Yampora gari na kumpiga risasi
Na Mwandishi Wetu, Kinondoni
KUNDI la majambazi wakiwa na silaha wamemvamia dereva wa Usalama wa Taifa, Emmanuel Joseph, mkazi wa Karakata, kisha kumpiga risasi ya mguuni na kumpora gari alilokuwa akiliendesha.Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo limetokea jana saa 5 usiku eneo la Makumbusho Kinondoni. Imedaiwa kuwa dereva huyo, akiwa na gari hilo aina ya Toyota Town Hiace, alipofika maeneo hayo ghafla alivamiwa na majambazi ambao walikuwa wakimfuatilia kwa pikipiki. Imedaiwa kuwa majambazi hao walimfyatulia risasi dereva huyo iliyompata mguu wa kushoto. Shuhuda wetu amedai kuwa inawezekana majambazi hao walianza kumfuatilia mbali mtu huyo kwa kuwa alikuwa akitokea Ubungo na mara baada ya kufika eneo hilo ndipo walipokamilisha azima yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa kamili ataitoa baadaye. |
No comments:
Post a Comment