Watendaji wapongezwa
Na Salma SaidMheshimiwa Makamu huyo wa Pili wa Rais aliyaeleza hayo katika mkutano wake na Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Ofisi yake uliofanyika ofisini kwake Vuga.
Alisisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano wao katika kazi zote za utekelezaji za kila siku na wasiishie kwenye maandalizi ya Bajeti pekee bali waongeze bidii hata katika kazi nyengine.
Akizungumzia Semina Elekezi ya Viongozi wa Maidara na Watendaji Wakuu wa Serikali iliyomalizika hivi karibuni, Mhe Balozi Iddi alisema lengo kuu ni kuwataka wabadilike katika usimamizi wao kwa wanaowaongoza ili wafanyakazi nao wawajibike ipasavyo katika sehemu zao za kazi.
Alieleza kuwa baadhi ya viongozi wana matatizo katika usimamizi kwa hofu ya kuambiwa wanyapara, lakini alisema kusimamia vyema kazi ili watu wafuate taratibu za kazi kwa nidhamu iliyowekwa sio unyapara.
Hivyo alihimiza suala la kufika kazini kwa wakati na kubaki makazini hadi muda wa kazi uliyowekwa unapoisha.
“Hatukatai watu kuwa na dharura kama kwenda Benki, Hospitali na kadhalika lakini wakishamaliza shughuli zao wrejee kukamilisha muda wao kazini ndio nidhamu ya kazi”, alisema Balozi Iddi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud alimshukuru Mhe Balozi Iddi kwa mapenzi yake kwa wafanyakazi na ushirikiano mkubwa anaoutoa katika kuendesha Ofisi yake na ndio siri ya mafanikio hayo.
Akitoa shukrani kwaniaba wafanyakazi wa Ofisi hiyo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dr. Khalid Salum Mohd aliahidi kuendelea kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment