Saturday, 18 June 2011

WAZIRI JHAD HASSAN WA ZANZIBAR AKUTANA NA WAZIRIRI WA SINEMA NA TELEVISHENI WA IRAN

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Abdilah
Jhad Hassan wa mwisho kushoto akizungumza hapo jana na naibu waziri wa
Sinema na masuala ya Televion wa Iran Javad shamaq wa mwisho kulia

Zanzibar yaiomba Serikali ya Jamhuri ya Iran kubadilishana wataalamu katika fani mbali mbali

WAZIRI wa habari Utamaduni

Utalii na Michezo Abdilah Jihad Hassan
Na Mwandishi wa Idara ya Habari,Zanzibar.
WAZIRI wa habari utamaduni utalii na michezo Abdilah Jihad Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Iran kubadilishana wataalamu katika fani mbali mbali na kuwapatia mafunzo ya uandishi wa bahari waandishi wa habari wa Zanzibar.
Amasema kuna haja kubwa kwa Serikali ya Iran kubadilishana wataalamu na kuwapatia waandishi wa habari wa Zanzibar mafunzo ili waweze kuijengea uwezo taaluma yao wanayoifanyia kazi.
Waziri Jihad alisema hayo leo huko ofisini kwake Kikwajuni wakati alipokuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa sinema na masuala ya televion wa Iran Javad Shamaqdari pamoja na ujumbe wake.
Akizungumzia juu ya suala la utamaduni wa Zanzibar Waziri jihad alisema kuwa Utamaduni wa Zanzibar na Iran ni Tamaduni ambazo zimeingiliwa na Tamaduni nyengine jambo ambalo limepelekea kuharibika kwa utamaduni huo
Hata hivyo Waziri huyo wa habari wa Zanzibar alisema kuwa mipango inafanywa ili kulipatia ufumbuzi suala hilo la kuchafuliwa kwa tamaduni zetu ambazo zinalingana kati ya Jamhuri ya Iran na Zanzibar.
Aidha alisema mbali ya kulipatia ufumbuzi suala hilo pia kuna haja kubwa kwa Serikali ya Iran kushirikiana na Zanzibar katika Nyanja ya masuala ya utalii.
Naye Naibu Waziri wa Sinema na masuala ya Televion wa Jamhuri ya Iran Javad Shamaqdari amesisitiza kuwepo na mashirikiano kati ya Zanzibar na Iran katika masuala ya Utamaduni na Habari.
Alisema ipo haja kubwa kwa nchi hizi mbili kuimarisha na kudumisha mashirikiano katika Nyanja hizo ambazo zinahusiana na masuala ya Habari na Utamaduni.
Akizungumzia juu ya maoyesho, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Jamhuri ya watu wa Iran wanayo maonyesho yao ambapo hata hapa Zanzibar yapo lakini alisema kuna haja ya kuanzishwa maonyesho ya Shirazi Festival.
Akizungumzia suala la makumbushoNaibu Waziri huyo wa Iran alisema wanayo makumbusho yao lakini katika hili alishauri kuwa kwa hapa Zanzibar kuwepo na makumbusho ambayo yanaelezea kwa uwazi kwa kitu maalumu ambacho hakikupi taabu unapofika hapa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment