Sunday, 19 June 2011



MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFURAHISHWA NA WAWEKEZAJI



Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kwamba Serikali imefurahishwa na nia ya Wawekezaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Bahari ya SMART TEC SOLUTION ya Uingereza ya kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar. Akizungumza na Uongozi wa Kampuni hiyo ulioongozwa na Mkurugenzi Husein Abdulkadir ambao umeonana na Makamo wa Pili Ofisini kwake Vuga Zanzibar. Makamo wa Pili amesema Serikali imekuwa ikitafuta Wawekezaji kutoka katika kila Pemba Dunia


kuja kuweka hivyo haioni sababu ya Wawekezaji hao kufuata taratibu hizo kwa kupitia Mamlaka ya Uwekezaji (ZIPA) kwa lengo la kupata maelekezo ya kisheria ya Uwekezaji na kuwaahidi kuwa Serikali inawaunga mkono. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe huo umesema kampuni yao ikipata ridhaa ya kuwekeza mitambo ya kisasa ya Internet yenye mwendo mkubwa itakayoweza kutumika nchi nzima kwa urahisi na kwa gharama nafuu. Amesema mtandao huo utasaidia kuboresha mawasiliano katika Taasisi za Serikali na zile za binafsi.

No comments:

Post a Comment