MAKAMANDA WA MAREAKANI WAOMBA RADHI KWA MAUAJI YA RAIA.

Makamanda wa Marekani katika majeshi ya NATO nchini Afghanistan wameomba radhi kwa mauaji ya raia tisa, wakati walipofanya mashambulizi ya anga Jumamosi iliopita.
Wanajeshi wa Marekani wameomba msaada wa ndege za kivita baada ya kambi yao katika wilaya ya Nawrad, kusini mwa jimbo la Helmand, kushambuliwa na waasi waliomuua mwanajeshi mmoja aliyekuwa akifanya doria.
Maafisa wa Kiafghanistan katika eneo hilo wamesema ndege za kivita zilizipiga mabomu nyumba mbili na kuwauwa watoto 12 na wanawake wawili.
Kamanda wa NATO kusini mwa Afghanistan Meja Jenerali John Toolan, amesema kipa umbele cha majeshi ya muungano ni kuepusha athari miongoni mwa raia.
Uchunguzi kamili umeanza huku rais Hamid Karzai wa Afghanistan akilaani vikali mauaji hayo ya raia.
Posted by Ebou's
No comments:
Post a Comment