Thursday, 14 April 2011


Vijana wanahatarisha amani


SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) limesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linatishia usalama wa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa visiwani hapa.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Khamis Mwinyi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho hilo zilizopo Kikwajuni Mjini Unguja, alisema vijana wengi hawana ajira hali inayotia wasiwasi kwa taifa.
Aliwaambia waandishi wa habari kwamba tatizo kubwa linalowakabili kwa sasa ni kukosa kazi za kufanya hivyo serikali ia wajibu mkubwa wa kuwapatia kazi ili kuweza kukabiliana na ukali wa maisha lakini hali hiyo imekuwa ikiendelea jambo ambalo linatishia amani.
Katibu mkuu huyo akitaja changamoto zinazoikabili shirikisho hilo ni ni pamoja na masuala ya kazi kupelekwa katika wizara zizizohusika na masuala ya ajira, wasiwasi wa wafanyakazi kuhusu kuendelea kupanuka kwa pengo baina ya watumishi wa kawaida na wale wa ngazi za juu.
Changamoto nyengine ni ugumu wa maisha ya wafanyakazi na wananchi wa kawaida kutokana na wahusika wameshindwa kudhibiti mfumko wa bei ambao kila uchao unaongezeka huku fedha nyingi za serikali zikitumika kuwalipa posho makatibu wakuu, mawaziri, wakurugenzi na maafisa ambao ni wengi sana kulingana na udogo wa Zanzibar.
Alidha mazingira ya kazi kiafya na usalama katika sehemu za kazi pia ni kikwazo chengine ambacho kinahitaji kupatiwa ufumbuzi, wasiwasi kuhusu ukubwa wa serikali kukidhi uwezo wa serikali kimapato.
Akielezea mafanikio katika shirikisho hilo ni Kuendeleza hali ya amani na utulivu hapa nchini kilicgowafanya wafanyakazi kuendelea na kazi zao bila wasiwasi.
Kautoa fursa kwa vyama vya wafanyakazi kutekeleaza shughuli zao bila kuingiliwa au kubuguziwa na mtu au chombo chochote humu nchini.
Kuundwa kwa Wizara ya kazi ambayo kwa majukumu yake yote yanahuusiana na mambo ya ajira, Kuundwa kwa Wizara inayohusiana na utumishi wa umma, Kuunda sheria ya utumishi wa umma na kuwapatia wafanyakazi mishahara yao kwa wakati.
Mengine ni kuyatambua na kuyaeleza kwa ufasaha matatizo ya wafanyakazi na kuahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo na kuahidi kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika kutatua kero zao na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumzia mafanikio ya awamu ya sita ambayo yalipaswa kuendelezwa ni pamoja na kuepukana na madeni ya wafanyakazi wastaafu wa serikali ya Mapinduzi katika mfuko wa hifadhi ya jamii, kutekeleaza sheria za kazi za 2005 kama zilivyopitishwa na kutekeleza sera ya ajira ya Zanzibar .
Mengine ni kutekeleza mpango wa kuondoa ajira za watoto Zanzibar , kutekeleza sehemu ya Service za mawizara ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar .
Akitaja mapungufu naibu katibu mkuu huyo alisema kuendeleza kuwepo kwa mifumo isiyozingatia sheria za kazi na taratibu za ongezaeko la mishahara yaani,kutokuwepo kwa utaratibu wa increaments na kutokuwepo kwa utaratibu wa kupandisha ngazi watumishi pamoja na ongezeko la kutatanisha la mishahara.
Alisema kutokutekelezwa masuala ya kisheria juu ya masuala ya kisheria juu ya masuala ya maslahi ya wafanyakazi,uundwaji wa kanuni za sheria za kazi, uundwaji wkwa masuala ya kisheria juu ya masuala ya maslahi ya wafanyikazi na uundwaji wa kanuni za sheria za kazi pamoja na uundwaji wa vitengo vya masuala ya kazi chini ya kamisheni ya kazi.

No comments:

Post a Comment