Ujerumani kuvimaliza vinu vya nuklia
Kufuatia mazungumzo ya usiku kutwa ya serikali ya mseto nchini Ujerumani, nchi hiyo imetangaza kubadilisha sera kuhusiana na nguvu za nuklia.
Mtu aliyebeba bango ambalo linauliza; 'Nguvu za nuklia? - La, hasha!'
Uamuzi huo unaifanya Ujerumani kuwa taifa la kwanza kubwa ambalo limeendelea sana kiviwanda kutangaza kutupilia mbali utumizi wa nguvu za nuklia.
Mataifa kadhaa yamekuwa yakizichunguza sera zake kuhusiana na nguvu za nuklia, hasa kufuatia janga la Fukushima nchini Japan, mwezi Machi.
Nchi ya Uswisi wiki iliyopita ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kutangaza kwamba itasimamisha utumizi wa nguvu za nuklia.
No comments:
Post a Comment