Malumbamo yaibuka kati ya Marekani na Russia, IAEA
Malumbano makali yamezuka leo kati ya Marekani na Russia baada ya Moscow kutahadharisha katika kikao cha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) juu ya hatari ya kuvuja kinu cha utafiti wa masuala ya nyuklia cha Syria iwapo majeshi ya Marekani yaishambulia nchi hiyo.
Russia imetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuvuja kinu hicho cha nyuklia baada ya Marekani kuishambulia Syria.
Mwakilishi wa Marekani katika wakala wa IAEA Joseph Macmanus amedai kuwa wito wa Russia wa kufanyika uchunguzi kuhusu uvujaji wa kinu cha utafiti wa nyuklia nchini Syria iwapo Marekani itaishambulia nchi hiyo si kazi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.
Wiki iliyopita Russia ilitahadharisha kuwa iwapo Marekani itaishambulia Syria na kupiga kwa makusudi au kwa bahati mbaya kinu cha utafiti wa nyuklia nchini humo kilichoko katika viunga vya jiji la Damascus, suala hilo lichafua eneo zima la Mashariki na Kati na kusababisha maafa makubwa.
No comments:
Post a Comment