Marekani yaionya Syria
Marekani imeeleza wasiwasi wake juu ya taarifa kuwa Syria inapeleka vikosi vyake katika mpaka wao na Uturuki, na kuonya kuwa huenda kukawa na mapigano zaidi.
Waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton amesema hatua hio ya majeshi ya Syria "inatia wasiwasi".Anasema hali hii huenda ikasababisha kukithiri kwa mapigano kati yao na Uturuki na kuwaweka wakimbizi katika mazingira magumu zaidi.
Imeripotiwa kuwa vifaru vya kijeshi vya Syria vimeonekana vikiingia katika kijiji cha Khirbet al-Jouz,kulazimisha wakaazi kukimbia hadi nchi ya Uturuki.
Zaidi ya watu 1,300 wameuawa tangu kuanza wa makabiliano dhidi waandamanaji wanaopinga utawala wa Syria mwezi Machi.
Maelfu ya waandamanaji wamekamatwa, wanaharakati wa upinzani wanasema.
Miji mingine ya Syria - ikiwemo Homs na Hama - imetangaza mgomo baada ya makabiliano na maafisa wa usalama pamoja na wanaomuunga mkono Rais Bashar al-Assad mapema wiki hii.
'Ukatili'
" Hadi pale vikosi vya Syria vitakapositisha mashambulio na ukatili ambayo sio tu yanawaumiza raia wake wenyewe bali hata kuzidisha mapigano katika mpaka, basi tutaona machafuko yakiongezeka katika eneo hilo."
Clinton pia alisisitiza wito wa serikali ya Marekani kwamba Rais Assad atekeleze mabadiliko aliyoahidi au ajiuzulu.
No comments:
Post a Comment