Thursday 30 June 2011

Muungano wa Afrika waishutumu Ufaransa

Kamishna Jean Ping
Kamishna Jean Ping
Kamishna wa tume ya Muungano wa Afrika Jean Ping amesema kuwa uamuzi wa Ufaransa kuwarushia silaha waasi wa Libya kutoka angani ni hatari na kuwa mtindo huo unahatarisha eneo zima.
Ameiambia BBC kuwa hatua hii huenda ikaitumbukiza Libya katika matatizo sawa na yale yanayoonekana katika nchi ya Somalia ambayo imekabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Ufaransa imekiri kuwa iliwapa silaha wapiganaji wa Berber kwa kuzirusha toka angani katika milima ya kusini-mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli.
Wadadisi wanasema kuwa hatua hiyo huenda inakiuka vikwazo vilivyowekwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupinga silaha kupelekwa Libya.
Bw Ping alikuwa anazungumza kutoka Equatorial Guinea ambako viongozi wa Afrika wanakutana katika kikao cha kikele cha Muungano wa Afrika.
Kuna matatizo kadhaa, hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, hatari ya kuigawa nchi, hatari ya kuwepo na somalia nyengine, hatari ya kusambaa silaha kila mahali na vile vile ugaidi. Hatari hizi zitazitia hofu pia nchi jirani.
Kamishna Jean Ping
Suala la Libya inatarajiwa kupewa kipaumbele katika mkutano huo.
Bw Ping amesema kuwa mpango wa amani wa Muungano wa Afrika kwa Libya ulioafikiwa mwezi Marchi bado upo na unafaa. Mpango huu unahusu utaratibu wa amani unaonuiwa kufungua njia ya mazungumzo ya kisiasa.
Taarifa kuhusu Ufaransa kuwapa silaha waasi zilifichuliwa na gazeti la Le Figaro hapo jana.Gazeti hilo liliongeza kusema kuwa Ufaransa haikuwafahamisha wenzake katika kikosi cha kujihami cha Nato kuhusu hatua yake hiyo.

Hofu ya kuendelea kwa mapigano

.
Taarifa hiyo imesema silaha hizo ni pamoja na makombora ingawa maafisa wa Ufaransa wanasisitiza na kuthibitisha kuwa silaha zilizorushiwa waasi hao zilikuwa ndogo ndogo.
Uwamuzi huu inaarifiwa uliafikiwa baada ya mkutano wa mwezi Aprili kati ya Rais Sarkozy wa Ufaransa na kiongozi wa wapiganaji wa waasi Jenerali Abdel Ifatah Younis.
Ufaransa imekuwa ikionesha wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa mapigano haya ya Libya yalioanza mwezi February.
Waasi wameonekana kupiga hatua na wanatumai kuelekea Tripoli kutokea maeneo ya milimani ya Nafusa kilomita 65 kutoka mji mkuu huo.
Urusi na Uchina zimeshutumu mashambulio ya Nato, zikisema kuwa yamevuka mipaka ya azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1973 linaloruhusu hatua za kijeshi kuchukuliwa nchini Libya.
Hatahivyo Marekani inasema kuwa azimio la mwaka 1973 linaruhusu nchi kuwapa waasi silaha licha ya azimio la awali la mwaka 1970 ambalo liliiwekea Libya vikwazo vya silaha.

This is the moment Nicolas Sarkozy was today attacked while meeting and greeting voters in France.

The 55-year-old President was grabbed by a 43-year-old man as he visited the town of Brax, near Toulouse.

'President Sarkozy was shaking hands with people across a crash barrier when he was attacked,' said an onlooker.

The president recoils, with the officials behind him still apparently oblivious to the altercation
The president recoils, with the officials behind him still apparently oblivious to the altercation

The hand of Mr Sarkozy's attacker can be seen on the president's shoulder, taking a good grip of his suit
The hand of Mr Sarkozy's attacker can be seen on the president's shoulder, taking a good grip of his suit


With a fierce tug, the president is pulled towards the crowd of onlookers
With a fierce tug, the president is pulled towards the crowd of onlookers

The president's men react, as Sarkozy pulls himself free
The president's men react, as Sarkozy pulls himself free

'The man reached out as if he wanted to shake the President's hand, but then he grabbed him by the suit lapel and sent him flying.

'Plain-clothes security guards moved in immediately and bundled the attacker to the grounds. The President looked very shaken and white-faced, but otherwise he looked unhurt.'

An Elysee Palace source in Paris confirmed that the attacker had been restrained by four members of the presidential security and protection service.
He said the unnamed attacker, who is French and a local man, was now in custody in nearby Agen.
'He was taken away very quickly, allowing President Sarkozy to continue with his walk-about,' said the Elysee source.

The man faces up to three years in prison and a £40,000 fine if found guilty of assaulting a public figure, said a judicial source in Paris.

Mr Sarkozy's aggressive manner has led to frequent unpleasant incidents while on walk-about. In 2008 he was involved in a crude slanging match with a member of the public at a farm show in Paris, telling him: 'Get lost, you poor cretin'.

Earlier in his presidency, Mr Sarkozy threatened to have a fight with a fisherman who had been baiting him about his high salary.

Mr Sarkozy has also frequently had projectiles including coins and stones thrown at him during trips to high-rise housing estates around major cities.
He also caused widespread anger as Interior Minister by describing a gang of his young tormentors as 'scum'.

Death threats including bullets have also been received for Mr Sarkozy at the Elysee Palace.
Despite all this, today is the first time anybody is thought to have got close enough to physically attack the President.

Earlier this year it emerged that Mr Sarkozy was starting to use a £10,000 bullet-proof umbrella to protect him from attackers.

It followed opinion polls which portrayed him as the most unpopular head of state in recent Gallic history.
The umbrella is carried by security guards who have to be taller than the 5ft 5ins president.

The so called 'Para Pactum' – Latin for 'prepare for peace' – is coated in Kevlar, a high strength material originally used as a replacement for steel in motor racing wheels.

It was not thought to have been available today, because Brax was considered a peaceful small town, and the hot summer weather would have made an umbrella look incongruous, said the Elysee source.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akipokea kabrasha ya mpango mkakati la maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Issa Ahmed Othman ofisini kwake Migombani

Na Abdi Shamnah
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, kupanua wigo wa kujitangaza ili kuimarisha soko la Utalii nchini.
Amesema hayo leo ofisini kwake Migombani, wakati alipozungumza na ujumbe wa Bodi hiyo, uliofika kwa ajili ya kujitambulisha.Ameitaka Bodi hiyo kufanya juhudi kubwa za kuitangaza Zanzibar kiutalii ili kuvutia soko lake ambalo alisema limejaa vivutio kadhaa an kutoa wito wa kuviendeleza vivutio hivyo.
Alisema moja ya njia muhimu ya kuitangaza ni pamoja na kushiriki katika matamasha mbali mbali yanayofanyika kila mwaka Duniani kote, ambako Makampuni na wadau wa sekta hiyo hukutana na kuonyesha vivutio vya nchi wanazotoka.
Alisema katika kuimarisha soko hilo, Serikali inalenga kuwa an Wawekezaji makini watakaowekeza katika ujenzi wa hoteli zenye hadhi kubwa ya nyota tano pamoja na kuwa na kumbi za mikutano ili kuvutia watalii, pamoja na kutoa fursa ya kufanyika kwa mikutano ya kimataifa.
Akizungumzia mafanikio ya sekta hiyo, Maalim Seif alipongeza juhudi zinazochukuliwa na Kamisheni hiyo pamoja an wadau nchini, hali iliopelekea kuwepo ongezeko la uingiaji wa watalii na kutaka jitihada zaidi zichukuliwe kuongeza idadi hiyo, kwa kuzingatia nafasi nzuri iliyonayo Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine za Visiwa ikiwemo Maldvies.
Alisema ongezeko hilo limeweza kuimarisha shughuli za utoaji huduma muhimu, ambapo wananchi hupata fursa za kuuza mazao yao mbali mbali katika mahoteli.Alipongeza hali ya upatikanaji wa ajira kupitia sekta hiyo, inayokadiriwa kufikia nafasi 20,000 (kwa ajira rasmi) na 45,000 kwa ajira zisizo rasmi kwa mwaka, na kusema hali hiyo inatia moyo sana.
Aidha alionya juu ya matukio mabaya yanayoikabili dunia wakati huu, hususan katika nchi za Kiarabu na kusema kuwa moja ya vyanzo vya matatizo yake yanatokana na vijana kukosa ajira, baada ya kumaliza masomo yao.Hata hivyo, alishangazwa na taarifa za kuwepo tatizo la takwimu (idadi halisi) ya watalii wanaoingia nchini, ikizingatiwa kuwa kuna milango miwili tu ya Uwanja wa Ndege na Bandari, inayotumika rasmi kwa safari zao.
Aliitaka Bodi hiyo kushirikiana na wadau wa sekta hiyo, katika kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazokabili, ikiwemo Idara ya Uhamiaji yenye jukumu la kurikodi taarifa za kuingia na kutoka kwa wageni wote nchini.
Akigusia uharibifu wa mazingira unaotokana na maendeleo kiutalii na maeneo ya kitalii, Maalim Seif alisema, suala la uhifadhi wa mazingira (ambalo liko chini ya Ofisi yake), lina umuhimu mkubwa na kulitahadharisha Taifa kuwa lisipokuwa makini katika uwekezaji, litajikuta mazingira yake kuwepo hatarini.
Alisema eneo la Maruhubi (Maruhubi Ruins),likiwa moja ya eneo lenye uharibifu mkubwa wa mazingira na kutia doa shughuli za kiutalii, hivi sasa linashughulikiwa kwa kufukia mashimo kwa taka, ili hatimae mashimo hayo yafukiwe kwa mchanga.
Alieleza kuwa sehemu hiyo inaingia katika mpango wa Serikali wa ujenzi wa Bandari ya Mizigo kutoka eneo la Mpigaduri. Alipongeza hatua ya baadhi ya wawekezaji kisiwani Pemba ya kujenga Hoteli za kitalii bila ya kukata miti, hatua aliyosema ni matumizi mazuri ya uhifadhi wa ardhi ndogo iliopo.
Katika hatua nyingine, Maalim Seif alitumia fursa hiyo kuukosoa mfumo wa Kamisheni hiyo uliopo, na kusema ni vigumu kujiendesha kama Idara, akiainisha umuhimu wa kujitegemea kwa kuwa na mfuko wake ili kuendeleza shughuli zake.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Issa Ahmeid Othman alisema moja ya changamoto kubwa inayoikabili Bodi hiyo wakati huu ni juu ya uimarishaji wa soko lake, hali inayotokana na sababu mbali mbali ikiwemo mashirikiano duni na baadhi ya wadau wa sekta hiyo.
Alisema mbali na kuwepo mafanikio katika ujio wa watalii nchini,suala la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya maeneo (ikiwemo Maruhubi) nalo limekuwa changamoto kubwa inayowafanya wageni kuacha ujumbe mbaya mara wanapoondoka.
Aidha alisema urasimu kutoka katika baadhi ya taasisi za Serikali, imekuwa kikwazo kwa Bodi hiyo kuwa mfuko wake wa kujiendesha.Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii nchini, inafanyakazi chini ya sheria namba 6 iliorekebishwa mwaka 2009.


Na Salma Said
Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akiongea katika moja ya vikao vyake na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Zan ID LAWAMANI
WAJUMBE Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamehoji fungu kubwa lililotengwa kwa ajili ya Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Makaazi (Zan-ID) na utumiaji mbaya wa fedha za walipa kodi na urasimu unaofanywa na idara hiyo.
Wakichangia hutuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ya mwaka wa fedha wa 2011-2012 wawakilishi hao wamesema utumiaji wa fedha katika idara hiyo umekuwa mkubwa mno.
Aidha wawakilishi hao walihoji fungu lililotengwa na serikali kwa ajili ya idara hiyo ambayo tokea kuanzishwa kwake imekuwa ikilalamikiwa na kushutumiwa kwa ubaguzi wa kutoa vitambulisho hivyo kwa misingi ya kichama ambapo Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema idara hiyo baijaweza kutenda haki katika kwa baadhi ya wananchi wenye kutaka vitambulisho mbali ya uasimu mkubwa uliopo katika upatikanaji wa vitambulisho hivyo.
Akichangia hotuba ya bajeti Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alisema anashangazwa kwamba fungu lililotengwa kwa ajili ya ofisi hiyo mwaka jana lilikuwa shilingi 910 millioni lakin mwaka huu limezidi na kufikia shilingi 1248 milioni.
Alisema kipindi cha mwaka jana kulikuwa na harakati nyingi zikiwemo zile za uchaguzi na utayarishaji wa ofisini hiyo lakini jambo la kushangaza wakati ofisi yatari imeshajipanga kuongezeka idadi hiyo ya fedha wakati sasa ni muendelezo wa shughuli zake.
“Inakuwaje fedha zilizotengwa zizidi kiasi hiki wakati mwaka jana tuliua kuna uchaguzi na mazonge mengi tu ya utoaji wa vitambulisho ambavyo ni vingi lakini kwa nini mwaka huu bajeti hiyo iongezeke kiasi hicho wakati hhaikupaswa kuzidi kiasi kama hicho” alihoji Jussa.
Jussa alisema katika ununuzi wa vifaa na matengenezo pia kuna fedha nyingi zimetengwa ambazo hazilingani na hali halisi ambapo katika bajeti iliyopita kulitengwa shilingi 15 millioni lakini katika bajeti ya mwaka huu imezidi na kufikia shilingi 50 millioni.
Aidha katika fungu la ushauri nasaha kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi idara hiyo imetengewa shilingi 2 millioni katika bajeti iliyopita na bajeti ya mwaka huu zimeengezeka na kufikia shilingi 12 millioni kwa Unguja wakati upande wa Pemba bajei yao ni hiyo hiyo kama ya mwaka jana 2 millioni.
“Kwa nini kwa upande wa Pemba ziwe shilingi 2 millioni kama mwaka jana lakini kw aupande wa Unguja ziwe zimedidi na kufikia shilingi 12 milioni ina maana maambukizi ya ukimwi amezidi kiasi kico kwa upane wa Unguja? Alihoji Jussa ambaye tokea kuanza kwa bajeti amekuwa akihoji namna ya fedha zinavyotumika kwa kila kifungu.
Akichangia suala la urasimu Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (CUF) Salim Abdalla Hamad alisema bado wananchi wananyimwa vitambulisho ambavyo ni haki yao ya kikatiba licha ya kelele nyingi zilizopigwa juu ya idara hiyo ambayo inayoa vitambulisho kwa ubaguzi.
Hamad ameitaka idara hiyo kuondosha urasimu na msururu wa vikwazo visivyo na msingi kwa ajili ya wananchi kupata vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kwani hiyo ni haki yao kikatiba
“Mheshimiwa naibu spika vitambulisho vya ukaazi ndiyo utambulisho wa mzanzibari katika nchi yake ambavyo hivi ni muhimu sana lakini leo wananchi wananyimwa kwa makusudi tunaomba suala hili lishughulikiwe ili kila mwananchi apate haki yake…na urasimu uondolewe” alisisitiza Mwakilishi huyo.
Alisema licha ya katiba kutamka bayana kwamba kila mwananchi anayefikisha umri wa miaka 18 anastahiki kupatiwa kitambulisho hicho lakini idara inayohusika imekuwa kikwazo katika kuwapatia wananchi vitambulisho hivyo imekuwa ni shida kubwa kwa idara hiyo.
Salim alisema matokeo yake wananchi wengi walishindwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa sababu hawana vitambulisho hivyo na kwa mujibu wa sheria kama huna kitambulisho huwezi kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
“Kitendo cha kuwanyima wananchi vitambulisho vya ukaazi wa mzanzibari ni ukiukwaji wa katiba na haki za binaadamu kwa sababu wananchi wanashindwa kupiga kura katika nchi yao wakati kisheria wana haki ya kufnaa hivyo …serikali tunaoimba ilishughulikie suala hili” alisema.
Hamad aliitaka serikali kuhakikisha kwamba wananchi wanapata vitambulisho hivyo na kuwawezesha kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Mwakilishi huyo amesema Zanzibar imetoka mbali katika migogoro ambayo imesababishwa na matatizo kama hao ya kisiasa jambo ambalo serikali inatakiwa kujifunza ili kutorejea walipotoka kwani hali ilivyo sasa ni ya amani zaidi na inahitaji kuendelezwa.
Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni (CUF) Subeit Khamis Faki alisema haoni sababu ya wananchi wa Zanzibar kukoseshwa vitambulisho vya ukaazi kwa kukosa cheti cha kuzaliwa kwa kuwa wazanzibari wengi haakuwa na vyeti vya kuzaliwa kutokana na kuokuona umhimu wa kuwa na vyeti na elimu juu ya suala hilo haikuwepo huko nyuma.
Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita wapo wananchi wengi wakiwemo watu wazima walikosa kupiga kura kwa sababu hawana vyeti vya kuzaliwa jambo ambalo wamenyimwa haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
“Mheshimiwa Spika kasoro hii tunatakiwa kuirekebisha mara moja…haiwezekani mtu kukosa cheti tu cha kuzaliwa na hivyo kumkosesha kupata kitambulisho cha mzanzibari mkaazi hali ambayo inamfanya kushindwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu tunaomba sana hili litizamwe kwa umakini” alisema Faki.
Mwakilishi huyo alisema Serikali irekebishe kasoro hizo ambazo aliziita ni kubwa sana zinazotishia uhuru wa demokrasia katika mfumo wa vyama vingi ikiwemo wananchi kukosa haki zao za msingi ikiwemo kupiga kura na kupata haki nyengine kama pasi za kusafiria kwa kuwa usipokuwa na kitambulisho huwezi kupata pasi ya kusafiria na baadhi ya mambo mengine.
Katika hatua nyengine Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wananchi ambao hadi sasa hawana vitambulisho vya mzanzibari mkaazi na ambao hawajavichukuwa vitambulisho hivyo kwenda katika ofisi za idara hiyo na kuchukuwa.
Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud Mohammed aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa viti maalumu, Kazija Khamis Kona wa (CUF) aliyetaka kujuwa suala la vitambulisho na Serikali imejipanga vipi katika uchaguzi mkuu ujao.
Aboud alisema yamekuwepo malalamiko ya wananchi kuhusu vitambulisho vya ukaazi wa mzanzibari mkaazi ambapo wananchi wengi wadai kwamba hawajapata vitambulisho hivyo lakini vitambulisho vipo vinasubiri wenyewe.
Alisema nia ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona wananchi wote wanapata vitambulisho hivyo kwa mujibu wa sheria kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba.
Alisema zipo jumla ya kadi za vitambulisho vya mzanzibari mkaazi vipatavyo 42,000 katika ofisi za idara hiyo ambavyo wananchi wameshindwa kwenda kuzichukuwa.
Aboud alisema wakati wananchi wanalalamika kukosa kadi za vitambulisho vya ukaazi wa mzanzibari lakini kumbe kadi hizo zipo katika ofisi za idara ya vitambulisho katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi,huwezi kupiga kura katika uchaguzi mkuu kama utakosa kadi ya usajili wa mzanzibari ambapo pia ni kosa kwa mujibu wa sheria mtu atakayefikisha umri wa miaka 18 kukosa kitambulisho hicho.

Mtondoo magerezani basi tena

NaSalma Said

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini

MAGEREZA KUSHUGHULIKIWA
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuyashughulikia malalamiko yaliotolewa na wawakilishi ya kuimarisha magereza, watuhumiwa na wafungwa ambao wanakosa haki zao za msingi kwa muda mrefu.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini alisema hayo wakati akifanya majumuisho ya hoja mbali mbali za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotoa wakati wa kuchangia hutuba ya majeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi kwa mwaka wa fedha 2-11-2012.
Waziri huyo alisema serikali itaimarisha magereza yake yaliopo Unguja na Pemba yanaimarishwa na kutengenezwa pamoja na watuhumiwa kuwekwa katika mazingira mazuri ikiwa pamoja na kupatiwa haki zote za msingi za kibinaadamu. Kama ilivopendekezwa na wajumbe hao.
Aliwaambia wajumbe hao kwamba katika kulishughulikia suala hilo timu ya wataalamu kutoka wizara ya afya inakusudia kufanya ziara katika magereza ya Unguja na Pemba kwa ajili ya kuangalia hali za afya za wafungwa na magereza kwa ujumla.
“Mheshimiwa naibu spika tumesikia kauli za wajumbe wa baraza lako tukufu waliokuwa wakichangia bajeti ya wizara hii wamesema hali za magereza ni mbaya na wafungwa bado hali zao haziridhishi timu ya wataalamu kutoka wizara ya afya itatembelea katika magereza yetu yote kuhakikisha tunawaangalia afya zao wafungwa na wale watuhumiwa ili kwenda sambamba na azimio la kuheshimu haki za binaadamu” alisema waziri huyo.
Alisema hivi sasa hakuna tena utaratibu wa kutumia ndoo za kwa kwenda haja ‘mtondoo’ katika magereza kwani ni hatari na zinaweza kusababisha hali mbaya ya kiafya kwa wafungwa kwa ujumla kuata maradhi hasa yale ya mripuko na kuharisha.
“Waheshimiwa tumeondowa mtondoo kuweka katika chumba cha wafungwa safi na chenye mazingira mazuri kiafya hili tumeliondowa kwa kuzingatia suala la afya kwa waliopo ndani” alisema Mwinyihaji ambapo Mtondoo ni ndoo zinazotumiwa kujisaidia kwa haja ndogo na kubwa kwa wafungwa ambapo huweka ndani ya chumba chao na kwa anayetaka kujisaidia hujisaidia humo humo chumbani na utaratibu wao ni atakayejisaidia mwisho ndiye hubeba ndoo hiyo na kwenda kuimwaga nje, utaratibu huo umepigiwa kelele kwa muda mrefu wanaharakati wakielezwa ni kwenda kinyume na misingi ya haki za binaadamu.

BAJETI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS YAPITA

Na Kauthar Abdulla
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo iliyowasilishwa juzi Barazani hapo na Waziri wa Wizara hiyo Fatma Abdul-habib Ferej.

Bajeti hiyo ilipitishwa baada ya wajumbe wa Baraza hilo kuridhishwa na ufafanuzi wa hoja na masuali yao waliyoyatoa kupata ufafanuzi kutoka kwa waziri huyo.

Akitoa ufafanuzi wa huo Waziri Fatma alisema ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais nje ya nchi zilikuwa na maslahi na faida kubwa kwa maendeleo ya Zanzibar.

Waziri huyo alitaja baadhi ya faida za ziara za Makamu wa Kwanza wa Rais nchi za Mashariki ya Kati ni pamoja na kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji ambao baadhi yao wameonesha nia ya
kushirikiana na Zanzibar.

Mbali ya faida hiyo, waziri huyo alisema pia yalifanyika mazungumzo nchini Oman ya kuanzisha Shirika jipya la ndege la Zanzibar, msaada wa uchimbaji mafuta, pamoja na Shirika la ndege la nchi hiyo kuanzisha safari za moja kwa moja visiwani hapa.

Waziri alilazimika kutoa ufafanuzi huo, baada ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu, kutaka aelezwe faida ya safari hizo ambazo hapo awali hazikuainishwa katika kitabu cha bajeti ya ofisi hiyo.

Aidha waziri huyo alisema mbali ya faida hizo, pia yalifanyika mazungumzo ya kuomba msaada wa ujenzi wa Bandari mpya na kudumisha uhusiano mwema baina ya Zanzibar na nchi za eneo hilo.

Akielezea kwa nini bajeti ya UKIMWI imevimba ikilinganishwa na Idara nyengine, alisema hali hiyo inatokana na kuwepo majukumu mengi na watalaamu sekta hiyo kuhitaji fedha nyingi katika kulishughulikia tatizo la maradhi hayo ambayo yamekuwa janga la jamii.

Alisema sekta za utalii zinapaswa kuwa na mikakati ya kupunguza kasi ya maambukizi ya UKIMWI, pamoja na kuongeza kasi ya mapambano hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar imekuwa na uingiaji na utokaji mkubwa wa watu.

Alifahamisha kuwa tatizo la maradhi ya UKIMWI limekuwa kubwa na msingi wa kuondoka kwake na kulimaliza kabisa ni mabadiliko ya tabia za watu katika kuachana na mambo yenye kuongeza kasi ya maambukizi.

Akizungumzia juu ya tatizo la dawa za kulevya, waziri huyo alisema Ofisi iko kwenye mikakati ya kuangalia mapungufu ya sheria ili kuweza kuzuia uingiaji wa dawa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiathiri vijana ambao ndio nguvu kazi ya uchumi wa Taifa.

Kuhusu uharibifu wa maliasili zisizorekebishwa alilifahamisha baraza hilo kuwa Ofisi yake ipo hatua za mwisho kuweka kanuni ambazo zitasaidia kuzilinda na kuzihifadhi kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Alisema Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya tabia nchi, ikiwemo mashamba kuingia maji ya bahari, maji kuingia chumvi na hata baadhi ya maeneo kumegwa na bahari na kubainisha kuwa Ofisi inaandaa mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakichangia bajeti ya Ofisi hiyo wajumbe hao wajumbe wa Baraza hilo waliomba nyumba za Sober House ambazo zimekuwa zikiwahifadhi vijana walioacha matumizi ya dawa za kulevya kujengwa mbali ya nyuma za makaazi ya watu.

Aidha walisema maradhi ya UKIMWI yamekuwa tatizo kubwa na kusisitiza haja ya kuwepo mabadiliko hasa katika mavazi huku wakitilia mkazo kudumishwa kwa mila na silka za Kizanzibari.

Wawakilishi hao pia walionesha kukerwa na tabia mbaya za uchafuzi wa mazingira hasa ya uchimbaji wa mchanga katika maeneo kadhaa huku sheria za zikikiukwa.

Tabia ya ubakaji wa watoto katika jamii ya visiwa vya Zanzibar

Tabia ya ubakaji wa watoto katika jamii ya visiwa vya Zanzibar, inaonekana ikizidi kuota mizizi siku hadi siku kutokana na ufatiliaji usio makini wa vyombo vya sheria, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limewachosha wananchi na kukata tamaa kabisa ya kupata haki pindipo watoto wao wanapopatwa na kadhia ya ubakaji .
Wengi wetu tunajiuliza ni kwa nini iwe hivi kila siku utasikia kesi imekosa ushahidi na matokeo yake kuishia visivyojulikana bila ya kujali athari alizozipata mtoto lakini cha kusikitishwa wabakaji kuachiwa watambe mitaani wakiwa hawana hata chembe ya wasi wasi.

Hii ndio hali halisi iliyozoeleka kwa muda mrefu sasa, hadi masikio yetu yamezoea kusikiliza leo mtoto wa Fulani kabakwa na kesho wa Fulani lakini kesi zao hazina ushahidi wa kumtia mtendaji wa kosa hatiani.

Hebu tujiulize kukosa ushahidi kwa kila kesi za ubakaji na udhalilishaji ndio utendaji sahihi wa kazi? utendaji ambao unawapa fursa watu wenye roho za kinyama kuendeleza vitendo vya ubakaji huku wakijua dhahiri kwamba hakuna kitakachofanyika dhidi yao .

Hivi karibuni Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alikemea vikali kuhusu ongezeko la vitendo hivi na kuitaka idara ya mahakama kuacha tabia ya kuzipiga danadana kesi za ubakaji na kutaka zishughulikiwe haraka iwezekanavyo.

Alionesha kukasirishwa sana na utendaji wa vyombo vya sheria kwamba inasikitisha kuona kesi zinazofunguliwa zinaishia kilholela kwa kisingizio cha kukosa ushahidi hata pale mtuhumiwa anapopatikana akiwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo.
Kutokana na utendaji huu usio wa uhakika isipokuwa ni nenda rudi ya kila siku bila mafanikio, ni lazima wananchi wakose imani ya kuripoti kesi zao katka vituo vya sheria na hatimae kufikia kuchukua hatua mikononi mwao jambo ambalo kisheria halikubaliki.
“haiwezekani kuwaachia wabakaji watambe, mahakama nenda rudi zisikuwepo kama ushahidi upo sheria ichukue mkondo wake, haipendedezi mbakaji kukutwa juu ya mgongo bado hakuna ushahidi mnataka ushahidi gani?”alihoji Balozi Iddi .
Wakati akifungua kituo cha kuwahudumia waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto (One Stop Centre ) kilichopo katika hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zazibar,

Balozi Iddi aliitaja idadi ya watoto waliobakwa tangu mwaka 2006 hadi kufikia mwaka 2010 imefikia 3,116 matukio ambayo yameripotiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja , Makunduchi, kivunge, Abdalla Mzee, Chake Chake na Wete ambapo kati ya takwimu hizo yamo matukio ya ubakaji na mamba za utotoni.
Kwa kweli juhudi za Serikali katka kupambana na tatizo la makosa ya ubakaji na udhalilishaji kwa wanawake na watoto ni kubwa sana ili kuona matendo hayo yanafikia kikomo, lakini bila ya mashirikiano ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa au kumwaga chumvi baharini.

Kuanzishwa kwa kituo hicho ni hatua muhimu itayowezesha kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na lengo kuu ni kuona kazi zinazohitajika zinafanyika ipasavyo pamoja na kuwarejeshea matumaini wananchi hasa wale wanaofikwa na matatizo hayo kama ni watu wenye mahitaji muhimu, na kukifanya kituo kuwa endelevu na sio Non Stop Centre badala ya One Stop Centre.

Itakuwa ni jambo la busara sana kama kituo hichi kitahakikisha kinapambana na wale wote wenye tabia ya kuendeleza vitendo vya udhalilishaji vikiwemo ubakaji kwa wanawake na watoto na hakuna budi kufanya kazi kwa bidii bila ya kuoneana aibu ambayo mwisho wa siku inatuweka katika rekodi mbaya ya kuwa na idadi kubwa ya kesi za udhalilishaji na ubakaji.

Mkoa wa Kaskazini unguja umetajwa kuwa ndio unaongoza kwa matendo ya ubakaji jambo ambalo lilikemewa vikali na mhe Balozi Seif ikizingatiwa ndio mkoa wake anakotoka, amewataka waache mara moja vitendo hivyo na wale wataobainika kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yao.

Ni mara nyingi sana kusikia kuhimizwa kwa polisi, madaktari na wanasheria kufanya kazi zao kwa mashirikiano na umakini mkubwa, ikizingatiwa wao ndio wadau wakubwa wa kikimbiliwa pindipo yanapotokea matatizo na wanategemewa kuwa waadilifu katika kuyapatia ufumbuzi.

Kufunguliwa kwa vituo vya kutoa huduma za matendo yatokanayo na udhalilishaji wanawake na watoto ni miongoni mwa juhudi za serikali katika kujivua gamba la aibu la kuwa na wimbi kubwa la kesi za udhalilishaji ambazo hazitafutiwa ufumbuzi wowote, hivyo basi kinachohitajika kuonekana ni utendaji wa kazi na haki bila ya kujua mtendaji wa kosa ni nani na ana cheo gani.
CUF yapata pigo Mtwara


Aliyekuwa mwanachama wa CUF na mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita, Mohamed Chiungulumana akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipotangaza kurejea CCM kwenye mkutano uliofanyika 28/6/2011 mjini Mtwara. Jumla ya wanachama 154 wa CUF walijiunga na CCM katika mkutano huo.Kuhsoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma
CHAMA cha CUF kimepata pigo mkoani Mtwara, baada ya wananchama wake 154 kutangaza kukihama chama hicho na kukabidhi kadi zao kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini hapa.
Baada ya kutangaza kuhama CUF wanachama hao walikabidhiwa kadi za CCM na kusema wameamua kuhamia CCM baada ya kubaini kwamba viongozi wa CUF wanapigania maslahi yao binafsi na si ya wananchi kama ambavyo wamekuwa wakijinadi.
“Nisingependa kusema mengi siku ya leo, kwa kuwa nina furaha sana kurudi nyumbani, nimerudi na wenzangu baada ya kubaini kwamba wale viongozi wa CUF hawapiganii maslahi yetu wananchi bali yao binafsi”, alisema, Mohammed Chiungulumana baada ya kukabidhi kadi yake ya CUF kwa Nape na kupewa ya CCM.
Chiungulumana ambaye alikuwa mgobea udiwani Mtwara mjini, aliwataka Watanzania kuacha kuhadaika na vyama vya upinzani kwa sababu hawataambulia chochote kama ilivyomtokea.
Mapema akihutubia mkutano huo uliofurika mamia ya watu, Nape alisema, alisema vyama vya upinzania ni sawa na baba wa kambo ambaye huonyesha mapenzi kwa mtoto kwa sababu ya kumfurahisha mama wa mtoto huyo hivyo viongozi wa upinzani wanapopiga kelele kwamba wanatetea haki za wanannchi huwa si kweli bali wanatengeneza mazingira ya kuboresha maisha yao binafsi.
Alisema, ni kutokana na tabia hiyo ndiyo sababu serikali inapopanga mipango mizuri yenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi wapinzania huibuka kupinga kwa kuwa kufanikiwa kwa mipango hiyo huwakosesha njia ya kuwalaghai wananchi.
Nape alisema moja ya mfano wa tabia hiyo ya wapinzani kuwa ni ule uliotokea katika bunge wakatika kupitisha bajeti ya mwaka 2011/2012, katika kikao kinachoendelea mjini Dodoma.
Alisema, baada ya CCM kuituma serikali iondoe ushuru kwenye mafuta ili kupunguza ukali wa maisha uliosababishwa na kupa kwa bei ya nishati hiyo, katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa upinzania walipinga isipitishwe lakini ikafanikiwa kupita kwa kuwa idadi yao ni ndogo kuliko ya wale wa CCM.
Nape alitumia fursa hiyo kufafanua kwa kina sababu na hatima iliyopo sasa baada ya maamuzi yaliyofanywa na CCM Aprili mwaka huu, katika kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma.
Alisema baada ya mabadiliko hayo hanayiotwa kujivua gamba, CCM imeongeza uwezo zaidi katika utendaji wake ikiwemo kusimamia serikali ili iweze kutekeleza vilivyo ilani ya uchaguzi ya Chama na pia kusogea zaidi kwa wananchi ili kukifanya Chama kuwa chao kuliko ilivyoanza kuonekana miaka ya karibuni.
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma ambaye ameambatana na Nape katika ziara ya mkoani hapa, alisema, baada ya mabadiliko hayo Chama kitahakikisha, kinaendesha taratibu zake kisayansi zaidi ikiwemo kuweka uratibu wa kuwajua kwa undani wanachama wake.
Alisema kufanya hivyo kutasaidia kuondoa wanachama mamluki ambao hawana manufaa kwa Chama kwa kuwa wengi wao hukisaliti Chama wakati wa uchaguzi.

Wednesday 29 June 2011

Mwanamke wa kwanza kuongoza IMF

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Christine Lagarde ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF.
Christine Lagarde
Lagarde ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza IMF
Kufuatia uteuzi huo Ufaransa itakuwa imeshikilia kiti hicho kwa miaka 26 kati ya miaka 33 iliyopita.
Christine Lagarde mwenye umri wa miaka 55, alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa waziri wa fedha katika muugano wa nchi saba zilizostawi maarufu kama G-7.
Lagade anatarajiwa kujiuzulu kutoka serikali ya Ufaransa ili kuandikisha historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuongoza shirika la fedha duniani IMF.
Uteuzi wake umefuatia kujiuzulu wa mfaransa mwenzake Dominique Strauss Kahn, baada ya kukabiliwa na kashfa ya ubakaji.
Sio wengi walioshangazwa na uteuzi wa wakili huyo wa zamani ambaye ana sifa nzuri kote duniani.
Amekuwa msuluhishi wa matatizo mengi ya kiuchumi yanayokumba mataifa kadhaa barani ulaya katika miaka ya hivi karibuni.
Kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa ameungwa mkono na China na India na hivyo kuteuliwa kwake kama mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la fedha duniani ilikuwa jambo lililotarajiwa.
Kuna maelewano ambayo hayajanakiliwa kuwa raia wa mataifa ya bara ulaya pekee ndio wanaopaswa kuteuliwa kuhudumu kama mkurugenzi mkuu wa IMF huku raia wa marekani wakipewa nafasi za kuongoza benki kuu ya dunia.
Mataifa yaliostawi yanataka kupewa nafasi kuu katika siasa za dunia, lakini huu ni wakati mgumu kwa mataifa ya ulaya huku mzozo wa kiuchumi wa Ugiriki ukitishia kuathiri mataifa mengine katika kanda hiyo.
Muungano wa ulaya na IMF zimeishurutisha serikali ya Ugiriki kupunguza matumizi yake ili kuendelea kupata msaada kutoka kwao.
Lagarde amekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kutatua matatizo hayo ya nchi wanachama wa EU. 

Radi yasababisha vifo zaidi Uganda

Nchini Uganda radi imesababisha vifo vya wanafunzi 18 na wengine 50 kujeruhiwa ilipopiga shule moja ya msingi magharibi mwa nchi hiyo.
Uganda
Ramani ya Uganda
Msemaji wa polisi Judith Nabakooba ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wanafunzi wakike 15 na wakiume watatu walikufa jana jioni katika shule ya msingi ya Runyanya wilaya ya Kiryandongo.
Wasiwasi kuhusu mfululizo wa radi kali zinazoipiga Uganda kwa wakati huu umesababisha wabunge nchini humo kulijadili suala hili bungeni.

Wasiwasi


Wiki iliyopita watu wasiopungua 28 waliuawa na radi na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa mwanasayansi anayeshughulika na masuala ya hali ya hewa kutoka Uganda Kiza Aderi, ukosefu wa vifaa vya kukabiliana na radi katika majengo kadhaa huenda ikiwa ni moja wapo ya sababu zinazosababisha watu kuuawa na radi.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Kiryandongo Patrick Byaruhanga ameliambia gazeti la taifa la New Vision kuwa radi hiyo ilipiga karibu saa kumi unusu jioni za Uganda wakati wanafunzi walikuwa bado madarasani wakisubiri mvua itue kabla ya kwenda nyumbani.
Msemaji wa polisi amesema baadhi ya waliopata majeraha makubwa wamepelekwa katika hospitali ya Mulago katika mji mkuu wa Kampala kilomita 200 kusini mashariki ya Uganda.
Nchi ya Uganda inashuhudia kipindi cha mvua na dhoruba kali na visa vya vifo kutokana na radi vimewatia watu wengi wasiwasi.

Misri: Mapigano mapya yazuka Tahrir

mamia ya waandamanaji wakiwa eneo la wazi la Tahrir
Polisi nchini Misri wamepambana na mamia ya waandamanji wanaoipinga serikali mjini Cairo katika eneo la wazi la Tahrir na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.
Polisi wa kuzuia ghasia walitumia mabomu ya machozi kujaribu kutawanya waandamanaji, wengi wao waliwarushia mawe polisi.
Uwanja wa Tahrir ulikuwa kitovu katika mageuzi ya mwezi Februari yaliyosababisha Rais Hosni Mubarak kuachia madaraka.
Wengi wa waandamanaji walikuwa wanataka kesi za maafisa wa zamani ziendeshwe kwa haraka.
Hadi kulipopambazuka alfajiri, mawe na vioo vilikuwa vimetapakaa mitaani karibu na eneo la Tahrir.
Walioshuhudia walisema ilikuwa ni ghasia mbaya kuwahi kutokea katika wiki kadhaa.
Vurugu zilianza Jumanne wakati polisi walipowafukuza katika ofisi za Televisheni ya Taifa wanafamilia wa wale waliouawa katika vurugu za mwezi Februari, wanaharakati walisema.
Baadaye waandamanaji walikusanyika nje ya ofisi za wizara ya mambo ya ndani na kupambana na polisi.
Mapigano yalisambaa na kufika katika eneo la Tahrir ambako polisi waliokuwa na ngao za kuzuia ghasia waliwazuia kuingia katika mitaa mikubwa ambayo ilikuwa na magari kadhaa ya usalama.
Wakati mabomu ya kutoa machozi yakimiminika majeruhi walionekana wamelala chini baadhi wakititikwa na damu
"Watu wanataka kuondolewa kwa utawala," baadhi ya waandamanaji walikuwa wakiimba.
Ahmed Abdel Hamid, mwenye umri wa miaka 26, ambaye alikuwa miongoni mwa waandamanaji alisema watu walikuwa wamekasirika kwa kuwa kesi mahakamani dhidi ya maafisa waandamizi zilikuwa
zinacheleweshwa.
Wiki iliyopita waziri wa zamani wa Biashara nchini humo Rachid Mohamed Rachid alihukumiwa miaka mitano jela bila kuwepo mahakamani kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

Afrika yahitaji msimamo juu ya Libya

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Mataifa ya Afrika wanakutana mjini Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea kwenye mkesha wa Mkutano wa kilele wa viongozi wa Mataifa wanachama wa AU na Libya ikiwa juu ya ajenda ya mkutano.
waasi wa Libya
Waasi wa Libya

Itabidi Maofisa hao wa Africa waondowe tofauti zao na wapate suluhisho juu ya mgogoro nchini Libya.
Waziri wa Libya wa m,ashauri ya kigeni ameiambia BBC kuwa Kanali Gaddafi atakubali uwamuzi wa raia wa Libya ikiwa watamkataa kupitia Uchaguzi.
Suala kuu kwa Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka kote barani Afrika ni tafsiri ya msimamo mmoja juu ya Libya kabla ya Mkutano wa kilele wa viongozi wa AU hapo kesho.
Lakini Waziri wa Libya wa mashauri ya kigeni Abdul Ati Alobidi ameiambia BBC kuwa ana matumaini kuwa wenzake watajitahidi kumsukuma Kanali Gaddafi akubali suluhu la kisiasa badala ya kushikilia msimamo wake wa kutoshiriki kwa njia yoyote ile mazungumzo kama hayo.
kiongozi Gaddafi
Kanali Muammar Gaddafi

Waziri huyo anasema kuwa kiongozi wa Libya yuko tayari kusikiliza, Nini anataka kusikia?
Na je yuko tayari kung'atuka madarakani, kwa kuitikia sauti za raia wake ikiwa watamkubali kwa kura au kumkataa?
Abdul Ati Alobidi amesema kua daima Kanali Muammar Gaddafi atabaki kuwa mwenye ushawishi katika siasa za Libya mfano wa Nelson Mandela nchini Afrika ya kusini. Wakati huu ambapo masuali yanajitokeza kuhusu uingiliaji wa majeshi ya NATO nchini Libya Mataifa makuu ya magharibi yanatarajia kuona kukiwepo msimamo wa pamoja dhidi ya Gaddafi.
Lakini matarajio kama hayo ni vigumu kufikiwa kutokana na Mataifa ya Afrika kushindwa kuondoa tofauti zao ili mazungumzo ya sasa yaweze kupata muelekeo wa pamoja.

Ufaransa imewapa waasi wa Libya silaha

Muasi wa Libya
Ufaransa imewarushia silaha waasi wanaopigana na majeshi ya Kanali Gaddafi magharibi mwa Libya, jeshi la Ufaransa limethibitisha.
Silaha na risasi zilipelekwa kwa wapiganaji wa kikabila wa Berber katika milima ya Nafusa.
Awali, ripoti iliyotolewa na gazeti la Le Figaro lilisema silaha hizo ni pamoja na roketi na makombora.
Ufaransa, nchi inayoongoza harakati za kijeshi za umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato, haikuwaeleza washirika wao kuhusu hatua hiyo, limesema gazeti la Le Figaro.
Msemaji wa jeshi la Ufaransa, Kanali Thierry Burkhard alisema, " Tulianza kwa kurusha msaada wa kibanadamu: chakula, maji na vifaa vya matibabu".
Aliliambia shirika la habari la AFP, " Wakatai wa harakati hizi, hali ya raia ilizidi kuwa mbaya. Tuliwarushia silaha na vifaa vya kujilinda, hasa risasi.
Posho kumfukuza Shibuda Chadema





MBOWE, ZITTO WASEMA NI MSALITI ASIYEAMINIKA KATIKA CHAMA
Kizitto Noya na Edwin Mjwahuzi, Dodoma
KITENDO cha Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kupingana na sera ya chama chake kuhusu suala la posho za vikao (sitting allowance), kimeichefua Chadema ambayo imemuita msaliti ikisema, "adhabu yake ni kufukuzwa."Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliliambia Mwananchi mjini Dodoma jana kuwa, alikerwa na kauli iliyotolewa na Shibuda ya kwenda kinyume na msimamo kambi hiyo kupinga posho za vikao kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa umma.

Mbowe alisema kwamba kwa kauli yake ya juzi ya kuunga mkono posho ilidhihirisha kwamba mbunge huyo ni msaliti wa kambi hiyo, hivyo sheria zitafuata mkondo wake.

"Kutokana na tukio la jana (juzi) bungeni, Shibuda kutusaliti katika suala la posho za vikao, taratibu za kisheria zitafuata mkondo wake kwani utovu wa nidhamu haukubaliki katika kambi yetu, hata katika chama chetu,"alisema Mbowe na kuongeza:

"Suala la posho si la mtu binafsi, lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chetu na kama kuna kiongozi hafahamu hili basi hakustahili kugombea ubunge kwa sababu naamini Ilani ya Uchaguzi, Shibuda anayo."

"Posho zilijadiliwa na kupitishwa katika vikao maalumu vya chama, kwa hiyo kama Katiba yetu ya chama inavyotuongoza, Shibuda alitakiwa kulipinga katika vikao hivyo sio kutoka nje ya kikao na kuanza kupingana na maamuzi yake,"alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.


Akinukuu kifungu katika Katiba ya chama chake kinachoeleza maadili ya viongozi, Mbowe alisema, "Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni."

Kauli ya Zitto
Kwa upande wake, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge kupingana na sera ya chama chake, ni kutokiamini chama hicho.

"Maana yake hakiamini chama, hivyo hafai kuendelea kuwa mwanachama na mbunge wa chama hicho,"alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.

Aliendelea, "Hapa kuna mambo mawili; masuala ya kisera na masuala ya utaratibu. Mbunge anayepingana na taratibu adhabu yake ni kumwita na kumpa onyo, lakini mbunge anayepingana na sera, huyo hakiamini chama na dhabu yake ni kufukuzwa."

Kwa mujibu wa Zitto, suala la kupinga posho kwa Chadema ni sera kwa kuwa limo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

"Hili (suala la posho), lipo kisera. Kwenye Ilani yetu ya uchaguzi tulisema, tutapunguza mishahara ya wabunge na posho zao. Sasa kama mbunge anachaguliwa kwa sera hiyo halafu anaipinga haradhani, huyo hakiamini chama na chama hakipaswi kumwamini."

Aliendelea,"Sasa, adhabu ya juu kabisa ya mbunge asiyekiamini chama, ni kufukuzwa. Huu ni usaliti. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa chama ameshalitolea tamko suala hilo halafu mbunge anakuja kumpinga hadharani maana yake nini,?" alihoji.

