*Agongwa na greda kichwani *Kichwa chake chageuka chapati *Chanzo ni kumwelekeza kazi Na Waandishi Wetu, Manyara JESHI la Polisi Mkoani Manyara linaendesha operesheni kabambe ya kumsaka dereva Mwaisiga Emmanuel (22), kwa tuhuma za kugomnga hadi kumuua mkandarasi wa Kichina aliyekuwa akimuelekeza afanye kazi kwa ufasaha. Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmela Sumari amesema kuwa, ajali hiyo imetokea Desemba 31, mwaka jana, saa 10 jioni. Amesema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Babati iendayo Kateshi eneo la Kijiji cha Endagaw wilayani Hanang. Amesema kuwa, mkandarasi huyo Giangao Ged (20), imedaiwa kuwa, alikuwa na kawaida ya kumuelekeza mara kwa mara dereva huyo kulima barabara vizuri jambo ambalo lilionekana kumkera dereva huyo na ndipo alipoamua kumpitishia greda kichwani mkandarasi na kufa papo hapo. Kamanda Sumari amesema kuwa, dereva huyo alitoweka baada ya tukio hilo na upelelezi zaidi unaendelea ambapo uchunguzi wa awali wamebaini kuwa, Emmanuel ni mkazi wa Kigoma. Amewataka wafanyakazi mbalimbali nchini kushirikiana na wageni katika kazi mbalimbali na kuacha tabia ya kusababishiana vifo au kuhatarisha maisha. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Tuesday, 4 January 2011
Dereva amuua mkandarasi wa Kichina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment