Monday, 28 February 2011

Dk. Shein awaapisha wateule wake

Na Salma Said





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wapya wa serikali muda mfupi baada ya kuwaapisha leo Ikulu Mjini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amewaapisha baadhi ya watendaji wapya serikali, ikiwa ni katika hatua za kupanga safu yake ya uongozi.
Walioapishwa ni pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Said Hassan Said, Katibu wa Rais wa Zanzibar, Haroub Shaibu Mussa, Naibu Katibu wa Rais wa Zanzibar, Mariam Haji Mrisho, na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar, Chande Omar Omar.
Hafla ya kuwaapisha watendaji hao ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wakiwamo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahamod, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mwinyihaji Makame.
Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu, Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej.
Walikuwapo pia Waziri wa Afya, Juma Duni Haji, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassour Ahmed Mazrui, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi, Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Khatib Abdulrahman Khatib na viongozi wengine kadhaa.

No comments:

Post a Comment