Tundu Lissu je?
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kitendo cha Shibuda kupingana na sera ya chama chake, "ni uasi usiovumilika".

"Sasa nikiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni nadhani ninahitaji kukaa naye. Nitamwita anieleze kulikoni. Aseme kulikoni ameamua kukiasi chama na upinzani kwa ujumla?"

Aliendelea, "Lakini kwa bahati mbaya sana, adhabu kubwa inayoweza kutolewa na kambi ya upinzani ni kumtenga na kambi. Lakini kwa mtu kama Shibuda ambaye tayari anaijua adhabu hiyo na kuitafuta kwa makusudi, inaonekana haitamtosha."

"Kwa sababu hiyo basi, kambi ya upinzani itaenda mbali zaidi baada ya kumtenga. Tutakiandikia chama barua kukijulisha usaliti huo wa mbunge wake halafu chenyewe kina taratibu zake za kinidhamu."

Kauli ya Shibuda
Juzi alipokuwa akichangia Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012, Shibuda alitoa mpya pale alipopingana na misimamo wa Chadema kuhusu malipo ya posho kwa wabunge na watumishi wengine wa umma.

Akitumia lugha yake ya mashairi, Shibuda aliliambia Bunge kuwa utata uligubika posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, unatokana na tafsiri potofu ya neno hilo ambalo asili yake ni Ujira wa Mwia.

"Ujira wa Mwia (sasa posho) yalikuwa malipo anayopewa mtu kwa kazi anayoifanya ili kumwongezea hamasa ya kuendelea kuifanya kazi hiyo. Kwa bahati mbaya sasa neno hilo linaitwa posho na ndiyo sababu linaleta mjadala bungeni,"alisema Shibuda huko akishangiliwa na wabunge wa CCM.

Kwa mujibu Shibuda, kama maana ya posho ni Ujira wa Mwia kama ilivyokuwa ikitumika na wakoloni, haina sababu kuifuta kwa kuwa ndiyo hamasa kwa wabunge na watumishi wengine wa umma kuendelea kufanya kazi yao.

Shibuda alilitahadharisha Bunge kuwa mjadala wa posho umetokana na Bunge kuwa na aina mbili ya wabunge; wabunge maslahi jamii na wabunge maslahi binafsi.

"Wabunge maslahi binafsi hawashiriki misiba, hawatembelei hospitali wakasaidia dawa, hawaendi kwenye sherehe na hawana msaada wowote kwa jamii. Sasa aina hiyo ya wabunge hatutegemei kwa nini watake posho,"alisema

Aliendelea,"tabia ya choyo ndiyo inayowasumbua wabunge hao. Lakini pia tujue kwamba kuna wabunge wafanyabiashara na wabunge maslahi, mbunge maskini hawezi kuacha kuchukua posho, sasa ni vema tukatambua tofauti hizo ili tumalize mjadala huo."

Shibuda alipendekeza posho ziendelee kutolewa tena kwa haraka zaidi na nyongeza kubwa badala ya kuendelea kuvutana kuhusu uhalali wake nje na ndani ya Bunge.

"Mheshimiwa Spika, posho haitoshi, inafaa kuongezwa hadi Sh500,000. Mimi nasema na kazi ya kutafsiri ninachosema inategemea busara ya mtu, lakini posho ziongezwe ili zisaidie wabunge maskini, shughuli mbalimbali za kijamii."

Wakati Shibuda akiwa anaeleza hayo, Mbowe, alionekana akitikisa kichwa kwenye kiti chake.

Msimamo wake
Lakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.

"Nitashangaa kama nitaitwa na kiongozi yoyote wa kambi yetu ya upinzani au Chadema kwa tuhuma za kutoa maoni yangu huru niliyoyatoa bungeni jana (juzi), hata nilipokuwa CCM nilipenda kusahihisha palipokuwa na makosa".

"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".

"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".

Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.

Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".

CCM yatimua makatibu wa mikoa sita


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM,Nape Nnauye akipata maelezo kwa Mhariri mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL),Theophil Makunga (kulia) kuhusu namna magazeti yanavyochapishwa wakati alipotembelea ofisi za MCL,zilizopo barabara ya Mandela,Tabata Relini jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni msaidizi wake Sixtus Mapunda.Picha na Silvan Kiwale
Boniface Meena
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaondoa makatibu wake wa mikoa zaidi ya sita nchini ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa kujivua gamba ulioanzishwa mapema mwaka huu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wahariri wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), alipofanya ziara katika makao makuu ya kampuni hiyo Tabata-Relini jijini Dar es Salaam.

MCL ndiyo inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.Katika ziara hiyo, Nape alisema kuwa zoezi hilo la kuwaondoa makatibu litaendelea hadi ngazi ya makatibu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya falsafa ya CCM ya kujivua gamba.

Alisema kujivua gamba ni dhana pana ambayo msingi wake ni kufanya mabadiliko ya kiutendaji na uendeshaji wa CCM kwa ujumla wake na kwamba yapo mambo mengi ambayo yamefanywa katika kutekeleza azma hiyo.

“Makatibu wa mikoa kama sita au saba hivi wameshaondoka na wengine wamestaafu, ni katika kujivua gamba na tutaenda kwenye wilaya pia,”alisema Nape.

Alipoulizwa iwapo hao walioondoka katika nyadhifa zao wamestaafu au wameondolewa, Nape alijibu kwa kifupi “vyote kwa pamoja”.

Alitaja baadhi ya mikoa ambayo makatibu wake wameondolewa kuwa ni pamoja na Shinyanga, Dodoma na Kagera.

Utaratibu wa kumpata mgombea urais
Alisema jambo jingine ambalo linafanyika kupitia mchakato huo ni chama hicho kuangalia upya utaratibu wa kumpata mgombea urais ambao utakuwa tofauti na uliokuwa ukitumika katika chaguzi zilizopita.

“Kuna kamati inashughulikia hilo,” Nape alisema na kuongeza:
"Pia tunataka tuwe na kamati kama za Bunge ili kutathimini jinsi Serikali inavyotekeleza ahadi ambazo chama kimezitoa ama kupitia wagombea au kwenye Ilani ya Uchaguzi."

Alisema hatua hiyo itakiwezesha chama hicho kubaini udhaifu uliopo katika utekelezaji wa wajibu wake kwa umma, tofauti na sasa ambapo hakuna mfumo unaowawezesha ufuatiliaji huo.

Nape alisema kuwa hivi sasa wanafanya mabadiliko katika mfumo wa uongozi katika makao makuu ya chama hicho na ndiyo maana hakuna mawaziri katika safu za juu za uongozi.

"Hivi sasa hakuna mawaziri, kwani wakati ule walikuwepo mawaziri katika chama ambao ni viongozi, sasa tupo wenyewe na tunakiendesha chama,"alisema na kuongeza:"Hata mfumo wa ndani katika kitengo changu cha Itikadi na Uenezi nako tunafanya mabadiliko na taarifa zitakuwa zikitolewa in details(kwa undani) na si kwa ufupi ili wananchi wazipate."

Kauli yake kuhusu watuhumiwa ufisadi
Kuhusu watuhumiwa wa ufisadi na siku 90 walizopewa kujiondoa kwenye nyadhifa wanazoshikilia ndani ya chama, Nape alisema kuwa hakuna suala la siku 90 bali ni vikao vya chama vitakutana na kutoa maamuzi.

"Siku 90 zinazozungumzwa ni tafsiri ya watu pale mwenyekiti wa chama (Jakaya Kikwete) aliposema tutakutana baada ya miezi mitatu na watu wakatafsiri hivyo, lakini vikao vya NEC ndivyo vinatoa maamuzi,"alisema Nape.

Alisema kuwa hadi hivi sasa hajui makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alichozungumza na watuhumiwa hao wa ufisadi baada ya kukutana nao.

"Sikuwepo kwenye kikao hivyo hadi sasa sijui walizungumza nini, na siwezi kwenda kumtaka Katibu Mkuu anieleze kilichozungumzwa kwani katika vikao vijavyo tutapata taarifa,"alisema Nape.

CCM na vijana
Nape ambaye alizungumzia mambo mbalimbali ya chama na Serikali alisema kuwa hali ya CCM kuwasahau vijana iliwaletea matatizo katika Uchaguzi Mkuu uliopita na ndiyo maana hivi sasa chama hicho kimeamua kujivua gamba.

Aliwaasa vijana walioko vyuoni kwa sasa akisema kuwa siyo vizuri kwao kudhani kuwa siasa ni ajira na kwamba endapo kila mwanafunzi atafikiria hivyo, hali hiyo haitawasaidia kitu.

Kuhusu takwimu za Serikali na ndani ya CCM, Nape alisema kuwa kuna ugonjwa mkubwa katika utoaji takwimu kwa kuwa takwimu nyingi zimekuwa ni za uongo.

“Udanganyifu wa takwimu unakuwa kama ni tabia na ipo kwenye chama na kwa Serikali,”alisema.

Alisema katika kila jimbo takwimu zao zinaonyesha asilimia 70 hadi 80 ya watu ni wanaCCM, lakini inashangaza kwa nini wanapata ushindi wa chini kwenye uchaguzi.

Wananchi wana haki ya kupata habari
Alisema kuwa atakuwa tayari kuwasaidia wanahabari kupata taarifa za serikalini ambazo zinakaliwa na maafisa habari au watu wa serikalini kwa kuwa wananchi wana haki ya kupata taarifa kuhusu Serikali yao.

“Kama kuna taarifa mnaihitaji serikalini nitawasaidia kuipata ili watu wapate habari kwa kuwa, Serikali ni ya CCM na sisi ndiyo viongozi wa chama,”alisema Nape.

Kuhusu kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, Nape alisema kuwa ni vizuri wananchi na wanasiasa wakalinda historia ya taifa kwa kuwa limetoka mbali tangu Uhuru ulipotikana.

“Ombi langu kwa wananchi ni hili, miaka 50 ya Uhuru ni safari ndefu, nataka dhana ya kwamba hakijafanyika chochote iondoke, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzia jengo la Ushirika na leo kipo eneo lake halafu mtu anabeza, hilo haiwezekani,”alisema.

Alisema kuwa pamoja na vyombo vya habari kufichua maovu ndani ya nchi, lakini ni lazima vilinde historia ya nchi tangu ilipopata Uhuru.

Akingia kifua gazeti la Mwananchi

Akizungumzia hali ya CCM na Serikali dhidi ya gazeti hili , Nape alisema kuwa fikra ya kwamba chama chake kinaliona gazeti la Mwananchi kama lina mlengo wa chama kingine haipo na ifutike.

“Nimekuja kwa mambo matatu, kufahamiana, kufuta dhana ya CCM kulalamikia magazeti na kutoa msimamo wa chama kuondoa dhana kwamba Mwananchi ina mlengo wa chama kimoja cha siasa,”alisema.

Alisema kuwa ni muhumu CCM ikatambua kuwa gazeti la Mwananchi ni wadau wa mabadiliko katika jamii, hivyo mstari uliopo kati ya CCM na Mwananchi ufutwe.

“CCM kama taasisi tunajua Mwananchi inaaminika na ina wasomaji wengi kuliko gazeti jingine nchini, pia tunajua linaaminiwa na watu na chama pia,” alisema Nape.

Akizungumza kuhusu hilo, Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya MCL, Theophil Makunga alisema kuwa Mwananchi kama gazeti lina sera zake na moja ya sera hizo ni kutoegemea upande mmoja.

Alisema kuwa maamuzi ya habari gani inayofaa kuchapwa kwenye magazeti ya MCL hayafanywi na mtu mmoja bali hupitia vikao vya wahariri vinavyofanyika mara mbili kwa siku.

“Hata editorial (tahariri) haifanywi na mtu mmoja ni uamuzi wa wahariri,”alisema Makunga.

Maalimu Seif ataka CCM kuchukua uamuzi mgumu






Raymond Kaminyoge
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, amesema CCM, inapaswa kuchukua uamuzi mgumu katika kupambana na rushwa ndani ya chama hicho.Amesema uamuzi huo upaswa kuchukuliwa mapema kabla madhara makubwa hayajajitokeza.

Maalim Seif alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha 'Je Tutafika' kinachorushwa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten.

Alisema CCM imefikia mahali kwamba kama mwanachama hana fedha hawezi kuchaguliwa katika nafasi za uongozi,hata kama mtu huyo anakubalika na wananchi wanaomzunguka.

"Uamuzi mzito unapaswa kuchukuliwa ndani ya chama hicho ili kurudisha maadili ya zamani ya sitatoa wala kupokea rushwa,"alisema Hamad ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar wakati wa chama kimoja cha CCM.

Alisema "uamuzi wa kujivua gamba nadhani unatafsiriwa vibaya, lakini maana yake ni kujirekebisha na kurudi katika maadili ya zamani. Lakini kujivua gamba kusichelewe, ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni."

Maalim Seif alisifu utendaji kazi wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere ambaye hakuchelewe kumshughulikia mtu aliyejihusisha na vitendo vya rushwa.

"Mwalimu alikuwa na vyanzo vingi vya kujipatia taarifa, hakutegemea vyombo vya serikali pekee, aliwatumia watu wa kawaida hata kwenye mchezo wa bao ili kumpa taarifa hivyo aliwashughulikia wapenda rushwa na hakufanya hivyo kwa kuwaonea,"alisema Hamad.

Alisema ubaya wa rais kutegemea vyombo vya serikali kumpa taarifa ni kwamba vyombo vingi humpa taarifa hata kama ni za uongo ili kumfurahisha.

Maalim Seif alisema ushahidi wa vitendo vya rushwa ndani ya chama hicho ni namna viongozi wengi walivyokamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mwaka jana katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

"Hali ile ilionyesha kwamba hali si shwari ndani ya CCM, maadili waliyojiwekea wenyewe sasa hawayafuati... uamuzi mgumu na wa haraka unatakiwa kuchukuliwa ndani ya chama hicho,"alisema Hamad.


Viongozi wa upinzani Makamu huyo wa rais, amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kukosoa bila kutumia lugha zinazoweza kuchochea vurugu nchini.

Alisema wafuasi wa vyama vya upinzani wako tayari kufanya vurugu ikiwa viongozi wao wataruhusu kufanya hivyo.

"Tukosoane kwa kutumia maneno ya kistaarabu ili kuepusha vurugu ili amani iliyodumu kwa muda mrefu iendelee kuwepo na kufurahiwa, Tanzania ni yetu sote,"alisema Hamad.

Maandamano
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Hamad alisema ni kosa kwa polisi kuzuia maandamano bila kutoa sababu za msingi."Maandamano ni haki ya vyama vya siasa,polisi wanajulishwa ili kutoa ulinzi, lakini polisi wanapokataza maandamano bila ya kuwa na sababu za msingi ni kutofahamu haki za wananchi,"alisema.


Pia alisema vyama vyenye wafuasi wengi ambao wanajaa kwenye maandamano na mikutano ya hadhara iwe changamoto kwa chama tawala kujitathimini kwa nini hali hiyo inajitokeza hivi sasa.

Zanzibar yawakaribisha diaspora

NaSalma Said
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini
ZANZIBAR YAKARIBISHA DIASPORA
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefunguwa milango wazi kwa Wazanzibar waliopo nje ya nchi kuja nchini na kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa nchi na kuleta maendeleo zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2011-2012 hapo katika baraza la wawakilishi.
Dk Mwinyihaji alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambuwa mchango mkubwa wa wananchi hao katika kusaidia na kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo imeanzisha idara ya kuratibu maendeleo ya wazanzibari walipo nje inayojulikana kwa jina la Diaspora.
Alisema Idara ya Ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa shughuli za Wazanzibari waliopo nchi za nje (DIASPORA) tayari imeandaliwa mipango ya kuwashirikisha wataalamu mbali mbali katika mikutano ya kikanda ikiwemo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mjadala wa soko la sarafu.
Aidha Idara hiyo pia imeanza utaratibu wa kukutana na wazanzibari walionje ya nchi ikiwemo Uingereza na kuwataka kuwa tayari kushirikiana na serikali ya Zanzibar kwa kutoa michango yao baada ya kuandaliwa kwa mpango na sera inayowashirikisha na serikali yao.
Dk Mwinyihaji alisema mazingira ya kisiasa yaliopo sasa ni mazuri,ambapo Zanzibar ipo chini ya mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa iliyowashiriikisha wanan chi wote kufanya kazi.
Aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba serikali tayari imeanza kufanya mawasiliano na wazanzibari waliopo nje kuja na kushirikiana na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nchi.
Alisema mafanikio hayo yameanza kuzaa matunda ambapo wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kushirikiana na umoja wa wazanzibari waliopo Uingereza kufanya mkutano mkubwa ambao ulikuwa na lengo la kuwakutanisha na kutambuwa Mchango wa Watanzania walio nje ya nchi.
“Mkutano ule ulikuwa na manufaa makubwa ambapo ulihudhuriwa na waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe…..watendaji wetu kutoka SMZ walihudhuria na mambo mengi yalizungumzwa kwa faida ya Zanzibar ikiwemo kuitangaza Zanzibar”alisema Mwinyihaji.
Alisema tangu kufanyika kwa mkutano huo yamekuwepo mafanikio makubwa kwa baadhi ya wananchi wazanzibari waliopo nje kuonesha nia ya kuja nchini na wengine kusaidia shunguli mbali mbali za ujenzi wa taifa.
Mwinyihaji aliliambiya baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashirikishwa kikamilifu katika mikutano mbali mbali ya kimataifa na kanda ikiwemo taasisi za kimataifa.
Kwa mfano Mwinyihaji alisema kwamba Zanzibar itanufaika kwa kiasi kikubwa kufuatia kuanzishwa kwa eneo huru la biashara la utatu COMESA pamoja na Jumuiya ya Afrika ya mashariki pamoja na SADC.
Alisema eneo la soko hilo ni muhimu sana likiwa na nchi wanachama zipatazo 26 likiwa na idadi ya watu Milioni 600 na wastani wa pato la taifa linalofikiya dola za kimarekani Trilioni moja.
Mwinyihaji alisema kuanzishwa kwa soko huru la utatu utakuza biashara na kuongeza uwekezaji katika viwanda na kukuza miundo mbinu katika nchi wanachama wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“Mheshimiwa hili eneo la biashara la utatu ni muhimu sana tukilitumia vizuri basi yapo manufaa makubwa ya kuimarika kiuchumi na biashara” alisema waziri huyo.
Aidha aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashiriki kikamilifu katika vikao vyote vya jumuiya ya Afrika ya mashariki,ambapo watendaji wake wamekuwa wakishiriki katika mikutano ya matayarisho la baraza la mawaziri na wakuu wa nchi.
Mwinyihaji aliliomba baraza la wawakilishi kuidhinisha jumla ya sh.33,127,.2 Milioni ambapo kati ya hizo jumla ya sh.29,386.2 kwa ajili ya kazi za kawaida na jumla ya sh.1,930.0 kwa kazi za maendeleo katika mwaka 2011-2012.
ZIARA ZA MAALIM SEIF ZIMELETA TIJA
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo iliwasilishwa juzi Barazani hapo na waziri wa Wizara hiyo Fatma Abdul-habib Ferej huku akitetea ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais nje ya nchi kwamba zilikuwa na maslahi na faida kubwa kwa maendeleo ya nchi.
Bajeti hiyo ilipitishwa baada ya wajumbe wote wa baraza hilo kuridhishwa na ufafanuzi wa hoja na masuali yao waliyouliza wakati wakijadili ambapo alitaja ziara za Makamu wa Kwanza faida zake ni nyingi ikiwemo ile ziara ya nchi za Mashariki ya Kati alipokutana na wafanyabishara na wawekezaji ambao baadhi yao wameonyesha nia ya kushirikiana na Zanzibar katika uwekezaji kufungua mahusiano kati ya Zanzibar na nchi hizo.
Katika ziara ya nchi za kiarabu ikiwemo Oman Waziri huyo alisema Makamu wa kwanza katika ziara yake hiyo imefungua milango kwa kurejesha mahusiano mema kwa kuwa Zanzibar na Oman ni marafiki na ndugu wa muda mrefu ambapo katika mazungumzo hayo yameweza kurejesha upya safari zake kati ya Oman na Zanzibar, mazungumzo ya kuanzisha shirika jipya la ndege la Zanzibar na msaada wa uchimbaji mafuta.
Wakati wakichangia hutuba ya bajeti ya ofisi ya makamu wa kwanza wa rais baadhi ya wawakilishi walitaka kujua mafanikio yaliopatikana katika ziara za makamu wa kwanza wa rais kwa kuwa kitabu cha hutuba hakijaeleza mafanikio yoyote yaliopatikana katika ziara hizo.
Aidha waziri huyo alisema mbali ya faida hizo, pia yalifanyika mazungumzo ya kuomba msaada wa ujenzi wa Bandari mpya na kudumisha uhusiano mwema baina ya Zanzibar na nchi za eneo hilo.
Akizungumzia suala la madawa ya kulevya ambalo limechukua muda mrefu kujadiliwa na wajumbe na kuitaka serikali kujikita katika suala hilo kwa kuweka mkazo mahsusi kwa lengo la kuwanusuru vijana Waziri huyo alisema anakubaliana na maoni ya wajumbe na kuahidi kwmaba serikali itaendelea na juhudi zake na kupambana na tatizo hilo kwa kushirikiana na vyombo husika na wananchi.
Kuhusu maambukizi ya vizuri ya ukimwi Ferej alisema Zanzibar kwa akiasi fulani imefanikiwa kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kueleza huku akijibu hoja za wajumbe ambao wamehji mfuko huo kutengewa fedha nyingi alisema ni kutokana na umuhimu wa kazi hiyo kubwa na kupambana na ukimwi.
Alisema Ofisi ya makamu wa kwanza wa rais ipo kwenye mikakati ya kuangalia mapungufu ya sheria ili kuweza kuzuia uingiaji wa dawa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiathiri vijana wengi na hatimae kupata maambukizi ya vizuri vya ukimwi.
Kuhusu uharibifu wa maliasili zisizorekebishwa alilifahamisha baraza hilo kuwa Ofisi yake ipo hatua za mwisho kuweka kanunui ambazo zitasaidia kuzilinda na kuzififadhi kwa manufaa ya vizazi vilivypo na vijavyo.
Alisema Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya tabia nchi, ikiwemo mashamba kuingia maji ya bahari, maji kuingia chumvi na hata baadhi ya maeneo kumengwa na bahari na kubainisha kuwa ofisi inaandaa mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakichangia bajeti ya Ofisi hiyo wajumbe hao wajumbe wa Baraza hilo waliomba nyumba za Sober House ambazo zimekuwa zikiwahifadhi vijana walioacha matumizi ya dawa za kulevya kujengwa mbali ya nyuma za makaazi ya watu.
Aidha alizungumzia suala zima la sekta ya utalii ambapo alisema zinapaswa kuwa na mikakati ya madhubuyi ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ukimwi, pamoja na kuongeza kasi ya mapambano hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar imekuwa na uingiaji na utokaji mkubwa wa watu kutoka sehemu mbali mbali.
DK CHEIN KUONGEA KILA MWEZI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ataanza kuwasiliana na waananchi kupitia vyombo vya habari kila baada ya miezi mitatu imeelezwa.
Hayo yameelezwa waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, wakati akisoma bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ndani ukumbi wa Baraza la wawakilishi uliopo Chukwani Mjini Zanzibar.
Alisema Utaratibu huo una dhamira ya kukuza mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao na waandishi wa habari watatakiwa kuuliza maswali mbali mbali yatakayotolewa ufafanuzi ili wananchi wapate kujua masuala yanayoendelea katika serikali yao.
Lengo la kutekelezwa kwa mpango huo moja ni kuwasiliana na wananchi moja kwa moja lakini pia kuweka twaasira nzuri baina ya Rais na wananchi wake na washirika wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia Zanzibar katika masuala mbali mbali.
Alisema katika mazungumzo hayo na vyombo vya habari yatalenga zaidi masuala yanayohusu Zanzibar na maendeleo yake kwa kuwaelezea wananchi yale yalioahidiwa na serikali kuyatekeleza katika awamu hii ya saba.
Waziri huyo alisema kuwa utaratibu huo utapoanza kutumika utaweza kukuza mawasiliano ya umma kama kiungo kati ya rais na wananchi wake ambapo wizara hiyo imeamua kuutumia baada ya kuimarisha taasisi ya mawasiliano Ikulu.
Hatua ya serikali kuanzisha utaratibu wa rais kuzungumza na vyombo vya habari umeitikiwa kwa furaha na wajumbe wa baraza la wawakilishi wkatai wakichangia bajeti hiyo ambapo wamesema ni hatua nzuri ambayo itatoa fursa ya wananchi kufahamu yanayofanyika kwa serikali yao.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu alisema wananchi wengi wamekuwa na malalamiko juu ya serikali yao kutokana na ukimya wa taarifa juu ya mambo muhimu yanayotendea ndani ya serikali yakiwemo yake ya mafanikio.
Alisema katika kipindi kifupi cha serikali ya umoja wa kitaifa kmekuwepo na mafanikio makubwa ambayo wananchi walipaswa kuyafahamu lakini kutokana na kutokuwepo taarifa sahihi kwa wananchi imesababisha wananchi hao kulalamikia sana serikali yao jambo ambalo alisema linapaswa kuwekwa wazi ili wajue nini serikali yao inawafanyia kwa lengo la kukuza demokrasia na maendeleo ya nchi yao.
“Ni utaratibu mzuri ulioanzishwa kwamba mheshimiwa rais atakuwa na mazungumzo na waandishi wa habari kila baada ya miezi mitatu….yapo mambo mengi ambayo amefanyika tokea kuanza mfumo mya wa serikali ya umoja wa kitaifa lakini wananchi haafahamu kwa kuwa hayaelezwi sasa kwa utaratibu huu itasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi” alisema Jussa.
WAZANZIBARI WATANO NI MABALOZI
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba ni Wazanzibar watano tu ambao wana hadhi ya kuwa mabalozi kamili wanayoiwakisha Tanzania nje ya nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed aliliambiya baraza la wawakilishi. Kati ya Wazanzibari hao wawili tayari wamestaafu kazi akiwemo aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia balozi Ali Karume.
Aboud alisema hayo wakati alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa ni wazanzibari wangapi ambao ni mabalozi kamili wanayoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na vigezo gani vinavyotumika katika kuwachaguwa.
Akifafanua zaidi Aboud aliwataja mabalozi hao kuwa ni Balozi Mohamed Mwinyi Mzale ambaye anaiwakilisha Tanzania huko Sweden, balozi Ali Shauri anayeiwakilisha Tanzania Misri,balozi Omar Ramadhan Mapuri aliyeko China pamoja na Ali Karume aliyekuwa Italia na Hussein Said Khatib huko Oman ambao tayari wamestaafu kazi.
Alifafanua na kusema kwamba vigezo vya mtu kuwa balozi kamili anayeiwakilisha Tanzania ni kufuata ngazi mbali mbali ambazo zipo katika wizara ya mambo ya nchi za nje ikiwemo vyeo na elimu.
Aidha alisema uamuzi wa kuteuliwa kuwa balozi unatokana na rais wa nchi ambapo akiamuwa kumteuwa mtu kuwa balozi basi anakuwa balozi na kumtangaza.
Aboud alisema Zanzibar haina sifa kuwa na ofisi kamili za ubalozi wa nchi za nje ziliopo Tanzania ambapo kwa mujibu wa sheria za kibalozi,makao makuu ya nchi ndiyo huwepo ofisi za kibalozi.
Kwa sasa Zanzibar zipo ofisi ndogo za ubalozi wa nchi za nje ikiwemo ubalozi wa China.India pamoja na ubalozi wa Misri,Oman pamoja na Msumbiji na nchi za Skandinavia. Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa ni miongoni mwa mambo yaliomo katika orodha ya mambo ya muungano ya asili.
FEDHA ZA WAJASIRIRIAMALI TAYARI
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema tangu kuanzishwa kwa mfuko wa kusaidia wajasiriamali unaojulikana kwa jina la AK pamoja na JK jumla ya sh.1,463,640,000 zimetumika kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali mbali mbali Unguja na Pemba.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman wakati akijibu swali aliloulizwa na mwakilishi wa jimbo la Matemwe (CCM) Abdi Mosi Kombo aliyetaka kujuwa wananchi wa kipato cha chini wamefaidika vipi na mifuko hiyo.
Haroun alisema jumla ya sh.Bilioni mbili zimebakia zikiwa zinawasubiri wajasiriamali kwa ajili ya kukopeshwa na kuanza kufanya miradi mbali mbali ya maendeleo na kukuza uchumi.
‘Mheshimiwa spika mfuko wa JK na AK kwa sasa upo katika harakati za kuwapatia elimu ya ujasiriamali wananchi mbali mbali kwa ajili ya kupiga hatua kubwa za kiuchumi’alisema Haroun.
Aidha alisema mipango imo mbioni kuona kwamba unaanzishwa mfuko wa AS ambao ni wa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk.Ali Mohamed Sheni.
‘Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanzisha mfuko wa AS ambao ni wa rais wa Zanzibar dk.Ali Mohamed Sheni’alisema Haroun.
Alisema suala la kuwapatia elimu ni muhimu sana kwa wajasiriamali ambao watapewa mikopo hiyo ni ili kuweza kujuwa kama wakipata fedha hizo watazitumia kwa njia gani.
Alikiri mikopo iliyopita ambayo walipewa wajasiriamali mbali mbali Unguja na Pemba marejesho yake yalikuwa na matatizo hali ambayo ilipelekea benki kusitisha utoaji wa mikopo hiyo.
Haroun aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba wananchi katika majimbo ya uchaguzi wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuibuwa miradi mbali mbali ambayo wataifanyia kazi wakati watakapopewa fedha hizo.
Alisema lengo la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lengo lake kubwa ni kuona kwamba wananchi wake wakiwemo wajasiriamali wanajikomboa na umasikini wa kipato.
ZIARA ZA SHEIN ZALETA MATUNDA
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba ziara zilizofanywa na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Sheni zimeanza kuleta matunda ikiwemo ile ya Uturuki.
Hayo yalisemwa na waziri wa nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
Dk Mwinyihaji alisema rais Shein alifanya ziara ya kiserikali nchini Uturuki mwaliko wa mwenyeji wake rais wa Uturuki Abdull Gul ambapo nchi hiyo imeahidi kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo utalii, uwekezaji pamoja na sekta ya afya.
Alisema katika sekta ya afya, Uturuki kupitia wataalamu wake wanatazamiwa kufanya ziara kuja Zanzibar na kuangalia maeneo ya kuisaidia Zanzibar.
Aidha alisema Uturuki itaipatia Zanzibar nafasi za masomo kwa vijana mbali mbali wa Zanzibar katika sekta ya afya, ikiwemo kuipatia madawa,madaktari pamoja na wataalamu wa maradhi ya moyo.
Katika sekta ya utalii, serikali ya Uturuki imeonesha kuisaidia Zanzibar katika maendeleo ya sekta ya utalii na kuifanya sekta hiyo kusaidia kuingiza mapato ya nchi.
Katika mikakati hiyo, Uturuki inakusudia kuimarisha Chuo cha Utalii kiliopo Maruhubi kwa ajili ya kukipa nyenzo mbali mbali ili kuweza kutoa mafunzo zaidi kwa wanafunzi wanaosoma hapo.
Aidha alisema mazungumzo yameanza kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Uturuki kuanzisha safari za shirika la ndege moja kwa moja kuja Zanzibar.
Hatua hiyo Mwinyihaji alisema kwamba itasaidia sana kuinuwa sekta ya utalii kwani Zanzibar itakuwa ikipokea watalii moja kwa moja kutoka nchi mbali mbali za bara la Ulaya na Asia na hivyo kufanikiwa kulifia soko la Asia.
Katika hatua hizo hizo za kuimarisha sekta ya utalii, Uturuki imekubali kulifanyia ukarabati mkubwa jengo la kihistoria la Beit-el-Jaib liliopo eneo la mji mkongwe kwa ajili ya kuimarisha haiba yake ambayo ni moja ya kivutio kikubwa cha sekta ya utalii na historia.
Katika sekta ya elimu, Mwinyihaji alisema kwamba Uturuki imeonesha nia nzuri ya kuipiga jeki sekta ya elimu ambapo mashirikiano yameanzishwa kati ya Chuo kikuu cha Zanzibar SUZA pamoja na Vyuo vikuu vya Istambul na Ankara Uturuki.
Katika sekta ya kilimo, serikali ya Uturuki imekubali kukisaidia na kukipa uwezo Chuo cha Kilimo kilipo Kizimbani kwa ajili ya kuimarisha huduma za wanafunzi.
Alisema Chuo hicho kitapewa uwezo wa kufanya tafiti mbali mbali za kitaalamu ambazo zitasaidia kuwafanya wakulima kupiga hatua kubwa ya kuzalisha mazao mengi.
“Mheshimiwa kwa ujumla ziara ya rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Sheni nchini Uturuki imekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbali mbali kwa maslahi ya wananchi wa visiwa hivi” alisema.

Watendaji wapongezwa

Na Salma Said
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika mkutano wake na Wakurugnzi na Watendaji wakuu wa Ofisi yake kuhusu mafanikio ya utayarishaji wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Watendaji Wakuu na Wafanyakazi wa Ofisi yake kwa kazi nzuri walioifanya kwa ushirikiano na kupelekea kupitishwa Bajeti yake kwa mafanikio makubwa.
Mheshimiwa Makamu huyo wa Pili wa Rais aliyaeleza hayo katika mkutano wake na Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Ofisi yake uliofanyika ofisini kwake Vuga.
Alisisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano wao katika kazi zote za utekelezaji za kila siku na wasiishie kwenye maandalizi ya Bajeti pekee bali waongeze bidii hata katika kazi nyengine.
Akizungumzia Semina Elekezi ya Viongozi wa Maidara na Watendaji Wakuu wa Serikali iliyomalizika hivi karibuni, Mhe Balozi Iddi alisema lengo kuu ni kuwataka wabadilike katika usimamizi wao kwa wanaowaongoza ili wafanyakazi nao wawajibike ipasavyo katika sehemu zao za kazi.
Alieleza kuwa baadhi ya viongozi wana matatizo katika usimamizi kwa hofu ya kuambiwa wanyapara, lakini alisema kusimamia vyema kazi ili watu wafuate taratibu za kazi kwa nidhamu iliyowekwa sio unyapara.
Hivyo alihimiza suala la kufika kazini kwa wakati na kubaki makazini hadi muda wa kazi uliyowekwa unapoisha.
“Hatukatai watu kuwa na dharura kama kwenda Benki, Hospitali na kadhalika lakini wakishamaliza shughuli zao wrejee kukamilisha muda wao kazini ndio nidhamu ya kazi”, alisema Balozi Iddi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud alimshukuru Mhe Balozi Iddi kwa mapenzi yake kwa wafanyakazi na ushirikiano mkubwa anaoutoa katika kuendesha Ofisi yake na ndio siri ya mafanikio hayo.
Akitoa shukrani kwaniaba wafanyakazi wa Ofisi hiyo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dr. Khalid Salum Mohd aliahidi kuendelea kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi.

