Thursday, 9 June 2011

Benki ya Dunia yaipa Tanzania mabilioni

 
Benki ya Dunia (WB)
Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia (WB) jana ilihidhinisha mkopo mwingine wa Dola milioni 27.88 kwa Tanzania kusaidia sekta ya usambazaji na upatikanaji wa umeme kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).
Hayo yalisemwa jana na Mwakilishi wa WB nchini Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa wameamua kuongeza mkopo huo baada ya kuona bado kuna tatizo la upatikanaji na usambazaji wa umeme nchini.
“Pamoja na maendeleo makubwa ya kuwepo kwa umeme na usambazaji, bado kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme Tanzania,” Alisema Murray.
“Tunaamini kwamba pesa hizi za ziada kutoka katika Benki ya Dunia zitasaidiakuboresha usambazaji na upatikanaji wa umeme nchini,” alioongeza.

No comments:

Post a Comment