umasikini. Alipoachia madaraka mwaka    2003 Malaysia ikawa na asilimia 3 tu ya Raia wake wanaoishi katika    dimbwi la umasikini.        Mheshimiwa Spika,    Malaysia  iliweza  kwa  sababu  Viongozi  waliweza  kuwa  na  mwono    wa   mbali,   kufanya   maamuzi   na   kuyasimamia   maamuzi   hayo.    Ninaamini  kuwa  Tanzania  inaweza  kufanya  vizuri  zaidi  ya  Malaysia    kama  sisi  sote  kama  viongozi  tukiamua  kuweka  maslahi  ya  nchi    mbele,        kuweka        malengo         makubwa,           kufanya        maamuzi         na    kutekeleza maamuzi hayo.                                                    
    Kila mtu akitimiza wajibu wake, Tunaweza.     Tukiacha kuwa Taifa la walalamikaji, Tunaweza.     Tukiendeleza Umoja wa Kitaifa, mshikamano na kulinda Haki za raia,    Tunaweza.    Ninaamini, Tunaweza!      
Mheshimiwa Spika,    Naomba kuwasilisha                                                
 Kabwe Zuberi Zitto, Mb                                
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi                                                            

No comments:

Post a Comment