Monday, 31 January 2011

Taasisi za Fedha Zatakiwa Kuwa na Mahusiano Mema

Na Salma Said Zanzibar
MZANZIBARI aliyeshinda tuzo ya Miss Africa Australia Zaituni
Hunt.ameahidi kufanya kazi na taasisi mbali mbali zenye kufanya kazi
ya kijamii hapa Zanzibar ilikukuza vipaji na fusa kwa vijana na
wanawake.
Hunt (20) aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habri
katika mkutano hapo jana na kuongeza kuwa anaelewa mchango mkubwa
unaotarajiwa kutoka kwa Wazanzibari wanaoishi nje.
Tuzo ya Miss Africa Australia ilifanyika kwa mara ya kwanza mwezi
uliopita na kushirikisha walibwende 450 kati ya raia wa Australia
wenye asili ya Afrika na Hunt aliiwakilisha Tanzania na kupepea
bendera yake. Australia kuna Waafrika zaidi ya 200,000 ambao
wameshakuwa raia wa nchi hiyo.
Hunt, mwenye Shahada ya Kwanza ya ubunifu na teknolojia na diploma ya
biashara na hesabu ameeleza nia yake kusaidia kuiunganisha Zanzibar na
Australia katika nyanja kadhaa wa kadhaa.
Alisema anajua Australia kwa kuwa ni nchi iliyoendela ina mambo kadhaa
wa kadhaa inayoweza kuwa ushikiano kama vile kwenye sekta za utalii,
elimu, afya na hata mambo ya uwezeshaji vijana na wanawake.
“Naamini Zanzibar inaweza kufaidika sana kutoka Australia na la
umuhimu ni kuwepo taratibu za kuratibu shughuli hizo jambo ambalo
nataka nichukue dhamana ya kulifanya,” alisema Zaituni katika
mazungumzo hayo na waandishi wa habari.
Alieleza nia yake ya kusaidi wanawake wa Zanzibar kwa kutoa mafunzo ya
ubunifu na kufungua kiwanda cha uzalishaji wa nguo ambazo zitazalishwa
hapa Zanzibar na kuuzwa nchini lakini pia Australia na nchi nyengine.
“ Nakusudia kuanzisha lebo ambayo nitaiita Zaituni wa Zanzibar
(Zaituni of Zanzibar) ambayo nitaanza na nguo na kufuatia vitu vyengine
vya ulimbwende kwa kutumia rasilimali za ndani. Nataka kuanza kazi na
wasichana mbali mbali wa Zanzibar.” Alisema mlimbwende huyo.
Nae Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Zanzibar (ZATO)
Omar Said Shaaban amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Zanzibar
kutumia vyema Wazanzibari waliotawanyika sehemu mbali mbali duniani.
“Tuna Wazanzibari katika fani kadhaa wa kadhaa na wengine ni watu
maarufu sana nchini mwao na sioni sababu kwa nini tusiwatumie
kuitangaza Zanzibar,” alisema Shaaban.
Pia Shaaban alitoa wito kwa Serikali ya Zanzibar kuondosha marufuku
yake kwa mashindano ya urembo ambayo kirasmi mara ya mwisho
yalifanyika mwaka 1969 ambapo Hedia Khamis Mussa ndie aliyevishwa taji
la Mrembo wa Zanzibar.
“Hii ni ajira kama ajira nyengine na ni ajira inayoweza kuwapatia
wengine pia ajira na si vyema kuifunga milango ya fursa kama hizo”
alisema Shaaban.
Hunt anatazamiwa kuwepo nchini kwa mwezi mmoja na juzi alikutana na
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad

No comments:

Post a Comment