Tangazo la ZAWA UK

Assalamu alaykum,
Wazanzibari waishio UK,
Zanzibar Welfare Association UK [ZAWA], inapenda kuwajuulisha wanachama pamoja na Wazanzibari wote wanaoishi UK ya kuwa itakuwa inafungua Ofisi yake ilioko 1 Toronto Avenue, Froud Center Manor Park, kila Jumapili ya mwisho wa mwezi kuanzia mwezi huu wa January 2011 kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 11 jioni (1.00 – 5.00 pm) , ili kusikiliza matatizo walionayo katika masuala mbali mbali ya kijamii likiwamo la ukaazi wapo pia hapa UK.
Kw maelezo mafupi ni kuwa Zawa itakuwa ikitoa msaada wa mawazo kwa mwanachama na pia wa maandishi kwenye taasisi husika pale ambapo panapohitajika. Hivyo basi tunawataka kila Mzanzibari ambae anahisi amahitaji kupata huduma hizi kuwasiliana nasi kwa njia ya email ama kwa njia ya simu ili kuweka “appointment yake”.
Kwa kuwa huduma hizi ndio zinaanza Zawa ingependa kuwajuulisha Wazanzibari wote kuwa itakuwa ikitoa huduma ya kiasi ya watu 5 tu kila “session”. hivyo tutatumia ule msemo wa anaekuja mwanzo ndie atakae pata huduma mwanzo.
email: ukzawa@gmail.com
Mob:: 07588 550153
07535 656346
07946 626490
07508 016265
Ahsanteni
No comments:
Post a Comment