Jussa Awapa Moyo Vijana Zanzibar
Na Salma Said Zbar
MWAKILISHI wa Mji Mkongwe Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amewataka vijana wanaoacha madawa ya kulevya visiwani hapa kuendelea na ujasiri waliouonesha ili vijana wenzao waweze kuiga mfano wao.
Jussa alisema hayo muda mfupi baada ya kuwakabidhi vijana hao shilingi millioni 1.2 wakati alipowatembelea katika vituo vya nyumba za vijana hao ‘Sober House’ ambapo jumla ya vijana 300 wameonesha nia yak taka kuachana na madawa ya kulevya haa Zanzibar.
Fedha hizo ni zilizotolewa na Mbunge wa kuteuliwa Thuwaiba Idrissa na mwenyewe Jussa ambapo kila mmoja ametoa laki sita kwa ajili ya kuwasaidia harakati za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kwa vijana wa Zanzibar ambapo wametakiwa kuzitumia kwa kulipia kodi ya nyumba wanazoishi.
Alisema kitendo kilichooneshwa na vijana hao ni kikubwa na kinahitaji kuungwa mkono na jamii nzima kwani vijana hao wameonesha ujasiri mkubwa wa kujitambua na kukubali kwamba wamefanya kosa na wakaamua kuondokana na balaa hilo la madawa ya kulevya.
“Kwanza nakupongezeni hii n jihadi ya nafsi hakuna jambo kubwa kama kujitambua na hakuna kitu muhimu kama mtu kwanza kujua tatizo letu …ukishajua tatizo ndipo hapo utakapoweza kulitatua na huu ni ujasiri kubwa sana mliouonesha kwani sio kila mtu anaweza kuwa na ujasiri kama huu” alisema Jussa katika kuwapa moyo vijana hao ambao wanaishi pamoja katika nyumba maalumu.
Jussa ambaye kwa mara ya kwanza amepata uwakilishi katika jimbo la Mji Mkongwe amesema huwezi kulizungumzia jimbo lake na ukaliwacha suala la madawa ya kulevya kwani kiini cha watumiaji wa madawa ya kulevya kipo katika jimbo lake hivyo ameahidi kupambana nalo kwa njia za kitaalamu ili lengo la kupunguza vitendo vya utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya lipunguwe au kwisha kabisa katika jimbo hilo.
Alisema watumiaji wa madawa ya kulevya wamekuwa kero kwa wao wenyewe familia na hata taifa kwa ujumla ambapo kila mmoja amekuwa akilichukuliwa suala hilo kwa mtazamo tofauti kulingana na madhara aliyoyapata kutoka ndani ya familia yake.
“Sote tunajua kuwa suala la watumiaji wa madawa ya kulevya ni kubwa na linatuathiri sote maana hata kama wewe hutumii lakini akikujia mla unga unaona amekuudhi ..hvyo hivyo kwa mtu binafsi, familia na hata taifa kwa ujumla kwa hivyo hili suala linatuathri sote … kama mnakumbuka kwamba familia huwa haina raha iwapo kuna mtoto wao mmoja tu ndnai ya nyumba anatumia unga” alisema Jussa.
Jussa ambaye amejikubalisha kuwa balozi wa madawa ya kulevya, alisema chama chochote kilichokuwa makini hakiwezi kutaja sera zake kwa Zanzibar na kikawacha kuzungumzia suala la athari na ukubwa wa madawa ya kulevya hapa Zanzibar kwani suala hilo limekuwa kubwa na linahitaji kupata msaada wa serikali ili kuweza kukabiliana nao.
“Suala la mumiaji wa madawa ya kulevya ni suala la mtu mwenyewe kukubali kuachana nalo sio suala la familia wala sio suala la serikali …na hili mnaona wenyewe wakati mwengine familia huingilia kati kumchukua kijana na kumpeleka hospitali kumtibu lakini matokeo yake akitoa tu hospitali anakaa siku mbili tatu na anarejea tena pale pale ..sababu nini ….sababu ni kuwa yeye mwenyewe hajaamua kuacha” alisema Jussa.
Aidha aliwataka wale wote walioonesha nia hiyo ya kutaka kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya kuendelea kuwashawishi wengine bila ya woga ili waweze kuachana na suala hilo kwani vjana wengi wameathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya jambo ambalo linawasababishia madhara makubwa ikiwemo magonjwa na ukimwi na hatimae vifo.
Licha ya kuwepo unyanyapaa kwa watu wenye kutumia madawa ya kulevya Zanzibar , lakini Jussa amewataka vijana hao kutokubali kurudi nyuma kwani hatua waliofikia ni kubwa na haipaswi kuishia njiani.
“Ni kweli huko nje kuna stigma lakini hii ni hatua kubwa mliofikia na kuweza kujitambua na kukubali kwamba sasa mnataka kupambana na tatizo hili …sasa naona hapa ndipo panapohitaji mashirikiano makubwa ili na wengine wapate moyo wa kuja kujiunga na nyumba hizi na hatimae dhana ya Zanzibar bila ya madawa inawezakana ifanye kazi” alisema Jussa ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa CUF.
Meneja wa nyumba hizo ‘Sober Houses’ Ahmed Issa ametoa wito wazee wa vijana hao na serikali kwa ujumla kuwaunga mkono ili kukabiliana na changamamoto zinazowakabili kwani kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha tatizo la madawa ya kulevya Zanzibar.
Ahmed ambaye amekuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa miaka 32 amesema ameamua kuachana na utmiaji huo kutokana na kuwa alikuwa anadharaulika katika jamii na familia yake kutokana matumizi hayo jambo ambalo lilimsononesha na kuaza kuamua kuacha licha ya kuwa kuna changamoto nyingi ambazo amekabiliana nazo katika suala hilo .
Amesema hadi sasa wana vijana 55 na nyumba nne ambapo Pemba ipo moja na Unguja tatu ambapo wamekuwa wakipanga ratiba za masomo na kujadiliana na kubadilishana mawazo kama ni njia moja ya vijana hao kuelezea namna ambavyo wanajihisi wanapoamua kuachana na madawa hayo.
Sober Houses ambazo zipo maeneo mbali mbali hapa Zanzibar lengo lake ni kuwaepusha watumiaji wa madawa ya kulevya kuachana na utumiaji huo ambapo hadi sasa bado hawajapata wafadhili jambo ambalo limekuwa likiwasumbua na kusababisha vijana wengi wanaotaka kujiunga na nyumba hizo kushindwa kuchukuliwa kutokana na kukosekana nafasi ndani ya nyumba hizo.
Hadi sasa asilimia 70 ya vijana wanaoishi katika nyumba hizo wameacha moja kwa moja ambapo kila mtu anayetaka kujiunga hulazimika kulipa laki moja kwa ajili ya malazi na chakula na hulazimika kuishi humo kwa miezi minne bila ya kutoka na baada ya hapo huruhusiwa kutoka lakini kwa masharti maalumu ya kufuatana na waangalizi hadi hapo mazingira ya kutotumia madawa ya kulevya utakapoyazowea

No comments:
Post a Comment