KIKAO CHA BAJETI KIKIPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NCHI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Ferej akisoma majumuisho ya michango ya Wajumbe waliochangia
WAJUMBE Baraza la Wawakilishi wakiwa katika chumba cha Mkutano wakipitisha Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais jana.
MWAKILISHI wa Magomeni Salimin Awadh akitaka maelezo ya matumizi ya komoja ya Vifungu vya bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wakati wa kupitisha vifungu vya Wizara hiyo jana.
MWAKILISHI wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akitaka ufafanuzi wa kimoja cha kifungu cha Wazari hiyo wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Hija Hassan Hija( KIWANI) akitaka ufafanuzi wa kifungu cha bajeti wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Mamamu wa Kwanza wa Rais
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi akisikiliza hoja za Wajumbe katika kupitisha vifungu vya bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. 
Moto wawaka bungeni
                
MDEE, MACHALI WATIKISA KITI CHA SPIKA, WENJE ADAI NCHI IMEJAA WEZI
Kizitto Noya, Dodoma na Fidelis Butahe,Dar
KITI cha Spika wa Bunge, Anne Makinda jana kilitikiswa kufuatia malumbano makali baina ya wabunge hasa wa kambi ya upinzani walipokuwa wakichangia hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu, huku mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje akidai kuwa nchi imejaa “wezi wasiokuwa na hatia”.Kidhalika kikao hicho cha bunge jana, kilishuhudia malumbano makali baina ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba, ambayo yalitanguliwa na mvutano baina ya Spika, Anne Makinda na Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali.

Mvutano uliotokea kipindi cha bunge jioni, baina ya Mdee na Mabumba ulikwenda mbali kiasi kwamba Mdee alitoa matamshi makali kwa mwenyekiti huyo wa bunge akimwambia “….mwenyekiti ukiendesha mjadala huu kwa ushabiki, kiti kitakushinda”.

Malumbano hayo yalisababishwa na kauli za Mbunge wa CCM, Zarina Madabida kusema wanaopinga posho za wabunge (sitting allowance) wanataka chama chao kiwafidie fedha hizo, jambo ambalo lilisababisha Mdee, kusimama kuomba mwongozo.

Madabida alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi za Waziri Mkuu ya mwaka 2011/12 jana na bila kukitaja chama hicho alisema kama kina dhamira ya kweli ya kukataa posho hizo kwanini wabunge wake wanataka kufidiwa posho hizo na chama.

“Mwenyekiti hizi posho ni muhimu, mimi leo nikienda Dar es Salaam akinamama nakwenda kuwasaidia na hizi posho,” alisema Madabida.

Baada ya Madabida kumaliza kuchangia hotuba hiyo na kukaa chini, Mdee aliomba mwongozo wa mwenyekiti huku akitaja kanuni ya bunge inayomtaka mbunge asiseme uongo na endapo atasema jambo hilo atatakiwa alithibitishe.

Lakini kabla hajamaliza kukifafanua kifungu hicho, Mabumba alimtaka Mdee akae chini,  lakini mbunge huyo kabla ya kukaa alisita kwa sekunde kadhaa kutii amri hiyo.

Mabumba alimweleza Mdee kwamba Madabida wakati akizungumza hakutaja chama chochote na endapo angekitaja chama hicho ndio angetakiwa kuthibitisha.

Baada ya ufafanuzi huo, Mdee alinyanyuka na kusema kwamba chama kinachopinga posho ni  Chadema na NCCR-Mageuzi.

“Kwa implication, Mheshimiwa Madabida alikuwa anavilenga vyama hivi… Mwenyekiti usikikalie kiti kwa ushabiki, kitakushinda,” alisema Mdee.

Hata  hivyo kabla hajaketi, ilisikika sauti ndani ya bunge ikisema “Jumamosi mligombea posho’’ hatua iliyomfanya Mdee kumtaka mwenyekiti huyo wa bunge kumlinda.

Pamoja na ombi hilo la Mdee, Mabumba hakuzungumza lolote juu ya hali hiyo badala yake alimtaka mbunge huyo kukaa chini huku akiwaita wachangiaji wengine wachangie hotuba hiyo ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu.

Machali na Spika
Mvutano baina ya Machali na Spika Makinda, ulitokea katika kipindi cha asubuhi, kufuatia mbunge huyo wa Kasulu Mjini kudai kuwa “…kuna mambo yanafanyika kihuni ndani ya serikali”.

Machali alisema mwaka uliopita zilitengwa zaidi ya Sh6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidawe-Kasulu kwa kiwango cha lami lakini, fedha hizo hazijawahi kutolewa na kwamba hata katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi 2011/12 fedha hizo hazijatengwa.

“Kuendelea kuwaahidi wananchi wakati jambo lenyewe halijafanyika ni uhuni wa serikali.., inawafanyia uhuni watu wa Kigoma,”alisema Machali.

Kauli hiyo ilimfanya Spika Makinda kumtaka mbunge huyo kutumia lugha nzuri katika utoaji wa mchango wake na kuacha kutumia neno ‘uhuni’.

“Barabara inaanza kujengewa Nyakanazi.., Nyakanazi sio Kigoma. Hivi Kigoma tumewakosea nini, Rais Kikwete alisema barabara itajengwa, lakini leo mmezihamisha fedha hizo sehemu nyingine, kama sio uhuni ni nini,”alihoji Machali.

Kitendo cha Machali kurudia neno hilo kilimfanya Spika Makinda kumwonya tena mbunge huyo na kumweleza kuwa akitumia neno ‘uhuni’  anaweza asisikilizwe na anaowapelekea ujumbe huo.

Lakini Machali alionekana kutokubaliana na Spika kwa kujibu kuwa, “Hata Shelukindo alitumia neno ‘kijingajinga’ na alikuwa akitulenga sisi wapinzani, sasa sisi wapinzani tukitumia maneno ya ukali tutahukumiwa,  spika tuwe na 'check and balance' (kuangalia usawa)”.

Machali alikuwa akifanya marejeo ya mchango wa Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo (CCM), ambaye wakati akichangia alisema kumekuwa na wabunge wanaoingiza hoja za kijingajinga bungeni.

Machali aliweka wazi kwamba wabunge ni kama wamejivua uwakilishi wa wananchi kwani wamekuwa mbogo dhidi ya hoja ya kufutwa kwa posho za vikao.

Mbunge huyo alisema maendeleo ya Tanzania hayalingani na umri wa miaka 50 ya Uhuru wake na kwamba wananchi wa Tanzania hawana amani, bali wana utulivu ulioambatana na nidhamu ya woga.

“Siwezi kukubali kuwa kuna amani, wakati watu wanawaza watapata wapi mlo, polisi wanaendeleza vitendo vya kuwapiga raia kama wakimbizi ndani ya nchi yao, Serikali inakaa kimya na kusema mamlaka husika ziachwe zifanye kazi yake,”alisema Machali.

Kauli ya Wenje
Naye Wenje aliungana na Machali akisema kuwa Tanzania haina amani bali wananchi wake wana nidhamu ya woga akihoji kwamba maana ya amani ni mtu kutangazwa kuwa ameshinda ubunge baada ya vurugu polisi kupiga mabomu ya machozi?.

“Hapa mtu akieleza ukweli au watu wakiandamana wataelezwa kuwa wanataka kuchafua amani, hii si kweli,”alisema Wenje na kuongeza:
“….. tutaandamana kwa sababu, maandamano ni lugha ya sauti  isiyosikika na hata kesho tutaandamana tu,”.

Alisema kuwa baadhi ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonyesha kwa baadhi ya Halmashauri nchini zina hati chafu, lakini serikali haielezi wakurugenzi katika Halmashauri hizo wamechukuliwa hatua gani.

“Mimi nilitegemea Mkuchika (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI) wakati akisoma makadirio na matumizi ya ofisi yake atasema wakurugenzi hawa amewafuta kazi, nchi ina matatizo mnasema ina amani, amani ipi sasa,” alisema Wenje.

Wenje ambaye ni mbunge wa Nyamagana alisema nchi imejaa wezi na inaendelea kuporwa lakini,  serikali haionyeshi nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika. “Nchi imejaa innocent thieves (wezi wasio na hatia), lakini serikali haijali.

Mimi nilitegetemea wakati Waziri (Tamisemi) aliposema kuna halmashauri nne zimepata hati chafu, nilitegema asema tayari wakurugenzi wake tumewafukuza na zingine zenye kasoro, wakurugenzi wako under probation (chini ya uangalizi) na wakirudia hivyo miaka miwili waondoke. We must sack them!”alisisitiza.

Aliendelea,”ATCL is almost dead due to poor management, (imekufa kwa sababu ya uongozi mbovu). Nchi iko looted (imeporwa). Tulikuwa na Deepgreen Finance na sasa tuna issue (suala) la rada. Kwa nini hatuchukui hatua?”alihoji.

Wenje aliitaka serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika, akibainisha kuwa kuendelea kuwalea mafisadi na watu wasiowajibika, ni tatizo ambalo siku moja, litagharimu amani ya nchi.
Katika hatua nyingine mbunge huyo aliendeleza madai ya chama chake kutaka posho ifutwe akisema “kwenye suala la posho za vikao (Sitting allowance) haturudi nyuma, na as from tomorrow (kuanzia kesho), tunaomba mtuletee fomu mbili ili sisi (Chadema) tusisaini fomu ya posho hizo.”

Watanzania ndani ya Chupa
Mapema, Shellukindo aliwagutua wabunge pale aliposema Watanzania ni kama wako kwenye chupa hivyo kutofahamu chochote kinachoendelea katika nchi nyingine.

Shelukindo alisema, “ Ukiwachukua panzi ukawatumbukiza ndani ya chupa wataruka na kukosa chakula na baadaye wataanza kuumana, Tanzania tuko ndani ya chupa, nchi ina kila kitu, lakini Watanzania bado masikini, tumebaki kufanya siasa za kuchafuana.”

Alisema misaada mingi inayotolewa haiwafikii walengwa lakini, wabunge wamebaki kujadili hoja sizizo za msingi bungeni.

“Ajira kwa vijana hakuna, ndio maana wakiambiwa waandamane wanakubali,  ukabila, udini, mauaji ya albino. Jamani Watanzania tumefungwa, tupo ndani ya  chupa tumefungwa,” aliongeza.

Alisema Watanzania ili watoke ndani ya chupa, kila mtu anapaswa kutekeleza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kumwomba Mungu, huku akitolea mfano nchi ya Rwanda ambayo ilikuwa katika vita, lakini kwa sasa imepiga hatua kimaendeleo.

Naye Mbunge wa Lindi Mjini Salum Barwany, alipendekeza serikali kuanzisha mjadala wa kitaifa ili watu wajadili matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa serikali, inaonekana kushindwa.

Alisema serikali imeshindwa kutekeleza ahadi za rais anazozitoa maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Lindi mjini na hili linawafanywa wananchi wakose imani naye na serikali yake.

Barwany ambaye alikuwa akizungumza kwa hisia kali bungeni, alisema kuwa kitendo cha serikali kutotekeleza ahadi hizo za rais ni kumdharau rais mwenyewe ambaye maagizo yake, ni zaidi ya sheria.

“Kauli ya rais ni ya thamani kuliko hata sheria. Sasa rais kaja Lindi na akatuahidi soko kuu bandari, maji, uwanja wa ndege wa Kimataifa, mashamba ya mkonge na mambo mengine kibao, lakini mpaka leo anapobakiza miaka mitatu, hakuna kinachofanyika,”alisema Barwany.

Alihoji “Ahadi za rais ziko wapi Lindi leo? Kama nyie serikali mnamdharau rais wananchi watafanya nini? Leo manung’uniko kila kona. Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa na sio mipango isiyotekelezeka ya Kilimo Kwanza, ili watu wajadili namna ya kutatua matatizo yao.”